Search This Blog

Tuesday, July 30, 2013

PHOTOS: GONZALO HIGUAIN NA PEPE REINA WALIVYOTAMBULISHWA KUITUMIKIA NAPOLI KABLA YA MCHEZO DHIDI YA GALATASARY


Argentine striker striker Gonzalo Higuain
Argentine striker striker Gonzalo Higuain


Big money: Higuain was on the verge of joining Arsenal before a £34.5million move to Italy
Argentine striker Gonzalo HiguainHiguain salutes the Napoli cheering fans


SAKATA LA UHAMISHO WA FABREGAS: KWANINI BADO KUNA NAFASI FINYU KWA MAN UNITED KUWEZA KUMSAJILI CESC FABREGAS


Matendo, kawaida huwa yanaongea kwa sauti kubwa kuliko maneno. Japokuwa FC Barcelona imeshatoa kali kadhaa kwamba kiungo anayetakiwa na Manchester United, Cesc Fabregas, lakini ujumbe unaotolewa na klabu hiyo ya Catalunya unaweza usiwe na sauti kubwa, lakini wenyewe wameweka wazi Cesc hauzwi kwa bei yoyote. 


United tayari wametuma ofa mbili kwa ajili ya kumsaini nahodha wa zamani wa Arsenal na manager David Moyes alikaririwa hivi karibuni mapema wiki hii kwamba mazungumzo yalikuwa yanaendelea, akitumaini kwamba boss mpya wa Barca Gerardo Martino angeweza kuwa anataka kumuuza kiungo huyo mwenye miaka 26 kwa fedha nyingi kadri iwezekanvyo. Lakini hilo sidhani litaweza kuwa. 

Alipoulizwa Ijumaa iliyopita kuhusu uwezekano wa kumuuza Cesc wakati akitambulishwa, Martino alijibu: "Sitotaka kuingilia masuala ya kifedha ya klabu, lakini klabu tayari imeshakataa ofa mbili na nitaikataa ya tatu."

Kama hiyo haitoshi, makamu wa raisi wa klabu Josep Maria Bartomeu akaongeza kwamba;"Hatufikirii kabisa kumuuza Cesc, hatukwazwi na United kuendelea kumtaka mchezaji, tunajivunia kuona wachezaji wetu wanawavutia timu nyingine, lakini tuna furaha kuwa nae hapa. Ofa yoyote tutakayopokea, mchezaji huyu hauzwi."

Hivyo wakati mchezaji husika akiwa anaonekana kuchoshwa kwa kupigwa benchi mara nyingi na pia kuchezeshwa katika nafasi tofauti kwa klabu hiyo ambayo amekuwa akiisapoti, hataki kuondoka Barcelona. "Nataka kubaki Barca milele," kiungo huyo alikaririwa akisema mwezi wa pili mwaka huu, ingawa miezi miwili baadae alizomewa na mashabiki wake wa Barcelona wakati wa mchezo wa nusu fainali ya kombe la mabingwa wa ulaya, lakini bado alisema matamanio yake ni kubaki na kufanikiwa akiwa na Barca. "Cesc ana furaha na anataka kubaki hapa," mchezaji mwenzie na rafiki Gerard Pique alisema hivi karibuni, wakati boss wa zamani wa timu hiyo Tito Vilanova aliongeza mapema mwezi huu kabla ya kujiuzulu: "Ninafahamu kwamba tumepokea ofa, lakini mchezaji mwenyewe anataka kubaki."

Na Barca wanataka kuendelea kuwa na Cesc, huku Xavi akionyesha dalili za kuanza kuchoka na kucheza mechi mbili kwa wiki bila kuonyesha dalili za kuchoka. Pia Thiago Alcantara tayari ameondoka kwenda Bayern, Fabregas anaweza kupata muda mzuri wa kucheza kwenye kiungo kuanzia msimu ujao.

Lakini pia ujio wa Neymar unamaanisha Cesc atapata nafasi kidogo kucheza kwenye nafasi ya nyuma ya mshambuliaji, lakini kuondoka kwa Thiago ambaye alikuwa kama mbadala wa Xavi na Andres Iniesta katika kiungo - hivyo anaweza kuanza michezo mingi msimu ujao. Ikiwa watamuacha aondoke itabidi Barca waingie sokoni kutafuta mchezaji kama yeye au wampandishe kinda kutoka La Masia - na kuna wachezaji wachache wanaofanana nae.

Ingekuwa Thiago bado yupo Nou Camp, Barca wangeweza kumuuza Cesc na kuweka imani yao kwa Thiago, lakini baada ya kinda huyo kwenda kuungana na Guardiola, Fabregas sasa ni muhimu zaidi kwenye timu kuliko ilivyokuwa misimu uliyopita - Barca wamekuwa na utaratibu mzuri wa kupunguza deni lao, hivyo hawahitaji kuuza mchezaji ili kuweka hesabu za vitabu sawa. Lakini pia timu hiyo inasaka mabeki wa daraja la dunia hili kuimarisha nafasi ya ulinzi ambayo imeonekana kuwa dhaifu hivi karibuni, hivyo pia wanaweza wakamuuza Cesc ili kujiwezesha kutoa dau zuri ambalo litawawezesha kutoa ofa isiyokuwa rahisi kuikataa kwa aidha Chelsea wakiwa na nia ya kumsaini David Luiz, Dortmund kwa ajili ya saini ya Hummels au kwa PSG kwa ajili ya kumsajili Thiago Silva. 


Hivyo United bado wanaweza wakawa na nafasi japo finyu kuweza kumsajili kiungo huyo.

Monday, July 29, 2013

TAIFA STARS ILIVYOREJEA DAR ES SALAAM KWA UNYONGE - IKITOKEA KAMPALA KUPITIA KILIMANJARO


















KUTANA NA KINDA LA BURKINA FASO LILOMKUNA MOURINHO KWENYE PRE SEASON YA CHELSEA - AKIWA BADO SIO MCHEZAJI WA CHELSEA

Kinda la Burkina Faso Bertrand Traore ni mmoja wa makinda waliomvutia sana kocha wa Chelsea Jose Mourinho katika mechi za maandalizi ya msimu mpya huko barani Asia. 

Kwa sababu ya kanuni za usajili mchezaji huyo sio mchezaji rasmi wa The Blues mpaka atakapotimiza miaka 18 mnamo tarehe 6 September, hapo ndipo anaweza kusaini mkataba wa kuitumikia Chelsea.
Wiki hii katika mechi ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya  Malaysia XI alifunga bao zuri sana na akaongeza bao jingine katika ushindi wa 8-1 dhidi ya Indonesia All Stars.

"Ni kijana mdogo, lakini nina uhakika atakuja kuwa na umuhimu sana ndani ya kikosi cha Chelsea cha baadae," mchezaji mwenzie Gary Cahill alisema.

Traore alikuwa sehemu ya kikosi cha Burkina Faso kilichoshiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mwaka 2012 zilizofanyika Equatorial Guinea na Gabon - alicheza katika mechi aliyotokea benchi dhidi ya Sudan katika mchezo wa makundi.

Cahill anasema Traore sio muoga na anajiamini sana akiwa mazoezini akicheza na wachezaji wakubwa wa kikosi cha kwanza. 

"Ameweza kuingia vizuri kwenye timu ya wakubwa. Amezoea. Ni mapema sana kusema yupo tayari kucheza kwenye level ya juu, itakuwa sio vizuri akijiamini kupita kiasi." - Cahil

Traore hakuitwa na kocha Paul Put kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la mataifa huru ya Afrika mapema mwaka huu huko Afrika ya Kusini, ambapo timu yake ilienda na kushika nafasi ya pili nyuma ya Nigeria. Lakini amekuwemo katika kikosi cha sasa ambacho kipo katika nafasi nzuri ya kufuzu kuingia kwenye hatua ya mtoano ya michuano ya kufuzu kombe la dunia. 


Mapema January 2011, Traore alikaririwa akiongea na kipindi cha Fast Track cha BBC akisema; "Nataka kucheza kwenye kikosi cha kwanza Chelsea, nataka kucheza kwenye Champions league na timu zenye majina makubwa.

"Nataka kucheza kila mechi ya timu ya Chelsea na huko mbeleni ningependa kuja kuwa mchezaji bora kutoka Afrika kuichezea Chelsea."

MCHEZAJI WA ZAMANI WA BIRMINGHAM BENITEZ 'CHUCHO' AFARIKI DUNIA KWA MSHTUKO WA MOYO

Mchezaji wa zamani wa Birmingham Christian Benitez amefariki dunia leo hii akiwa na miaka  27.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ecuador maarufu kama   “Chucho”, mwezi uliopita tu alijiunga na klabu ya mashariki ya mbali ya El Jaish kwa ada ya uhamisho wa £10million.

Benitez, ambaye alikuwa akitakiwa na Tottenham, aliwahi kucheza kwa mkopo Birmigham katika msimu wa 2009-10.


Muda mchache uliopita chama cha soka cha Ecuador kimetoa taarifa rasmi na kusema 'Chucho' kutoka na mshtuko wa moyo.

BREAKING NEWS: MONACO YATHIBITISHA MANCHESTER UNITED IMEWAPA OFA YA KUMSAJILI LUIS NANI

Matajiri wapya katika soko la usajili barani ulaya klabu ya AS Monaco imesema kwamba walipewa ofa ya kumnunua winga wa klabu ya Manchester United Nani.

Winga huyo wa timu ya taifa ya Ureno amekuwa njia panda kujua hatma yake ndani ya Old Trafford kabla ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mpaka sasa chini ya manager mpya David Moyes. 

Billionea anayemiliki klabu ya Monaco - Vadim Vasilyev amekiri kwamba United walimpa ofa ya kumsajili  Nani.
Alisema: “Nani tulipewa ofa kumnunua. Ni mchezaji mzuri, lakini hakujawahi kuwa na mazungumo mpaka sasa.”
Monaco wamekuwa na vurugu sana kwenye soko la usajili hivi karibuni, wakiwasajili wachezaji kama Falcao, James Rodriguez  Joao Moutinho kwa bei mbaya sana.

HIZI NDIO SABABU KWANINI YANGA INAPINGA MKATABA WA KAMATI YA LIGI/TFF NA AZAM MEDIA KUONYESHWA KWA LIGI KUU KWENYE TV



















Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji (katikati) akiongea na waanidishi wa habari, Makamu mwenyekiti Clement Sanga (kushoto) na mjumbe wa kamati ya utendaji Mark Anthony (kulia)






















Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu  kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari: 
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.

Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF)  iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina  mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:

1. BODI YA TPL

1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe  ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.

1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.

1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.

2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA

2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani. 

2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie  urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.

2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania  watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.

2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa: 

2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi; 

2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama; 

2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.

3. MIGOGORO YA MASLAHI

3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na  kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.

3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira  wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.

3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.

4. KUTOKUWA NA UWAZI

4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari,  na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).

4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.

5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA 

5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia  kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."

5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji  wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo 
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.

Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA  Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji)  walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.

Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.

Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013

MJADALA: JE NI SAHIHI KWA VILABU VYOTE VYA LIGI KUU YA TANZANIA KULIPWA SAWA KUTOKANA NA MAPATO YA KUUZA HAKI ZA MATANGAZO YA TV?


Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao itaonyeshwa kupitia kituo cha Televison cha Azam TV baada ya kamati ya ligi kwa niaba ya vilabu kuingia mkataba wa mabilioni na kampuni ya Azam Media ili kurusha matangazo ya mechi hizo za Ligi kuu kuanzia msimu ujao. 

Kwa mujibu wa mkataba huo vilabu vyote vinavyoshiriki kwenye ligi hiyo vitapokea mgawo sawa wa mapato ya uuzwaji wa haki za matangazo ya Television bila ukubwa wala udogo wa klabu husika. Yanga tayari wameshapinga suala hilo la kulipwa sawa na vilabu vingine - JE Wewe kama Mdau wa soka/michezo kwa ujumla una maoni gani kuhusu suala? TUJADILI

TAIFA STARS WALIVYOONDOKA KWA MAJONZI JIJINI KAMPALA BAADA YA KUTOLEWA KWENYE CHAN





KOCHA WA SIMBA MFARANSA PATRICK LEIWIG KURUDI BONGO KUFUNDISHA SOKA

Aliyekuwa kocha wa Simba mfaransa Patrick Leiwig anatarajia kutua nchini kurudi kufundisha soka katika klabu ya African Lyon.

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha habari kilicho karibu na African Lyon ni kwamba klabu hiyo kwa sasa ipo kwenye mazungumzo mazito na kocha huyo aliyebobea katika kukuza vipaji vya wachezaji makinda.

"African Lyon pamoja na kushuka daraja lakini ni timu ambayo inafanya mambo yake kwa kuangalia mbele zaidi. Sasa wameamua kuwekeza zaidi kwenye timu zao za vijana na ndio maana wanaamua kumchukua kocha ambaye ana uzoefu mkubwa wa kukuza vipaji vya wachezaji makinda. 

"Mpaka sasa mazungumzo yanaendelea vizuri na siku chache zijazo tutegemee kumuona Leiwig akitua Bongo kuja kuiongoza African Lyon," kilikaririwa chanzo hicho cha habari.

MWANARIADHA WA KENYA NUSURA WAKATI AKIKIMBIA KWENYE MASHINDANO - AZIRAI BAADA YA KUMALIZA MBIO


Mwanariadha wa Kenya wa mbio za masafa marefu Irine Chebet Cheptai amekimbizwa hospitalini baada ya kuzirai katika mbio za uwanja wa Olimpiki.

Cheptai ambaye alikuwa kuwa mmoja wa wanariadha walioshiriki katika mbio za mita elfu tatu alizirai muda mfupi baada ya kumaliza mbio hizo ambapo alimaliza katika nafasi ya kumi na moja na kuweka muda wake kasi zaidi katika mbio hizo wa dakika nane na sekunde ishirini.

Madaktari waliokuwa uwanjani walimtibu mwanariadha huyo aliyekuwa amepoteza fahamu kabla ya kumkimbiza hospitalini kwa machela.

Ripoti zinasema Cheptai hatimaye alipata fahamu akipokea matibabu hospitalini.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na moja hushiriki katika mbio za mita elfu tano na mwaka huu tayari ameshiriki katika mashindano mawili ya dunia ya IAAF Diamond League.

Mwezi Mei mwaka huu mjini Shanghai, Cheptai aliandikisha muda wa dakika kumi na nne sekunde hamsini nukta tisa tisa, muda ambao ndio bora zaidi aliouandikisha katika mbio hizo.

Sunday, July 28, 2013

MAKALA: UDHAIFU WA LA LIGA - UIMARA WA LIGI KUU YA ENGLAND - NA KWANINI YANGA WANAWEZA KUWA SAHIHI KUKATAA DILI LA KUONYESHA MECHI ZA LIGI KUU KWENYE TV



Hili haliwezi kuja na mshtuko kwa mtu yoyote anayefuatilia ligi kuu ya Hispania kwa miaka kadhaa iliyopita, lakini La Liga imejitengenezea mfumo ambao taratibu unaiua ligi hiyo. Hivi karibuni wakati nchi ikiingia katika kipindi cha anguko la uchumi lilosababisha madeni makubwa na upungufu mkubwa wa ajira, pia klabu kadhaa za soka za nchi hiyo zimeingia kwenye matatizo ya kifedha yanayotishia uhai wao kwenye ramani ya soka.

Lakini pamoja uongozi mbovu na mipango tasa ya maendeleo ilyonayo baadhi ya vilabu, moja ya sababu kubwa ya vilabu vya Hispania kuwa kwenye hali mbaya ya uchumi imeletwa na namna wanavyojadili mikataba yao ya kuuza haki za matangazo ya TV.

Tofauti na Premier League, Serie A, Bundesliga na Ligue 1, hata ligi kubwa michezo mengine huko Amerika ya Kaskazini kama vile   (NFL, NBA, MLB, NHL), La Liga ni tofauti sana - klabu zinafanya biashara ya kuuza haki za matangazo ya TV binafsi - kila timu kimpango wake. Mfumo huu unafanya kazi kwa baadhi ya vilabu nchini Spain - klabu mbili, Real Madrid na FC Barcelona, klabu kubwa duniani ambazo zinatajwa kuvuna kiasi kinachofikia $180 million kwa mwaka kutoka dili za mauzo ya haki za matangazo ya TV ambazo wanajadili wao binafsi.

Lakini ukilinganisha namba hizi na zile wanazopata klabu inayofuatia kupata fedha nyingi ambayo ilishika nafasi ya 3 msimu uliopita, Atletico Madrid kunakuwa na pengo kubwa sana. Atletico ilipokea kiasi cha $61 million kutoka kwenye mauzo ya haki za TV. Kutokea hapo namba za kiasi cha fedha wanachopkea vilabu vingine zinazidi kwenda chini; Rayo Vallecano ilimaliza nafasi ya nane msimu uliopita ilipata kiasi cha $18 million kutoka kwenye dili za haki za matangazo ya TV, wakati timu uliyoshika nafasi ya 15 Granada iliweka kibindoni $16 million - fedha ndogo kuliko anayodaiwa Lionel Messi na serikali ya Spain kwa kukwepa kodi. 

Jambo ambalo lilipelekea kupata ahueni kwa wengi wiki baada ya serikali ya nchi hiyo kusema kwamba itasukuma haraka mchakato wa kupata sheria mpya mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka huu - sheria ambayo itaipa Liga de Futbol Profesional (LFP), Chama kinachosimamia ligi za soka za Spain - mamlaka ya kuweka mfumo wa ugawanyaji sawa wa mapato ya haki za Television kwa namna inavyofanyika kwenye ligi nyingine kubwa duniani. Serikali pia itafanya kazi na LFP katika kuhakikisha vilabu vinalipa kiasi cha   $1.3 billion mpaka 2016 ili kupunguza deni wanalodaiwa, wakitoa amri kwa vilabu 42 vinavyoshiriki kwenye La Liga na Segunda kukata matumizi yao kwa kiasi cha $130 million msimu ujao. Hii ni hatua nzuri ambayo italeta afya ya ushindani katika moja ya ligi bora duniani - ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikitawaliwa na vilabu viwili Real na Barca. 

Premier League ndio mfano mkuu wa namna mgawanyo wa kiuchumi unavyofanyika kutokana na fedha inayopatikana kupitia uuzwaji wa haki za matangazo ya TV. Ligi hiyo imeendelea kuwa maarufu kuliko zote duniani - pia ndio mfano mzuri wa namna vilabu vyote vinavyoweza kunufaika na fedha za kutoka kwenye matangazo ya TV - kiasi cha kuchafanya hata timu inayoshuka daraja inufaike kwa kiasi kikubwa kama ilivyo kwa bingwa. Msimu uliopita, Queens Park Rangers, ambao wameshuka daraja, walipata fedha nyingi za kutoka kwenye dili za haki za matangazo ya TV kuliko zile walizopata Bayern Munich na Borrusia Dortmund ukichanganya. Tena kwa mwaka huu fedha hizo zinaweza kuongezeka kwa timu nyingine itakayofuata mkondo wa QPR kwa sababu Premier League inatagemea kuingiza zaidi ya  $8 billion kutoka kwenye uuzwaji wa haki za matangazo ya TV katika kipindi cha miaka mitatu. 

Mfumo ambao La Liga wanataka kuondokana nao nahisi unaweza ukaja hapa Tanzania. Hivi karibuni kamati ya ligi imeingia mkataba na Azam Media Group kurusha matangazo ya mechi za Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa mkataba ambao utafanya vilabu vyote vinashoriki ligi kupata mgawanyo sawa wa mapato. Lakini baada ya hilo kufanyika zimeibuka taarifa kwamba klabu bingwa ya Tanzania Yanga imekataa kuafikiana na mpango huo, ikitoa sababu kwamba yenyewe ni klabu kubwa haiwezi kulipwa fedha sawa na timu nyingine (Yale yale ya FC Barcelona na Real Madrid), lakini pia wakatoa sababu kwamba hakukuwa na utangazaji wa tenda ya dili hilo kwa makampuni mengine?

Yanga wanaweza kuwa sawa kabisa kwenye sababu zao walizotoa - hasa hili kutokukubali kulipwa sawa na vilabu vingine. Kivipi? Ngoja tuangalie mfano wa ligi kuu ya England.

Mgawanyo wa mapato yanayotokana na mauzo ya haki za matangazo ya TV wa ligi kuu ya England upo kama ifuatavyo.

* Asilimia 50 ya fedha zote zinazopatikana kutoka kwenye mauzo ya haki za matangazo ya TV - hugawanywa sawa kwa vilabu vyote - yaani kama imepatikana millioni 10 basi kila timu itapa laki 5 miongoni mwa vilabu 20.

*Asilimia 25 - Hugawanya kutokana na kiwango cha timu kwenye msimamo wa ligi. Kwa maana ya mshindi wa kwanza wa ligi lazima apate kiasi kikubwa kuliko aliyeshika nafasi ya mwisho. Hii ni inaleta hali kushindana zaidi kwenye ligi kwa maana ya timu kushindania kupata mgawo mkubwa kwa kushika nafasi za juu kwenye ligi.

*Asilimia 25 iliyobakia inagawanywa kulingana na uonyeshwaji wa mechi za vilabu husika. Kwa sababu sio mechi zote zinazoonyeshwa live. Hivyo vilabu hupata mgawo wa hizi asilimia 25 kutokana na namna mechi zao zilivyooneshwa kwenye TV.

Huu ndio mfumo sahihi ambao unaifanya ligi kuu ya England kuwa mfano wa kuigwa - unaifanya ligi hiyo kuwa na ushindani mkubwa. Tanzania inapaswa tufuate mfumo huu katika hili suala la haki za matangazo ya Television.

By Aidan Seif Charlie

VIDEO: ANGALIA NAMNA BAYERN MUNICH WALIVYOPIGWA 4-2 NA DORTMUND KATIKA MECHI YA KUFUNGUA MSIMU WA BUNDESLIGA

Dortmund imeifunga Bayern Munich 4-2 katika mchezo wa Supercup uliochezwa leo.


[FutbolHD.ru] Borussia Dortmund 4-2 Bayern... by all-goals

HIVI NDIVYO TAIFA STARS ILIVYONYOLEWA NA UGANDA THE CRANES NA KUSHINDA KWENDA CHAN

Wachezaji wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na Uganda Cranes wakiingia uwanjani tayari kwa kuanza mechi yao ya kufuzu kucheza Chan iliyofanyika kwenye uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala.


Kikosi cha timu ya taifa ya Uganda 'Uganda Cranes'




Mchezaji wa Taifa Stars Aggrey Morris (katikati) akiwania mpira huku akizongwa na mabeki wa Uganda Cranes.Taifa Stars inadhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager.



Amri Kiemba akipongezwa na Mrisho Ngasa/ Aboubakar Salum 'Sure Boy' baada ya kushinda bao la kusawazisha dhidi ya Uganda Cranes



Washabiki wa Taifa Stars wakishangilia goli la kusawazisha..



Kiemba







HATIMAYE TAIFA STARS WATOLEWA CHAN - WAPIGWA 3-1 NA UGANDA THE CRANES


Tanzania (Taifa Stars) imeshindwa kufuzu Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kwa mara ya pili mfululizo baada ya leo (Julai 27 mwaka huu) kufungwa mabao 3-1 na Uganda Cranes, hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 4-1.

Stars ambayo ilicheza fainali za kwanza zilizofanyika Ivory Coast mwaka 2009 ilimaliza kipindi cha kwanza katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole nje kidogo ya Kampala ikiwa sare ya bao 1-1.

Wenyeji ndiyo walioanza kufunga bao dakika ya saba katika mechi hiyo iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka Madagascar. Frank Kalanda alifunga bao hilo akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Tanzania.

Bao hilo halikuonekana kuichangaza Taifa Stars, kwani ilitulia na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18 mfungaji akiwa Amri Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye kona ya eneo la mita 18.

Dakika ya 32 nusura Taifa Stars ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Mrisho Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa HAmza Muwonge uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki wa Uganda Cranes.

Mabao mengine ya Uganda Cranes yalifungwa dakika ya 48 kupitia kwa Brian Majwega na lingine dakika ya 63 mfungaji akiwa tenda Kalanda kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokonywa mpira wakati akiwa katika nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.

Kocha Kim Poulsen alifanya mabadiliko dakika ya 43 kwa kumuingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo aliyeumia, na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruni Chanongo na Vincent Barnabas badala ya David Luhende na John Bocco. Hata hivyo mabadiliko hayo hayakubadili matokeo ya mchezo.
Kikosi cha Stars kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.

Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani kesho (Julai 28 mwaka huu) saa 4 usiku kwa ndege ya PrecisionAir.