Search This Blog
Monday, July 29, 2013
MJADALA: JE NI SAHIHI KWA VILABU VYOTE VYA LIGI KUU YA TANZANIA KULIPWA SAWA KUTOKANA NA MAPATO YA KUUZA HAKI ZA MATANGAZO YA TV?
Ligi kuu ya Tanzania Bara msimu ujao itaonyeshwa kupitia kituo cha Televison cha Azam TV baada ya kamati ya ligi kwa niaba ya vilabu kuingia mkataba wa mabilioni na kampuni ya Azam Media ili kurusha matangazo ya mechi hizo za Ligi kuu kuanzia msimu ujao.
Kwa mujibu wa mkataba huo vilabu vyote vinavyoshiriki kwenye ligi hiyo vitapokea mgawo sawa wa mapato ya uuzwaji wa haki za matangazo ya Television bila ukubwa wala udogo wa klabu husika. Yanga tayari wameshapinga suala hilo la kulipwa sawa na vilabu vingine - JE Wewe kama Mdau wa soka/michezo kwa ujumla una maoni gani kuhusu suala? TUJADILI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hicho Ni kitu sahihi....ukiacha kwamba wanapokea sawa na hizo timu ndogo...sh million 100 kwa yanga Ni mapato ya mechi moja Tu kama wakicheza mechi yenye ushindani na either simba au azam au mtibwa...lakini to be honest bajeti ya yanga na hizo timu nyingine ndogo hazifanani kwa hiyo itakuwa Ni unfair kwa timu kama hiyo...economically Kuna vitu vingine ni market regulated yaani huwezi kulazimisha bei ya mchele ifanane na mahindi eti kwa kuwa zote ni nafaka na zinatumiwa sana na wananchi nooo... That's a different thing zaidi utawaonea wakulima wa mpunga na
ReplyDeleteMi binafsi sioni kama ni sahihi kwa timu zote kupata mgao sawa.Hata ukianza kuangalia maandalizi ya timu kubwa za simba na yanga hayafanani na ya timu ndogo.Kwa ujumla gharama za uendeshaji wa timu kubwa ni tofauti kbs na wa timu ndogo.Pili mapato ya timu kama yanga huwezi fananisha na timu kama rhino.Mechi ya yanga na azam inaingiza mil 236.Unategemea azam akicheza na timu nyingine anaweza kupata hz.
ReplyDeleteyanga wabinafsi tu,tunataka changamoto ya mpira,wanatakiwa wangalie vyanzo vyao vingine vya mapato.
ReplyDeleteNi negotiations tu nafikr kweli hao mamwinyi(simba na yanga)wana haki ya kulalamika kwani wao wanauza,ila wasizuie mwanzo mzuri huo wajadiliane na TFF na AZAM TV waweke mambu sawa ligi yetu ikue.
ReplyDeletePasu kwa pasu ndio mpango wenyewe.Iwapo tupo serious na kutaka ligi iliyo bora ukanda huu wa east and central Africa, timu kubwa kama Yanga zikubali ushindani.Hatuwezi kuwa na ligi timu mbili halafu tutegemee maendeleo ya soka!!Timu kama Azam, Coast, Mtibwa zimeanza kunogesha ligi! Viongozi wa Simba na yanga waache mawazo mgando!!
ReplyDeleteSababu walizoeleza Yanga kwa nini hawataki kulipwa sawa na vilabu vingine ni za kitoto, ni kweli wao ni klabu kubwa ni sawa na Simba lakini lazima wakumbuke Azam Media group hawadhamini vilabu wao wanadhamini ligi sasa labda watuambie hao vilabu vikubwa kama wanaweza kucheza ligi bila hivyo vilabu vingine wanavyoviita vidogo.
ReplyDeleteNa kingine watwambie mgawo wanaopata kutoka Vodacom je ni tofauti na mgawo wanaopata vilabu vingine? Je vipi kuhusu gate collection wanapocheza na hivyo vilabu vidogo wanagawana sawa au Yanga kwa sababu ni klabu kubwa wao wanapata zaidi? Na kama wanapata sawa kote huko kwa nini hizi za Azam wanataka wapewe tofauti na wengine?
Wao kama ni klabu kubwa na wanaamini wanaweza kuingiza hela kutokana na ukubwa wao si watafute wadhamini wengine kama vile walivyopata kutoka TBL. Yanga wanatakiwa wakubali hicho kiasi ili Azam waonyeshe hiyo ligi.
Suala la kwamba tenda haikuwa wazi mimi sina uhakika nalo lakini TFF wenyewe wanasema dau la Azam ndo lilikuwa kubwa zaidi kuliko la supersport sasa wao walitaka supersport wapewe eti tu kwa sababu wanaoenekana sehemu kubwa Afrika kwa Yanga wanafanya biashara gani nje ya Tanzania wanataka waonekana nje? Wao si ni wa hapa hapa tu.
Nafikiri ishu hapa ni dau lenyewe la kibiashara maana huu si udhamini..kama kuna sehemu Timu ianona inaweza kunufaika zaidi ya hiki basi wana haki ya msingi kulalamika na kuchukua hatua.. lakini na taarifa za TFF si za kuamika sana maana kuna taarifa ambazo huwa wanatoa mwisho wa siku zinakuja kuonekana si sahihi (na mara nyingi huwa wanajificha kwenye kichaka cha kusema ooh FIFA mara eeh mfano hai ni sakata la uchaguzi). Ukiona mti unapigwa mawe ujue una matunda..at the end of the day Yanga wataonekana wana hoja ..and that's way tunadadili.
Deleteninafikiri uendeshaji wa vilabu pamoja na gharama zinazohusika zinatofautiana sana kutoka timu ndogo hadi kubwa. mwelekeo wa Yanga (ambao naamini wataungwa mkono na Simba) una mantiki. mechi inayocheza Yanga na klab nyingine kama ilivyo kwa Simba inalipa kibiashara kuliko kama hizi timu 'ndogo' zikicheza zenyewe wa zenyewe. kwa mantiki hii kugawanya mapato sawa ni kuzinufaisha timu 'ndogo' na kuziumiza timu 'kubwa'. kuna umuhimu wa kufidia gharama wanazotumia timu 'kubwa' kuendesha timu zao vinginevyo haina haja ya mechi za timu 'kubwa' kuoneshwa kwenye hiyo TV na badala yake waviachie vilabu 'vikubwa' vijadiliane na Vituo vingine vya TV kupata maslahi zaidi.
ReplyDeleteninafikiri uendeshaji wa vilabu pamoja na gharama zinazohusika zinatofautiana sana kutoka timu ndogo hadi kubwa. mwelekeo wa Yanga (ambao naamini wataungwa mkono na Simba) una mantiki. mechi inayocheza Yanga na klab nyingine kama ilivyo kwa Simba inalipa kibiashara kuliko kama hizi timu 'ndogo' zikicheza zenyewe wa zenyewe. kwa mantiki hii kugawanya mapato sawa ni kuzinufaisha timu 'ndogo' na kuziumiza timu 'kubwa'. kuna umuhimu wa kufidia gharama wanazotumia timu 'kubwa' kuendesha timu zao vinginevyo haina haja ya mechi za timu 'kubwa' kuoneshwa kwenye hiyo TV na badala yake waviachie vilabu 'vikubwa' vijadiliane na Vituo vingine vya TV kupata maslahi zaidi.
ReplyDeleteKwanza Yanga wako sahihi sana, huu sio wakati wa kupelekwa pelekwa, dunia ni kijiji kila kitu kinachoendelea duniani kinajulikana na ukweli unaonekana wazi. milioni 100 kwa Yanga na Simba ni ndogo sana ukichukulia kila mechi Yanga ikicheza inaingiza zaidi ya milioni 20 kwa kipato cha chini na zaidi ya shilingi milioni 100 kwa kipato cha juu, kwa tunavyojijua watz zikianza kuonyeshwa kipato kitapungua lazima sababu watu hawataenda mpirani watabaki majumbani wakila raha na familia zao. sasa lazima hili gap lifidiwe na muonyeshaji. tuwe wakweli target ya mdhamini ni yanga na samba, na wala sio timu zingine sasa watakuwaje sawa? alijaribu kuonyesha mechi msimu uliopita hakuna mtu aliyekuwa anajali kuona labda ikukute bar huna issue ndo ulikuwa unaangalia ambapo ulikuwa unaweza kuhesabu watazamaji uwanjani. na ilifikia time timu zililalamika kuwa hawajalipwa na yeye alishindwa kulipa sababu alikosa audience haikumlipa. tatizo rage analeta siasa kwenye vitu serious, tuwaache Yanga waendelee na mipango yao wanaweza kuleta mabadiliko hawajamaa, nawakubali sana. Udahamini utangazwe watu waujadili kila mtu apate anachostahili
ReplyDeletekwakuanziaaa mie naona ni sawa mgao uwe sawa,kwasababu hata km 2takataa ukweli utabaki pale pale kua vilabu vingi hapa bongo vina hali mbayaaa sn kifedha.vinashindwa hata kuwalipa wachezaji wao....vilabu vinashindwa hata maji ya kunywa,,,wengi mna wadogo zenu wanachezeaaa vilabu vingine mnajuaaa kua wanacheza 2,,,kwakuaaa fani yao ni mpira ila hakunaaa wanachokipata,,,,hivyo kwa awamu ya kwanza km hii ni vizuri kufanya hivyo ili kuviwezeshaaa vilabu vidogo ili viweze kujiendeshaaa hasa ktk malipo ya wachezaji wao....hii ni basic...then baada ya huu mkataba kuisha 2anze sasa swalaa la kuangaliaaaa vigezooo vya vilabu ktk kupataa mgao,,,ila plzz vilabu vya simba,yanga na azam wasipende kua wabinafsi ktk hii km kwelii 2na nia thabiti ktk kutakaa ligi ye2 iwe bora lazima vilabu vyote vijiweze japooo kujiendeshaaa...sio timu za simba na yanga kufurahiaaa kucheza na timu ambazoo wachezaji wao hata swala la kula nakupataa mshahara hawalijuaaaa na 2tegemee kupata timu ya taifa bora,,,au uwezo wakushindana na vilabu km TP-mazembe,,,,,,,km ligi ni dhaifuuu
ReplyDeletesasa ndg yangu Kwenye katiba ya Yanga hakuna sehemu iliyoandikwa kwamba inapaswa kusaidia vilabu vidovidogo. Kila mtu ale kwa jasho lake. si kazi ya Yanga kulipa mishahara au kugharamia uendeshaji wa timu ndogo ndogo..
DeleteHapa ni biashara Azam TV wanataka kufanya biashara na kama wanataka kuzisaidia timu basi kila timu ipewe haki yake. Wavilipe vilabu kile wanachostahili alafu watoe pesa nyingine kusaidia hizo timu ndogo...najua kwa kuwa hii ni biashara hili la kusaidia timu ndogo Azam TV hawawezi ila wanataka kubeba sifa isiyo yao. Ngoja Yanga iliyojitambua ijitoe alafu uone ni watanzania wangapi watalipia hiyo TV..na kusema ukweli kama na Simba wangeliona hili basi dau lingeongezeka. kujitambua ni vema kuliko kufuata mkumbo..
JIthamini ndipo uthaminiwe
Yanga wapo sahihi, kw sabab kuna suala la timu zte chini ya kamati ya ligi n timu kama taasis binafsi. Lakini kw vile kuonesha ligi ni suala la hatua moja mbele ya maendeleo katika soka letu ni vyema Yanga kama taasisi wakatumia BUSARA kwa msimu huu halafu msimu ujaowakapenyeza hayo ya kwao
ReplyDeletekwanza kabisa naungana na makala ya Aidan Seif, pili mfumo wa uingereza nimeupenda yaani 50% sawa, 25% bingwa na wale wa juu wanaomfuatia na mwisho 25% ya wale wanaoonyeshwa kwa wingi wapate zaidi, Angalizo...yanga wanaposema kuwa wao ni klabu kubwa bila ya kutoa sababu za maana kwenye ishu nzito kama hiyo sio sahihi, pili yanga wanaposema tenda ingetangazwa sio sawa kwa sababu hata hilo dili kuja hapo TFF ni juhudi binafsi za kampuni ya AZAM kuiona fursa na kuitumia kama kulikuwa na matajiri wengine ndani ya yanga mate yanawatoka baada ya kuona AZAM wamewapiga bao nawaomba watulie na wasubiri hiyo fursa ya tenda baada ya mkataba huu kwisha...kwani hao viongozi wa simba na yanga kazi yao kubwa ni kuchukuliana wachezaji kwenye usajili kuhakikisha wanadhoofishana wao kwa wao na timu zikienda kwenye mashindano ya kimataifa zinachemsha, tumieni fursa acheni kupiga makelele na bado mtalia sana AZAM hongereni kwa kuonyesha njia nzuri. Kiyungi Postiga (Mdau wa soka)
ReplyDeleteTANZANIA NI NCHI YA AJABU SANA KILA SIKU MI BINAFSI NALAUMU SANA MEDIA ZETU NAMAANISHA MAGAZETI NA ,TV,REDIO NK,MPIRA UKIWA MBOVU LAWAMA ZOTE KWA TIM KUBWA NADHANI ZINAJULIKANA ILA KWENYE HILI KUNA WAANDISHI BADO WANAJIDAI HAWAONI NA WALA KUJUA UTOFAUTI WA YANGA NATIMU NYINGINE,MI NAONA YANGA WAKO MSAHIHI KABISA KWANI HATA HUYO MDHAMINI ANAJUA KABISA YANGA NASIMBA WAKIKATAA BASI MOJA KWA MOJA HANA BIASHARA HIVO SIONI MNTIKI YA YANGA KUPATASAWA NA TIMU NDOGO NASHANGAA HATA BAADHI YA VIOPNGOZI WA TIMU NDOGO WANASEMA ETI YANGA WASIKAZANIE KUONGEZWA MGAO BALI WATAFUTE VYANZO VINGINE VYA MAPATO KWANI TIMU NDOGO NAZO ZINASHINDWEJE KUTAFUTA HIVO VYANZO ? HEBU TUACHE UTANI YANGA WAPEWE HADHI YAO BWANA KAMA SIMBA HAWAONI UTOFAUTI WAO NA MTIBWA BASI NI WAO ILA WANAOUONA UTOFAUTI BASI TUWAPE HAKI YAO ,NAWASHAURI VIONGOZI WA YANGA WASIKUBALIANE NA UNYONYAJI HUO.
ReplyDeleteYanga wapo sahihi na hata hao azam wanalijua hilo na naamini yanga nasimba wakikataa hata huyo mdhamini atajitoa maana mi siwezi poteza hela yangu ninunue au kulipia azam tv kwa ajili ya rhino cjui mtibwa au mbeya city huo ni uongo hebu tumwogope mung u na tuache unyonyaji hakuna mafanikio ya njia ya mkato azam tv kufanya hivo ni kutafuta shortcut kwenye mafanikio jamani kila mtu ale kwa jasho lake ,hebu wapeni yanga wanachostahili umefika wakati tuwe wakweli na wawazi hebu viongozi wa yanga unyesheni ukomavu wa hilo ili heshima yenu ionekane
ReplyDeleteMi ni shabili wa kweli wa Yanga bt kwa hili yanga hawapo sahihi sababu tukitaka tujenge misingi mizuri ya mpira Tanzania tunatakiwa kuzingatia vigezo na tuache ubaguzi na kuptia m 100 yanga wanaweza tengeneza pesa nyingi. Asante Azam kwa msimamo na asiyetaka usawa mwacheni ile kwake ( mpira mbele mapenzi yafate )
ReplyDeleteKUwa na akili unachozikuzungumza wewe,umajua gharama za timu kama yanga,ushaona kuona mchezaji kasajiliwa dola elfu sabin jkt ruvu si unasikia simba au yanga,unajua mishahra yao
DeleteWewe ni mamluki tu na sio shabiki wa yanga coz shabiki wa yanga hawez kuongea pumba kama zako
Deletemi sioni kama ni fair bcause timu kama yanga kulipwa sawa na rhino fc si kitu cha kawaida sababu bajeti nitofauti hata kama wanacheza ligi moja na hao simba ni kwamba hawana hela ndio maana wamekubali
ReplyDeletemgao hauwezi kuwa sawa kwa timu zote, iyo ni duniani kote. JUVENTUS katika msimu uliopita wa EUFA wameengiza pesa nyingi kuliko timu zote, wamewazidi hadi mabingwa.
ReplyDeletelakini kwa soka la bongo kwa kua timu zingine hazipo vizuri kiuchumi mi nashauri kuwe na ratio au percentage ya gap (tofauti) ili kuzipa timu zisizo na vyanzo vizuri vya mapato kuongeza uchumi wao.
lakini pia timu zitafute wadhamini wao binafsi na wadhamini wa ligi wapate nafasi fulani katika jezi za timu kwa mfano begani.
mimi naona ni sawa bora iwe ivyo tuu maana tim za kibongo ni wasumbufuu sanaa
ReplyDeleteAchilia mbali gharama kubwa wanaotumia klabu kubwa kuanzia kuweka kambi,mishahara ya wachezaji na mambo mengine wanayotumia hizo timu kuna utashi wa kwenda mpirani hasa unapohusu hizi timu kubwa.
ReplyDeleteNi nadra kwenda mechi Rhino na JKT lkn kati ya timu hizo kama zina cheza na hizo timu kubwa utashi ni mkubwa sana.
Kwa wenzetu Spain timu za Barcelona na Real Madrid wanalipwa karibia 50% ya wapato yote ya Tv.
Kwa Yanga wako sahihi kabisa hawawezi kupata mgawo sawa na timu nyingine ndogondogo
Yanga wako sahihi kabisa na pia 2elewe c lazima wa2 wote wakawa na mawazo sawa..enzi za mwalimu kusingekuwa na upinzani wa mkataba nachoomaanisha ni kwamba wakati wa sasa c wakuangalia watu wameamua nn km kilichoamuliwa hakiendani na mipango yenu ni ruksa kukataaa c kupelekeshwa km polisi wanavopelekeshwa na chama tawala...NDO MAANA HATA MAKAZINI HUWEZI MLIPA DIRECTOR SAWA NA MANAGER AMA MKUU WA IDARA FULANI HATA KAMA WOTE WANATEGEMEANA!!!VIVA YOUNG AFRICA USIYUMBISHWE NA TFF WW ANGALIA MASLAI UJAZE BANK
ReplyDeletehao yanga hawako sahihi kabisa kwa maana katika kamati ya league iliyohusika na kutafuta mdhamini walikuwa na mtu anayewakilisha sasa walikuwa wapi kupinga kutoka huko wanakuja kutupigia kelele ifike mahala tuwe tunajua kwenda na muda, walibishia kuvaa nembo yenye red colour saiz wamekuja na hoja ambayo walitakiwa waikatae mapema sana, wanaogopa vilabu vingine vitakuwa na uwezo wa kununua wachezaji na kuboresha timu zao na kuleta upinzani mkali. MSIMU UJAO SIO WA DEZO MAANA HATA TIMU TUNAZIITA NDOGO WATAKUWA NA UWEZO WA KULA NA KULALA VIZURI NA KULIPA WACHEZAJI WAO KWA MDA
ReplyDeleteili kuelewa suala hili chukua mfano huu: we una uwezo wa kuingiza shilingi laki moja kwa mwezi na hicho kipato ndicho kinaendesha familia yako japo ndo ivo hakitoshi, haufanyi jitihada za kuongeza kipato ila unataka kipato kiongezeke kwa familia yako kwa kutaka kipato cha mtu mwingine kiletwe kwako..hapo utafurahi kwa sababu familia yako itakuwa inabebwa.
Deletechukua mfano huu; mtu mwingine anaingiza milioni 1 kwa mwezi na hicho kipato kinaendesha familia yake japo nacho hakitoshi kulingana na familia yenyewe ilivyo.mtu huyu anauwezo wa kuongeza kipato na anafanya jitihada ili kipato kiongezeke lakini anaambiwa akiongeza bidii kipato kikaongezeka basi agawane sawa na huyu ambaye familia yake inaendeshwa kwa laki moja kwa mwezi..katika hili nani atanufaika....ukipata jibu rudi sasa kwenye hoja ya Yanga.
Ukweli suala hili ni tata, ila kwa kuanzia nadhani Yanga wangeridhika ili na vilabu vidogo angalau viweze kujiendesha na kujijenga, hasa ukizingatia wao (Wanaojiita vilabu vikubwa) wana wadhamini wengine. Lakini kwa upande mwengine hakuna hoja ya maana ya kujiita wao ni vilabu vikubwa kwani hakuna jipya wanalolifanya zaidi ya kuliporomosha soka letu, hakuna kikubwa walichokifanya kwenye maendeleo ya soka cha kusema hizi timu kweli ni kubwa zipewe heshima na stahiki ya ukubwa wao, Si ndani ya nchi wala mashindano ya nje..
ReplyDeleteKwa maoni yangu "pasu kwa pasu" (equal ratio) ndio sahihi.. Vilabu vyote vipewe mgao sawa.
Mo de Bebeto
e yanga ukubwa gani mnaoulilia. eti hawataki kuoneshwa kwa sababu mmiliki wa tv ni mmiliki wa azam. huo ushamba. mbona David gill ni alikuwa mtendaji wa Manchester na ana cheo kikubwa UEFA? kwendeni zenu washamba nyie kama hamtaki ligi pia itaoneshwa na wala samba hatokuugeni mkono. Wewe manji kama una hela anzisha basi TV yako.
ReplyDeleteSishangai kwa comment yako kwa sababu hata ukubwa wa vilabu vya Yanga hiyo timu yako huvioni we kweli mbumbumbu. kwa sababu uwezo wako mdogo huwezi hata kuona kile yanga wanachokililia.
DeleteHivi wewe jamaa umepitia chekechea kweli? maana naona mawazo yako ni finyu sana, yaan umeshindwa hata kutaja matamshi sahihi ya timu yako! kweli duniani kuna vilaza. bro/sister ushauri wa bure kwako, achanana hivi vitu ubongo wako ni sawa na wa kuku jike
DeleteMgao sawa, hamna hili suala. Ndo maana hata makazini mtakuwa department 1 but mishahara tofauti. Kwanza hiyo milioni 100 kwa mwaka sawa na kitu kama milioni 8 na laki 3 kwa mwezi, sawa na laki mbili na elf 70 kwa siku. 270,000 kwa siku.hapo faida ni kwa Azam atapata subcribers kibao na wadhamini mbali mbali siku ya kurusha mechi. Wakae chini wajadiliane upya. Kuilipa klabu 270,000 kwa mwezi hata petty cash ya siku haitoshi hiyo.
ReplyDeleteNadhani watu wangepigiwa hesabu ya kiasi ambacho timu itapewa,maana kila mtu anaongea lake kwa kuto elewa kitu,nadhani yanga wapo sahihi kwa kila nukta,ukweli kamati ya muda haiwezi kuingia mkataba mrefu,then watu wa kwenye kamati ndio hao baadhi yao wapo azam,taratibu ilibidi zifuatwe hata tenda inge tangazwa kwani hata startv wangeweza kuingia nao kutaka kuonesha,clouds hari kadhilika,hapo wameibaka haki ya kununua matangazo kwa makampuni mengine.hauwezi ukaipa yanga milion 8 kwa game ni ujinga.......
ReplyDeleteHII YA KWETU NI MPYA!!!!MGAO HAUWEZIKUWA SAWA,WALA YANGA NA SIMBA WASITUMIKE KWA AJILI YA KUZINYANYUA TIMU NDOGO KAZI HIYO IFANYWE NA TFF.YANGA WAKO SAHIHINA WANA VIONGOZI MAKINI.NAMKUMBUKA PROFESSOR WANGU ALIYENIFUNDISHA,WAKATI FULANI ALIKWENDA MAREKANI AKAWAKUTA WAMAREKANI WEUSI HAWANA ELIMU KAMA WAMAREKENI WEUPE,AKAULIZA KULIKONI?AKAJIBIWA KUWA WAMAREKANI WEUSI WANAPENDA SANA PESA KWAHIYO WAO WEUPE WAMEPELEKA PESA NYING KWENYE MICHEZO,KWAHIYO UTAKUTA WAMAREKANI WEUSI WAMEJAA HUKO.NAWAONYA WATANZANIA WENZANGU TUSIKIMBILIE PESA AMBAZO HAZINA MANUFAA NA SISI HATA KAMA MIKATABA NI MIBOVU NA HAINA MASLAHI NA TIMU.HIVI NYIE MNAOUNGA MKONO KAMATITA LIGI MNATOFAUTI GANI NA KUUNGA MKONO MAFISADI WALIOINGIZA NCHI KATIKA MIKATABA MIBOVU NA BILA KUFUATA TARATIBU?YANGA DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
ReplyDeleteNapendekeza mgao sawa kwa wote kwani itasaidia kuinua vilabu vidogo na kuleta ushindani yanga waache ubinafsi huo sio mzuri kwa maendeleo ya mpira wetu wamewekeza sehemu mbalimbali wao sio sawa na totoafrica au transtcamp bwana mgawo sawa ndio mpango mzima.
ReplyDeleteMgao sawa ni kuuza ulichonacho wewe halafu nenda kale na watu wa kwenu kijijini ulikokimbia. Dunia ya sasa mpango mzima ni ubepari masuala yenu ya kijamaa peleka hukooo vijiji vya songambele au gezaulole, mshamba mkubwa wewe!
DeleteMgawo sawa kwa wote ndio mpango mzima.
ReplyDeleteNilishangaa jinsi Rage alivyokimbilia kuusifia mkataba kama huu wa karl peters na chifu mangungo, kwenye issue hii wacha yanga wawe wabinafsi..then mnunue hvyo vishumbuzi muone game ya rhino na orjolo,ruvu na mgambo!!.,hiyo mil 140 ni upuuzi mtupu kwa timu kama yanga
ReplyDeleteMh
ReplyDeleteMimi sijaona hiyo TV ya AZAM, nikiiona nitacomment!
ReplyDeleteTO BE FRANK,YANGA WAKO SAHIHI, NA UKWELI KWAMBA SIMBA NA YANGA NI TIMU KUBWA HAPA TANZANIA,HIVYO WANA WAPENZI,MSHABIKI NA WANACHAMA NCHI NZIMA KWA KUCHEZA KWAO LIGI KUU NI WAZI KWAMBA MAPATO YA VIWANJANI YANA KUWA JUU SANA UKILINGANISHA NA PRISON,KAGERA SUGAR ,JKT-OLJORO NK.HIVYO NI SAHIHI YANGA NA SIMBA KUONGEZEWA MAGO WAO KWA KUWA NA SOKO KUBWA KATIKA BIASHARA YA SOKA LETU,NI MUDA MUAFAKA AZAM MEDIA KULITAFAKARI HILO NA KUCHUKUA HATUA STAHILI KWA MUSTAKABALI WA SOKA LETU HAPA BONGOLAND.
ReplyDeleteHIVI AZAM TV INAPATIKANA CHANNEL NAMBA NGAPI AU KING'AMUZI KIPI INAPATIKANA....?
ReplyDelete