Search This Blog

Tuesday, June 26, 2012

TOP 10 YA MADEMU WA WACHEZAJI KWENYE EURO 2012 AMBAO WAMEKUWA VIVUTIO

Netherlands - Yolanthe Sneijder (Wesley Sneijder)

Don't feel too sorry for Wes after a hard day at the office, at least he's got something to look forward to!


Spain - Sara Carbonero (Iker Casillas)

No footballer likes a microphone shoved in their face at full time, but when it's Sara's, it's fair game

Ireland - Claudine Keane (Robbie Keane)

A woman with a rhyming name and blonde locks? Claudine is made for the LA lifestyle

Czech Republic - Radka Kocurova (Tomas Rosicky)

No, this isn't Tomas without the goatee - it's his delightful wife Radka

Germany - Aida Yespica (Mesut Ozil)

Ozil will look to follow in Aida's footsteps on Sunday and hold a cup of his own!

Spain - Lara Alvarez (Sergio Ramos)

Ramos will hope to avoid another Copa del Rey moment by keeping a tight grip on the lovely Lara

Germany - Sarah Brandner (Bastian Schweinsteiger)

Sarah Brandner completes the world's longest Mexican wave, spanning from Gdansk to the Costa del Sol

Italy - Alena Seredova (Gianluigi Buffon)

Nobody was more frustrated than Gigi when Italy-England went to penalties, delaying his bed time even further

Portugal - Irina Shayk (Cristiano Ronaldo)
Because sometimes two big guys up top does work...

Spain - Shakira (Gerard Pique)

Sorry, Sepp, but those hips probably are lying to you

OFFICIAL: ARSENAL YAMNASA MSHAMBULIAJI WA UFARANSA OLIVIER GIROUD

Hatimaye klabu ya Arsenal imefanikiwa kumnasa mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka kwa Montpellier ya Ligue 1.


Giroud ambaye alikuwa kwenye kikosi cha Ufaransa kilichokuwa kikishiriki kwenye michuano ya Euro 2012, amesaini mkataba wa miaka minne kuwepo Emirates na Gunners wamelipa kiasi cha paundi millioni 12 kupata huduma zake.

HUYU KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA - JAKOB MICHELSEN



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtambulisha rasmi leo mbele ya waandishi wa habari kocha mpya wa timu za Taifa za vijana, Jakob Michelsen kutoka Denmark ambaye amechukua nafasi ya Kim Poulsen ambaye hivi sasa anainoa Taifa Stars.
 
Michelsen ambaye amepewa mkataba wa mwaka mmoja alitambulishwa na Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah na kusema falsafa yake ni kama ile ya Poulsen ya kumiliki mpira na kushambulia muda wote wa mchezo.
 
Kabla ya kuja Tanzania, Michelsen alikuwa kocha wa timu ya daraja la kwanza ya Hobro IK ya Denmark. Ana leseni A ya ukocha kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA), leseni ya ukocha wa vijana kutoka Chama cha Mpira wa Miguu cha Denmark (DBU).
 
Moja ya mafanikio yake ni kuipa ubingwa wa Denmark, timu ya Skovbakken kwenye ligi ya timu zenye umri chini ya miaka 18. Ubingwa huo aliupata msimu wa 2005/2006.


TFF KUZAWADIA WAPIGA PICHA COPA COCA-COLA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) litawazawadia wapiga picha za magazetini watakaoripoti mashindano ya Copa Coca-Cola 2012 ngazi ya Taifa yanayoendelea kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.
 
Mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Coca-Cola na kushirikisha mikoa 28 yanafanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kumbukumbu ya Karume mkoani Dar es Salaam, na viwanja vya Tamco na Nyumbu mkoani.
 
Zawadi ya sh. 250,000 itatolewa kwa picha bora katika maeneo matatu; action picture, fair play picture na mpiga picha ambaye ameripoti matukio mengi ya mashindano hayo yanayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 17.
 
Washiriki wanatakiwa kuwasilisha picha zao zilizotumika (cuttings) ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 
NGORONGORO HEROES KUJIPIMA KWA MISRI, RWANDA
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) itacheza mechi nne za kirafiki na timu za Misri na Rwanda kabla ya kuivaa Nigeria kwenye mashindano ya Afrika.
 
Ngorongoro Heroes ambayo kwa mara ya kwanza itakuwa chini ya kocha mpya Jakob Michelsen itaanza kwa kucheza mechi mbili za Misri zitakazofanyika Julai 3 na 5 mwaka huu, na baadaye Julai 14 na 16 mwaka huu dhidi ya Rwanda.
 
Mechi zote zitachezwa nchini, na kama ilivyo Ngorongoro Heroes, Misri na Rwanda nazo ziko kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi za kucheza Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.
 
Katika raundi ya kwanza, Ngorongoro Heroes iliitoa Sudan ambapo katika raundi ya pili imepangiwa Nigeria, na mechi ya kwanza itafanyika jijini Dar es Salaam, Julai 29 mwaka huu. Timu hizo zitarudiana wiki mbili baadaye nchini Nigeria.
 
Iwapo Ngorongoro Heroes itafanikiwa kuitoa Nigeria, katika raundi ya mwisho itacheza na mshindi kati ya Congo Brazzaville na Afrika Kusini.
 
MABINGWA COPA WALALA KWA RUVUMA
Ruvuma imeanza vizuri michuano ya Copa Coca-Cola baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Kigoma mabao 2-0 katika mchezo wa kundi A uliofanyika leo asubuhi (Juni 26 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
 
Kigoma ambayo iliifunga Lindi mabao 2-0 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa juzi, ilishindwa kufua dafu mbele ya Ruvuma na kuruhusu bao katika kila kipindi.
 
Mabao yote ya washindi yalifungwa na mshambuliaji Edward Songo. Mshambuliaji huyo alifunga bao la kwanza dakika ya 34 wakati la pili alilipachika dakika ya 84.
 
Katika mechi nyingine zilizochezwa leo asubuhi, Tanga na Morogoro zilitoka sare ya mabao 3-3 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Tanganyika Packers ulioko Kawe, Dar es Salaam.
 
Mkoani Pwani, Mara iliifunga Temeke bao 1-0 kwenye Uwanja wa Nyumbu wakati Kagera ililala bao 1-0 mbele ya Kilimanjaro katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Tamco.
 

PIUS KISAMBALE AONDOKA RASMI YANGA - ASAINI COASTAL UNION

Pius Kisambale akitia saini mkataba wa miaka miwili kuichezea Coastal Union
Klabu ya Coastal Union ya Tanga imeendelea kuitunisha misuli kwenye soko la usajili hapa Tanzania.


Leo hii klabu hiyo imemsajili rasmi kiungo Pius Kisambale kutoka Day Young African kwa mkataba wa miaka miwili.


Kisambale ambaye ni mdogo wa damu wa kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Idd Chuji, amejiunga na Coastal Union akitokea Yanga ambayo alikaa nayo kwa msimu mmoja.



Monday, June 25, 2012

WAPINZANI WA JADI: SHABIKI WA YANGA JUMA NATURE NA MCHEZAJI WA SIMBA UHURU SULEIMAN


HIVI NDIVYO WACHEZAJI WA REAL MADRID WANAVYOITAWALA EURO 2012

Inawezekana ikawa ndio timu ya gharama zaidi ukiwaweka wachezaji wake kwa pamoja, timu yenye kikosi chenye wachezaji bora kabisa kwenye soka la level ya juu ni Real Madrid. Timu ambayo imemaliza msimu wa la liga kama mabingwa huku wakivunja rekodi ya kuwa pointi nyingi na kufunga magoli mengi zaidi.

Sasa msimu ukiwa umeisha wachezaji wengi wa Real Madrid wapo kwenye michuano ya Euro 2012, na kama ilivyo kwenye ngazi ya vilabu, huku napo wamekuwa wakitawala michuano hii kwenye nchi zao.
146644051_crop_650x440
CRISTIANO RONALDO
Kufuatia msimu ambao Real Madrid wakiwapora ubingwa Barcelona, Cristiano Ronaldo yupo katika mission ya kumpiku Lionel Messi kama mchezaji bora wa dunia.

Baada ya kuanza vibaya kwenye michezo miwili ya kwanza ambayo alikosa nafasi nyingi kufunga, Ronaldo alirudi kwenye fomu yake kwenye mechi muhimu dhidi ya Netherlands. Alifunga mabao mawili na kuiwezesha Ureno kuingia robo fainali.

Ronaldo alirudi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Czech na kucheza kwa kiwango cha juu kuliko mchezaji yoyote kwenye hatua hiyo ya Euro, Ronaldo alionekana anaweza akafunga muda wowote aliogusa mpira, aidha kwenye adhabu ndogo, tik tak hata kwa kichwa. Hatimaye alifunga goli la ushindi kwa kichwa safi.

Huku Ureno wakiwavaa Spain kwenye nusu fainali Ronaldo atakwenda kupambana na wachezaji wenzie wa Real Madrid, Sergio Ramos, Arbeloa, Alonso, na Iker Casillas.

Amefunga bao matatu 3



SERGIO RAMOS
Anatajwa kama mchezaji pekee wa Spain aliyeonyesha kwamba anaweza kuzuia kwa kiwango cha juu, Sergio Ramos ameonyesha kiwango kizuri kwenye michuao hii.

Huku Gerard Pique akionekana ku-struggle kuwa kwenye kiwango chake cha kawaida, Ramos amekuwa ndio mhimili wa ukuta wa Spain kumlinda Iker Casillas asiguswe, huku akifunika makosa ya mchezaji mwenzie aliye chini ya kiwango Alvaro Arbeloa, wakati Jordi Alba akionekana kusahau kwamba anapaswa kuzuia.

Tangu arudishwe kucheza kwenye nafasi ya beki wa kati kutoka kwenye shavu la kulia, Ramos amekuwa akicheza vizuri na kuzuia mashambulizi ya washambuliaji kwa nguvu alizonazo na speed.



MESUT OZIL
Huyu ndio master aliye nyuma ya mafanikio ya Ujerumani kwenye Euro 2012. Mesut Ozil , kiungo mchezeshaji wa kariba ya aina yake, amekuwa akiongeza kiwango chake, na ahatimaye alishinda tuzo ya man of the match kwenye mechi dhidi ya Ugiriki.

Master wa kupenyeza mipira kwenye lango la adui, Ozil anaifanyia Ujerumani mambo yale yale anayoifanyia Real Madrid ambayo imekuwa ikivunja rekodi za kufunga mabao ndani ya kipindi cha miaka miwili.

Njia sahihi ya kuizuia Ujerumani kwenye michuano hii, na kumzuia Ozil na kujaji kupitia kiwango chake, hilo litakuwa rahisi kusema kuliko kufanyika.

 

XABI ALONSO
Moja ya viungo wachache wanaoweza kucheza kwenye safu ya kushambulia na kukaba, uwezo wake wa kupiga pasi na kupiga mashuti ya mbali huku akicheza kwa kujituma kwa asilimia 100 kunamfanya kuwa mojaya viungo bora kabisa kwenye ramani ya dunia. Uwezo wake wa ku-control mchezo kutoka kwenye safu ya kiungo wakati akitoa usaidizi kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kimekuwa kitu muhimu sana kwa Spain kwenye michuano hii ya Euro.

Alonso ambaye juzi alisaidia kuiwezesha Spain kuvuka na kuingia nusu fainali baada ya magoli mawili kutoka kwa Xabi Alonso kuiondoa Ufaransa  kwenye mashindano.
Amefunga mabao 2

IKER CASILLAS
Mara nyingi amekuwa akitajwa kama golikipa bora kabisa kwenye soka duniani, nahodha wa Real Madrid na Spain amekuwa kwenye kiwango chake cha kawaida kwenye Euro 2012. Ukiondoa goli la Antonio Di Natale kwenye mechi ya kwanza Spain hawajaruhusu goli kutinga kwenye nyavu zao mpaka sasa.

Huku akiokoa michomo ya hatari dhidi ya Croatia, aliendeleza mchezo mzuri kwenye mechi dhidi ya France.

Akicheza kwa kutulia dimbani, Casillas anaweza akaonekana kuwa hana kazi kubwa ya kufanya, lakini amekuwa akifanya vizuri pale ukuta wake unaporuhusu wapinzani kumfikia.

Ikiwa atashinda kombe la Euro 2012, Casillas ataweka rekodi ya kuwa kipa na nahodha wa kwanza kushinda makombe matatu makubwa mfululizo, na hilo linaweza kumfanya kuwa golikipa bora wa muda wote kwenye soka.

 


PEPE NA FABIO COENTRAO
Hawa ndio nguzo ya ulinzi ya timu ya Ureno, Pepe amekuwa kwenye kiwango cha juu kwenye michuano hii akiepuka kujihusisha na matukio ya utovu wa nidhamu ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara. Pepe kwa kushirikiana na Perira, Coentrao na Bruno Alves wamekuwa wakiunda ngome ngumu ya Ureno ambayo imeiwezesha timu hiyo kuwemo kwenye hatua ya nusu fainali ambapo watacheza dhidi ya Spain.
PEPE amefunga goli 1.

Kwa upande wa Fabio Coentrao nae amekuwa kwenye kiwango cha hatari akikaba na kupandisha vizuri mashambulizi kumsaidia Cristiano Ronaldo kuwanyanyasa mabeki wa timu pinzani.


KHEDIRA
Performance ya Ujerumani kwenye michuano imekuwa nzuri sana, pamoja na mwanzoni kuonekana kama kwenye safu ya ulinzi kuna matatizo lakini chini ya ulinzi wa Sami Khedira safu ya mabeki wa Ujerumani wamekuwa wakicheza kwa kiwango kizuri.

Khedira amecheza vizuri kwenye mechi zote za Ujerumani na aliisadia timu yake kuvuka kwenye hatua ya robo faianali baada ya kufunga goli nzuri dhidi ya Ugiriki.
Amefunga goli 1

IPI PENALTY BORA KATI YA HIZI!

SHABIKI WA KICHINA AFARIKI KWA KUTOLALA SIKU 11 AKIANGALIA EURO 2012

Hii ndio ilikuwa mechi ya mwisho kuiona Italy vs Ireland
Kuangalia kila dakika ya michuano mikubwa ya soka ni tamanio la kila shabiki wa dhati wa soka, lakini kuendekeza sana kiasi cha kusahau japo kulala kunaweza kukaleta matokeo mabaya.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka kijiji cha Hunan China, shabiki aitwaye Jiang Xiaoshan amekutwa amekufa baada ya kukaa macho usiku kucha kwa siku 11 huku akiangalia Euro 2012 marathon. Mechi za Euro zimekuwa zikianza 2.45 a.m kwa muda wa China, hivyo Mr.Jiang alikuwa akiangalia mechi mpaka asubuhi na baada ya hapo alikuwa akienda kazini kufanya kazi siku nzima. Kwa bahati, gazeti la Telegraph linaripoti kwamba staili ya mchina huyu imeishia kwenye balaa.

"Kijana huyo mwenye miaka 26, alikutwa amefariki na mama yake baada ya kushindwa kulala kwa siku 11 akiangalia soka, na hatimaye mambo yakawa magumu siku ambayo Italia walishinda 2-0 dhidi ya Ireland.

"Tulikuwa tunapumzika kidogo lakini siku zote tulikuwa tunaangalia soka bila kukosa mechi yoyote," rafiki mmoja alisema.

Shabiki huyo ambaye alikuwa na afya njema, lakini mfumo wa kinga yake ya mwili uliodhohofika kutokana kutopumzisha mwili kwa kulala na tabia ya kuvuta na kunywa sana pombe wakati akiangalia mechi.

Marehemu Mr.Jiang aliangalia zaidi ya dakika 1,890 za mechi na kuona magoli 51 yakifungwa. Pia inasemekana alikuwa akiisapoti England na Ufaransa kwenye michuano hiyo.

JOE HART ANGEANGALIA HII - PIRLO ASINGEMFUNGA PENATI JANA

REAL MADRID YAFUZU NUSU FAINALI EURO 2012!

Michuano ya Euro 2012 sasa imefika hatua ya nusu fainali, miongoni mwa wachezaji wa timu hizo nne zilizofika hatua ya nusu fainali kuna jumla ya wachezaji 11 wanaochezea klabu ya Real Madrid hivi sasa au waliwahi kuichezea klabu hiyo hapo awali.

na hiki ndicho kikosi cha Real Madrid kinachoundwa na wachezaji kutoka mataifa ya Hisapania,Ujerumani,Italia na Ureno

MFUMO:
4:2:1:2:1

Arbeloa,Coentrao,Ramos,Albiol

Pepe &Xabi Alonzo

-Both kuwa-cover the back four
Special Duty ya Alonzo ku-dictate team pia.

Khedira

-Supporting Pepe & Alonzo wakati wa kukaba pia kuwa kama daraja la mipira kwenda mbele wanaposhambulia.

Ozil & Ronaldo

Ozil akitokea pembeni kulia , Ronaldo- akitokea pembeni kushoto

Negdredo

as a lone Striker

                        GOLIKIPA: IKER CASILLAS- NAHODHA ( HISPANIA )
                 BEKI WA KULIA: ALVARO ARBELOA ( HISPANIA )
                    BEKI WA KUSHOTO: FABIO COENTRAO ( URENO )
     BEKI WA KATI : RAUL ALBIOL ( HISPANIA )                       
   KIUNGO MKABAJI : PEPE ( URENO )
    KIUNGO MSHAMBULIAJI : SAMMY KHEDIRA-KULIA ( UJERUMANI )
     KIUNGO MSHAMBULIAJI : MEZUT OZIL-KUSHOTO  ( UJERUMANI )
    KIUNGO MKABAJI : XABI ALONZO ( HISPANIA )
                  BEKI WA KATI : SERGIO RAMOS ( HISPANIA )  
    MSHAMBULIAJI: ALVARO NEGREDO ( HISPANIA )
MSHAMBULIA: CRISTIANO RONALDO ( URENO )
KOCHA: VICENTE DEL BOSQUE

CHEMSHA BONGO! HIKI NI KIKOSI CHA TIMU GANI ? TAJA WALAU MAJINA 3 YA WACHEZAJI KWENYE KIKOSI HIKI.

ANAYEJUA ANAJUA: DAVID TREZEGUET APIGA 2 NA KUIRUDISHA RIVER PLATE LIGI KUU YA AREGNTINA

Wakati Ufaransa ikitolewa na Spain hatua ya robo fainali ya michuano Ya EURO 2012, mshambuliaji wa zamani wa Ufaransa mwenye asili ya Argentina David Sergio Trezequet alikuwa ni mwenye furaha baada ya kufunga mabao mawili yaliyoisaidia timu yake ya nyumbani na mabingwa wa zamani wa Argentina River Plate kuweza kupanda daraja na kurudi tena kwenye Ligi Kuu ya Argentina Maarufu Kama Primera A Nacional.

Rive Plate itacheza Primera A Nacional msimu ujao, baada ya kuifunga timu ya Almirante Brown mabao 2-0 na Kufanikiwa kuongoza na kuchukua ubingwa wa Primera B Nacional (Ligi Daraja la pili ya Argentina)
River Plate kwa mshangao mkubwa wa wengi msimu uliopita waliporomoka na kushuka daraja hadi Primera B Nacional baada ya kuwa na msimu mbaya na kufungwa katika mechi ya mwisho ya kuwania kushuka daraja.
Sasa Wamepanda na kurudi tena kwenye ligi kuu ya Argentina Primera A Nacional baada ya msimu moja tu tangu washuke daraja.
River Plate wamepanda daraja pamoja na timu ya Quilmes.

EXCLUSIVE: HIVI NDIVYO MASHABIKI WA CHELSEA TANZANIA WALIVYOSHEREHEKEA UBINGWA WA ULAYA











WAANZILISHI WA YANGA KIDS WALIPOKUTANA LEO KWA PAMOJA

Leo hii Jumapili wachezaji wa zamani na waanzilishi wa Yanga Kids walikutana kwa pamoja kuungana mchezaji mwenzao Kassim Manara ambaye alikuwa kwa takribani miaka 20 iliyopita. Yanga kids ilianzishwa mwaka 1972. Mkutano wa wachezaji hao wa zamani ulianzia kwenye makao makuu ya klabu Pan African - Kariako na baadae wakaelekea Kigamboni kwenye picnic iliyofanyika ufukweni.
   Waliokaa ni Kassim Manara na Juma Pondamali. Waliosimama mstari wa katikati kutoka kushoto ni Herman, Dr Dau, Jafari AbdulRahman, Mustafa Mnyepe, Dotto Mokili and Mapunda. mstari wa nyuma kutoka kushoto Hassan Sharifu, Adolf, Beda, Jafari Kajembe, Mlokwa, Mkweche, Mfaume Juma, Mshike Juma and Gordian Mapango


Picha ya pamoja kati ya waanzilishi wa Yanga Kids na waliokua Senior players,
waliokaa chini (kutoka kushoto ) Kitwana Manara,Athuman Chilambo hao ndo waliokua wachezaji wakongwe.

Waliokaa kutoka kushoto ni Mohamed Yahaya Tostao, Mohamed Mkweche, Jafari AbadulRahman, Michael Mapunda and Gordian Mapango. Waliosimama kutoka kushoto Jafari Kajembe, Beda Simtaji, Hassan Sharifu! 

Adolf Rishard akipata msosi eneo la Kigamboni walipokutana wachezaji na waanzilishi wa Yanga Kids

Hapa wakikumbushana matukio waliyoyafanya kipindi hicho walipokuwa moto wa kuotea mbali dimbani

Muda wa maakuli


Sunday, June 24, 2012

MICHUANO YA SHULE ZA SEKONDARI (UMISSETA) YASHIKA KASI MJINI KIBAHA

 Washangiliaji wa timu ya Nyanda za Juu wakishangilia wakati timu yao ilipokuwa dimbani ikimenyana na Kanda ya Kati katika mchezo wa Soka katika michuano ya shule za Sekondari UMISSETA zinazoendelea Mkoani Kibaha leo. Timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1 (PICHA ZOTE NA CLECENCIA TRYPHONE).
 Gori kipa (GK) wa Kaskazini Mashariki akiokoa hatari langoni mwa timu yake dhidi ya Zanzibar kwenye mojawapo ya mechi za michuano ya shule za sekondari (Umisseta) inayoendelea Kibaha mkoani Pwani. Kaskazini Mashariki ilishinda 20-13. 
 Kanda ya Dar es Salaam ikichuana na Magharibi katika mchezo wa Wavu ambapo Dar ces Salaam imeshinda kwa seti 3-0.
 Wachezaji wa ziwa Magharibi (kijani) wakichuana na wachezaji wa Mashariki katika mpira wa Kikapu uliofanyika leo. Mashariki wameshinda kwa pointi 99-27