Uongozi wa klabu ya Yanga leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu ya urushwaji wa michezo yake ya Ligi Kuu katika kituo cha luninga cha Azam ambacho kimeingia makubaliano na kamati ya Ligi Kuu kuonyeshwa michezo yote ya ligi kwa kipindi cha miaka miatatu (3).
Akiongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa klabu ya Yanga Yusuf Manji amesema uamuzi wa kamati ya ligi kuingia mkataba na kituo cha Azam Tv bila ya kuwashirikisha wahusika wenyewe ambao ni vilabu vishiriki haukuwa sawa.
Sisi kama klabu ya Yanga tulikaa kikao cha kamati ya utendaji na kuona taratibu za kupewa haki ya matangazo kwa kampuni ya Azam haikua sawa, sisi viongozi wa kalbu ya Yanga hatukushirikishwa katika mchakato huo hivyo tukaona ni vema tuje kwa vyombo vya habari tuulezee umma juu ya maazimio ya kamati ya utendaji.
Ifuatayo ni taarifa kamili kwa vyombo vya habari:
YAH: URUSHWAJI KATIKA TELEVISHENI MICHEZO YA YANGA.
Hivi karibuni, Tanzania Football Federation (TFF) iliunda Tanzania Premier League chini ya Bodi ya mpito Bodi ya TPL ambayo ni msimamizi mpaka hapo Bodi itakayokuwa imechaguliwa kidemokrasia. Bodi hii imeamua peke yake kuingia katika mkataba wa miaka 3 (mitatu) na kampuni inayoitwa Azam Television (ambayo ina mapromota wale wale wanaomiliki Azam Football Club). Makubaliano ambayo Bodi ya TPL inatarajia kuingia na Azam Television, Kamati ya Utendaji ya YANGA inalipinga kwa nguvu zote katika misingi ifuatayo:
1. BODI YA TPL
1.1 Bodi iliyoko sasa hivi ni ya mpito ambayo ilitakiwa kutenguliwa na Bodi iliyochaguliwa kidemokrasia kwa kupitia uchaguzi wa tarehe ……….. mwaka huu na haitakiwi kuingia katika mikataba a miaka mingi wakati inakaribia kuondoka katika ofisi.
1.2 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haikuchaguliwa kidemokrasia.
1.3 Bodi ya TPL iliyoko sasa hivi haina mjumbe hata mmoja aliyeteuliwa kutoka YANGA.
2. UTARATIBU WA DUNIA NZIMA
2.1 Haijawahi kutokea katika ligi ya mpira wa miguu ya kisasa kulazimishwa kwa Klabu inayoshindana katika ligi kuachia haki zake za urushwaji wa michezo zichukuliwe na chombo cha habari cha Klabu ya upinzani.
2.2 Mfumo (undertaking) ambao TPL inataka kuanzisha kwa njia ya kulazimisha mkataba kwa YANGA iachie urushwaji wa michezo yake ya soka yarushwe na Azam TV unatishia sana uwepo wa msingi wa ushindani katika soka ya Tanzania.
2.3 Makubalianokati ya TPL na Azam Television kuhusu utaratibu wa malipo yanasemakwamba Klabu ya YANGA na Klabu zingine zitakazoshiriki katika Ligi Kuu ya Tanzania watapata mgao sawa wa mapato ya urushwaji wa michezo hii, ambayo YANGA inapinga kwa sababu kama inavyofanyika duniani kote kwenye ligi zilizofanikiwa (angalau) kutofautisha mgawanyo wa mapato kati ya timu kufuatana na matokeo ya mwisho wa ligi.
2.4 Kamati ya Utendaji ya YANGA siyo tu haikubaliani na mgawanyo sawa wa mapato ambao hautofautishi kati ya timu ya kwanza katika ligi na timu ya mwisho katika ligi, lakini pia ukosefu wa viwango (premiums) vitakavyolipwa:
2.4.1 Vilabu vya mpira vyenye ufuasi wa washabiki wengi;
2.4.2 Vilabu vya mpira vinavyoendeshwa na Wanachama;
2.4.3 Vilabu vya mpira visivyopata ruzuku kutoka Serikalini n.k.
3. MIGOGORO YA MASLAHI
3.1 Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Mpito ya TPL ni Mkurugenzi mwandamizi wa Makampuni ya Azam na kwa hivyo mazungumzo ya siri kati ya Bodi ya TPL na Azam ni ya kutiliwa mashaka.
3.2 Makampuni ya Azam yana yanashindana kibiashara na makapuni mengi yakiwemo ya utengenezaji wa vinywaji baridi na imeonyesha huko awali inaweka “matakwa maalum” muhimu zaidi kuliko mprira wa miguu, kama vile Azam F.C. hawashiriki katika Kombe la Tusker na kwa hiyo YANGA inakuwa na msimamo kwamba kwa Azam Television kupewa leseni ya kurusha matangazo ya mpira wa miguu inatishia biashara za washiriki wa sasa na wa baadaye wa YANGA.
3.3 Azam na YANGA wana uadui wa kimichezo. Kumbuka, wakati MRISHO NGASSA alipotaka kwenda YANGA, Azam F.C. walimkopesha kwa nguvu kwa Klabu ya Simba! Kwa hiyo YANGA itahatarika kwa matangazo yenye upendeleo kama Azam Television itarusha hewani michezo yake n.k.
4. KUTOKUWA NA UWAZI
4.1 Mkataba wa utangazaji wa miaka mingi unaotaka kuingiwa kati ya TPL na ambao badohaujarushwa Television ya Azam haukushindanishwa na vyombo vingi vya habari, na vyombo ambayo wako tayari kwenye soka havikujulishwa kuhusu fursa hii au walizuiliwa kufikisha mapendekezo yao ya maombi ya haki za kurusha matangazo katika Ligi Kuu (Tanzania Premier League).
4.2 Ukosefu wa uwazi wa TPL unanonyesha kuwa MoU iliyokusudiwa kuwekewa saini na TPL haikufikishwa YANGA kwa ajili ya mapitio ya kisheria, licha ya YANGA kufanya ombi hilo kwaTPL.
5. MAZINGATIO YA KIBIASHARA
5.1 Mamlaka ya kuamua mzozo wowote wa mkataba wa leseni ya utangazaji wa Ligi Kuu (Tanzania Premier Leagu) itakuwa ni Mahakama ya kisheria na siyo FIFA. TPL inasingizia kwamba leseni ya matangazo ambayo inakusudia kufanya kuwa ni maagizo ya FIFA na kwa hiyo YANGA inapaswa kuukubali "lock, stock and barrel."
5.2 TPL inaelezea kimakosa makubaliano ya leseni ya urushaji wa mchezo ya mpira inayotarajia kuingia na Television ya Azam kama "makubaliano ya udhamini" (“sponsorship agreement”) ambayo siyo sahihi, kwa sababu urushaji wa michezo ya mpira wa miguu ni biashara inayotokana na maslahi ya uhusiano na hivyo
wahusika wote ni lazima wazingatie maslahi yao ya kifedha.
Kwa mfano, moja ya vyanzo muhimu vya mapato ya YANGA ni mapato ya kiingilio ya mlangoni yatokanayo na michezo ya mpira wa miguu ambayo urushwaji wa michezo hii itapunguza mapato haya. Kwa wastani michezo ya YANGA Dar es Salaam huingiza makusanyo ya mlangoni shilingi milioni 50 kwa kila mchezo na hata kushuka kidogo kwa 25% katika mahudhurio ya mechi za YANGA zinafikia mara mbili ya mapendekezo ya mapato takribani Sh milioni 8.3 kwa mwezi kupokelewa na YANGA kutoka mradi wa kibiashara kati ya TPL na Azam Television. Kwa kuzingatia haya, kwamba hata siku za nyuma kama kulikutokea fursa ya kurusha mchuano wa mpira unapochezwa, wadau wote (Timu za mpira wa miguu, TFF na Mtangazaji) walikuwa wanaafikiana kwanza kwa pamoja kuhusu mapato na mgawanyo wake.
Kamati ya Utendaji ya YANGA ina maoni kwamba makubaliano yoyote ya kibiashara yanayoihusu ni lazima iyalinde maslahi kifendha ya Klabu yake ambapo makubaliano ya TPL / Azam Television hayaangalii na kwa hiyo, Kamati ya Utendaji ya YANGA haitaki mchezo wake urushwe hewani na Azam Television.
Msisitizo wa TPL kuwa lazima Azam Television irushe hewani michezo ya YANGA linasikitisha. Kamati ya Utendaji ya YANGA haina tatizo na Vilabu vingine vya mpira wa miguu zikiruhusu michezo yao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha YANGA kuonyesha mchezo wake wa Vodacom Premier League katika Azam Television.
......................
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI
YOUNG AFRICANS SPORTS CLUB
29 JULAI, 2013
Duh...kama mkataba wenyewe umefanywa bila kuwashirikisha washiriki wanaotoa jasho uwanjani basi si sahihi. Haya ndio madudu ambayo bado Watanzania tunayaruhusu kuendelea kufanyika. Huwezi kulazimisha kurusha matangazo bila maelewano na mdau ambaye ndiye anayetoka jasho uwanjani. Ni wazi kuwa iwapo matangazo yatarushwa live, Yanga wataathirika kwenye mapato ya mlangoni hivyo basi ni lazima kukubaliana kiwango cha malipo. Pia ni ajabu kwa Bodi ya Ligi kuingia mkataba na Azam ambayo hata hiyo TV hatujawahi kuiona. Hii ndio miujiza inayotoke Tanzania na ukweli huu ni ufisadi unaoendela TFF kama ule wa kukata makato ya ajabu ajabu kwenye mechi. Klabu za Tanzania kama hazitapata viongozi wenye maono ya mbali, mpira wetu utaendelea kuwa wa kibabaishaji mpaka mwisho wa dunia. Mpira ni biashara na hamna biashara inaweza kufanyika bila maelewano. Yanga wapewe haki yao ya kushirikishwa na kujua huo mkataba unawanufaisha vipi. Ni hayo tu.
ReplyDeleteShaffih
ReplyDeleteIt's well written, Yanga ina kiongozi mwerevu, hajamung'unya hata neno moja.
Bravo Yanga
Hawa viongozi wa Yanga sasa hivi ni wafanyaiasara kweli kweli, naomba tuwaunge mkono kuna mahali watatupeleka hawa. Chelsea Tv inaingia ubia wa kudhamini ligi kuu, wao huwa wanaonysha mazuri tu Chelsea na mabaya ya timu zinginr, wapo sahihi tuwasurport, duu kumbe makamu mwenyekit wa TFL ni mkurugenzi wa Azam halafu tenda hazitangazwi. angalia anlisis za uongozi
ReplyDeleteNakubaliana na viongozi wa YANGA siku zote mkubwa ni mkubwa tu hata kama hautaki lakini ukweli ndio huo.Kiongozi unatakiwa uwe na uwezo wa kufikiri na kupambanua mambo hebu tujiulize lengo la AZAM ni nini? Utagundua kuwa lengo lao ni kutangaza biashara lakini matangazo hayo ya biashara yatatangazwa zaidi katika mechi za simba na yanga hivyo ni lazima ukubaliane kwanza na timu hizo na si kutumia nafasi yako ya uongozi kulazimisha mambo mwisho wa siku lazima utaumbuka tu. Si viongozi wote ambao wanatamaa ya fedha wengine wanaangalia kwanza maslahi ya timu ambazo wanaziongoza ndicho kitu ambacho wamekifanya Yanga nawapa hongera sana kwa hilo.Lazima tufahamu kuwa lengo la Yanga si kuzilalia timu ndogo ila ni kuhakikisha maslahi ya kila timu yanazingatiwa.
ReplyDeleteMpira ni biashara utake usitake. Bila pesa hakuna mpira tumeona timu nyingi zikishuka kwa kukosa pesa. safi sana viongozi wa YANGA kwa hilo. TFF waache ubabaishaji wa ezi za kale sasa hivi kila kitu kiko wazi watu wameelimika waache ubabaishaji.
ReplyDeleteKwa kweli kinachoendelea sio kizuri,nijambo zuri nala kimaendeleo km azam wangekubaliana na wahusika! Kwan wengi wangeona mechi nyingi popote walipo kupitia TV lakin imekosea ktk mchakato. Toka lini mchakato km huo usifanyike kwa kutangaza zabuni ili vyombo vingine vya habari vishiriki? Kuna Tbc,Itv, channel ten n.k vilipaswa vipewe navyo chance yakushiriki kwn co vbaya hata TV mbili zote kurusha matangazo hayo kwn hapo hata ushindan na ubora wa kitu ungeonekana..sasa km wao ndio wanataka waoneshe peke yao tena kwa bila kuridhia kwa vilabu vingine,hapo wamechemka na watapoteza hadhi yao sasa! Yanga wanapaswa kuungwa mkono na timu zingine,km kweli wana nia yakurusha basi tendering process ifanyike ili kutoa ushindan kwa vyombo vingne vya habari.. Safi yanga Value for money should be achieved nasio kukubali alafu wanufaike wengine! Mi nafikiri TFF waache kukurupuka na kua wasanii ktk masuala ya msingi..achen siasa hapo ndio maana mpira wetu haubadiliki mnawaza pesa nakusahau mipango na kuwekeza ktk vijana!! Yan mnafanya vitu utadhan hkn wasomi hapo,kaeni na wahusika mkubaliane yan umlipe mtu mil 8 wakati mechi moja tu mil50 nani mjinga anaweza kukubali nyie!!!
ReplyDeleteulichosema ni sahihi
ReplyDeletetupa kule itikadi za club, viongozi wa yanga wanajua wanachokifanya, hivi watu hawastuki kamati ya ligi ni ya mpito alafu wanasaini mkataba wa miaka 3? manake ni "nachukua changu nasepa", alafu kina rage wanafurahia au nao wans 10%! tunahitaji viongozi weredi wa kaliba ya manji wasiokua ns tamaa ya pesa za kiberiti! bravo dar young africans.
ReplyDeleteNajivunia kuwa shabiki wa Yanga, najivunia kuongozwa na Manji, najivunia kuongozwa na Sanga na cna uttata na utendaji wa Mwalusako! Bravo Yanga,atleast mnaonesha tutakwenda tunapopahitaji.
ReplyDeleteVIONGOZI WA YANGA HASA MHINDI SIJUI MWARABU WAACHE UBINAFSI NA KUUDANGANYA UMMA. HOJA YAO YA 2.1 SI KWELI KWA SABABU LIGI KUU AFRIKA YA KUSINI MATANGAZO YAKKE YANARUSHWA NA SUPERSPORT AMBAO NI WA MILIKI WA KLABU YA SUPERSPORT, PIA JUU YA MGAO MBONA MAPATO YA MILANGONI WANAGAWANA SAWA NA HIVYO VILABU WANAVYODAI WAO HAVINA MASHABIKI WENGI KAMA WAO? VILEVILE KUHUSU KUWA NA MJUMBE WAKATI WA MJADALA WA UDHAMINI WA HAKI YA MATANGAZO MBONA VIKAO VYOTE MWALUSAKO KAMA KATIBU WA YANGA NA CLEMENT SANGA WAMEHUDHURIA VIKAO VYOTE NA WALIONESHA KURIDHIA KWA HAWAKUPINGA HADI MAKUBALIANO YA AWAOUT YA MKATABA (MEMORANDUM OF UNDERSTANDING)KUFIKIWA? NAFIKIRI NI WIVU TU WA MANJI NA WANAOGOPA TABIA YAO YA KUNUNUA MECHI ITAKUFA KWA VILABU VITAJIENDESHA SI KWA KUPOKEA VISENTI VYAO KWA UKATA, PIA VIONGOZI WA YANGA NI WAOGA WA KUONGEZEKA USHINDANI. TFF WACHINJIENI HAO WAZANDIKI BAHARINI KWA FAIDA YA VILABU VIDOGO VIJITEGEMEE NA KUPOKEA RUSHWA TOKA VILABU VIKUBWA VYA YANGA NA SIMBA. BY MKINGA C.J wa Kimara DSM
ReplyDeleteWe Mzee wa Kimara...amka kumekucha!!!
DeleteAcha kuwa na mawazo yale yale ya enzi zileeeeeee!! Hata katika daladala abiria mnapanda kupita uwezo wa daladala na wakati mwingine abiria mwenzako akakukanyaga usisite kumwambia "tafadhali pamoja tumebanana ktk hii daladala lkn umenikanyaga mguu!!!"
Usipomwambia hivyo ataendelea kukukanyaga mpk mwisho wa safari...wanachofanya Young Africans ni kuwaambia TFF kupitia kamati ya usimamizi wa ligi hawapo tayari kukanyagwa ukizingatia ndo kwanza daladala ndo inakaribia kuanza safari.
So please wake up Mzee wa Kimara let's support the Young Africans on this...otherwise "big up MANJI na viongozi wote hapo mtaa wa Jangwani"
Usipo
WA KIMARA NASHUKURU KWA MAONI YAKO,ILA MFUMO ULIOUZUNGUMZIA WA SUPERSPORT NDIO TUNAOULILIA SISI,VILABU LAZIMA VIFAIDIKE KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE ILA KWA KUWA AZAM TAYARI IMESHAONYESHA DHAHIRI KUSHINDANA NA KLABU YA YANGA KIMAJUNGU NDIO SHAKA INAPOANZIA HAPO,SIPINGI KUONYESHWA LIVE KWA MICHEZO HIYO ILA TWAHITAJI USAWA NA USHIRIKWISHWAJI WA KLABU PIA.
DeleteMR.KIM
Mtoa maoni hapo juu ndo walewale wa enzi zileeeeee!!!!
ReplyDeleteSina hakika uwezo wake wa kupambanua mambo upo kwa kiasi gani (in percentage) because you can see it's non sence at all kwa alichokiongea...sema ni vile katiba ya nchi yetu inatoa uhuru kila raia kutoa maoni yake bila kuvunja sheria!!! Otherwise big up viongozi wa Dar Young Africans - YANGA!!!
Viongozi wa YAnga waache ubabaishaji wamekaa madarakani mwaka mzima hakuna mbele hakuna nyuma wanaenda enda tu nothing new out there...Wao wamekalia kupinga pinga tu bila point za msingi kwanza walipinga kuvaaa nembo nyekundu which is totally non sense in era sasa hivi wanapinga udhamini huu wenye manufaa kwa mpira wa Tanzania kwa sababu eti ya conflict of interest they have to remember that kule south Africa kuna supersport wanadhamini league by showing it na wana own a club na mambo yanaenda vizuri tu... its about time Yanga na simba waache fitna zao za kizamani waache watu wenye passion ya kweli na football walete maendeleo kwenye mpira wetu....
ReplyDeleteNo wonder national team yetu inafungwa kwa sababu ya msingi mbovu wa viongozi wa clubs kama hawa
ReplyDeleteNaomba kwanza uundwe umoja wa vilabu kisha vijadili matatizo yao na kubuni mbinu kwa makubalino yao kwa pamoja ilikutatua matatizo yao,kutambua fursa zao kwa maslahi yao na soka letu By datinatus wa mwanza
ReplyDeletewe manji tulia kama vipi fight upate uongozi tff na ww tukuone so kujifanya unajali sana maslahi wakati we mwenyewe ni mfanyabiasha kama hao azamfc.
ReplyDeletethis is politics hakuna cha kusifia hapa manji ana lolote anamuogopa bakhressa chunguzen vizuri, kwa hiyo yanga wakicheza na simba na simba akiwa mwenyeji ambapo anakuwa mmiliki wa mechi, mechi si itarushwanga sasa yanga si watakuwa wanajipunja, mechi zenyewe ambazo zitakuwa live hazizidi hata kumi na tano nyingine ni replay ambazo kimsingi hazina effect.
ReplyDeleteHoja no 5.2 ya vyanzo vya mapato haina mashiko, eti mechi ikiwa live mapato yanashuka, nakataa coz mechi nyingi zilizovunja record ni hizo hizo zilizorushwa live.
hoja nyingine ni ya kijinga eti yanga na azam wana uadui kwa hiyo haya matangazo yataiathiri yanga, cjaelewa hapa coz mechi ni live labda zingekuwa zinaeditiwa kama taarifa ya habari, lakini chuji akipiga pasi uwanja wa taifa basi na ss tunaocheki kwenye tv tutaona kapiga pasi no editting athari ipo wapi hapa.
Tatizo kubwa ni pale kitu cha mpito ambacho kinangatuka miezi miwili ijayo kinapofanya maamuzi makubwa kama haya.. WHY WHY WHY WHY? KWANINI? TFF nao hi hivyo hivyo, mnaondoka kesho mnampangia anayekuja vitu vya miaka mitatu ijayo. WHY WHY WHY, KWANINI? Au issue ni kuvuta tu chenu mapema.
ReplyDeleteAcha haya yote yajadiliwe na kufanyika kwa uwazi na kwa muda wa kutosha.
Inaonekana hawa Yanga wanapata ushindi kwa kutimia udhaifu wa kiuchumi wa timu pinzani, timu zikiwa na uwezo hii hegemony ya Yanga na Simba itaisha. Tunahitaji ligi yenye ushindani sio inatokea timu inaingia uwanjani hali ya kuwa hawajapata hata lunch!!
ReplyDeleteuongozi thabiti na maamuzi magumu yanahitajika inapobidi.
ReplyDelete