Sasa msimu ukiwa umeisha wachezaji wengi wa Real Madrid wapo kwenye michuano ya Euro 2012, na kama ilivyo kwenye ngazi ya vilabu, huku napo wamekuwa wakitawala michuano hii kwenye nchi zao.
CRISTIANO RONALDO
Kufuatia msimu ambao Real Madrid wakiwapora ubingwa Barcelona, Cristiano Ronaldo yupo katika mission ya kumpiku Lionel Messi kama mchezaji bora wa dunia.
Baada ya kuanza vibaya kwenye michezo miwili ya kwanza ambayo alikosa nafasi nyingi kufunga, Ronaldo alirudi kwenye fomu yake kwenye mechi muhimu dhidi ya Netherlands. Alifunga mabao mawili na kuiwezesha Ureno kuingia robo fainali.
Ronaldo alirudi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Czech na kucheza kwa kiwango cha juu kuliko mchezaji yoyote kwenye hatua hiyo ya Euro, Ronaldo alionekana anaweza akafunga muda wowote aliogusa mpira, aidha kwenye adhabu ndogo, tik tak hata kwa kichwa. Hatimaye alifunga goli la ushindi kwa kichwa safi.
Huku Ureno wakiwavaa Spain kwenye nusu fainali Ronaldo atakwenda kupambana na wachezaji wenzie wa Real Madrid, Sergio Ramos, Arbeloa, Alonso, na Iker Casillas.
Amefunga bao matatu 3
SERGIO RAMOS
Anatajwa kama mchezaji pekee wa Spain aliyeonyesha kwamba anaweza kuzuia kwa kiwango cha juu, Sergio Ramos ameonyesha kiwango kizuri kwenye michuao hii.
Huku Gerard Pique akionekana ku-struggle kuwa kwenye kiwango chake cha kawaida, Ramos amekuwa ndio mhimili wa ukuta wa Spain kumlinda Iker Casillas asiguswe, huku akifunika makosa ya mchezaji mwenzie aliye chini ya kiwango Alvaro Arbeloa, wakati Jordi Alba akionekana kusahau kwamba anapaswa kuzuia.
Tangu arudishwe kucheza kwenye nafasi ya beki wa kati kutoka kwenye shavu la kulia, Ramos amekuwa akicheza vizuri na kuzuia mashambulizi ya washambuliaji kwa nguvu alizonazo na speed.
MESUT OZIL
Huyu ndio master aliye nyuma ya mafanikio ya Ujerumani kwenye Euro 2012. Mesut Ozil , kiungo mchezeshaji wa kariba ya aina yake, amekuwa akiongeza kiwango chake, na ahatimaye alishinda tuzo ya man of the match kwenye mechi dhidi ya Ugiriki.
Master wa kupenyeza mipira kwenye lango la adui, Ozil anaifanyia Ujerumani mambo yale yale anayoifanyia Real Madrid ambayo imekuwa ikivunja rekodi za kufunga mabao ndani ya kipindi cha miaka miwili.
Njia sahihi ya kuizuia Ujerumani kwenye michuano hii, na kumzuia Ozil na kujaji kupitia kiwango chake, hilo litakuwa rahisi kusema kuliko kufanyika.
XABI ALONSO
Moja ya viungo wachache wanaoweza kucheza kwenye safu ya kushambulia na kukaba, uwezo wake wa kupiga pasi na kupiga mashuti ya mbali huku akicheza kwa kujituma kwa asilimia 100 kunamfanya kuwa mojaya viungo bora kabisa kwenye ramani ya dunia. Uwezo wake wa ku-control mchezo kutoka kwenye safu ya kiungo wakati akitoa usaidizi kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi kimekuwa kitu muhimu sana kwa Spain kwenye michuano hii ya Euro.
Alonso ambaye juzi alisaidia kuiwezesha Spain kuvuka na kuingia nusu fainali baada ya magoli mawili kutoka kwa Xabi Alonso kuiondoa Ufaransa kwenye mashindano.
Amefunga mabao 2
IKER CASILLAS
Mara nyingi amekuwa akitajwa kama golikipa bora kabisa kwenye soka duniani, nahodha wa Real Madrid na Spain amekuwa kwenye kiwango chake cha kawaida kwenye Euro 2012. Ukiondoa goli la Antonio Di Natale kwenye mechi ya kwanza Spain hawajaruhusu goli kutinga kwenye nyavu zao mpaka sasa.
Huku akiokoa michomo ya hatari dhidi ya Croatia, aliendeleza mchezo mzuri kwenye mechi dhidi ya France.
Akicheza kwa kutulia dimbani, Casillas anaweza akaonekana kuwa hana kazi kubwa ya kufanya, lakini amekuwa akifanya vizuri pale ukuta wake unaporuhusu wapinzani kumfikia.
Ikiwa atashinda kombe la Euro 2012, Casillas ataweka rekodi ya kuwa kipa na nahodha wa kwanza kushinda makombe matatu makubwa mfululizo, na hilo linaweza kumfanya kuwa golikipa bora wa muda wote kwenye soka.
Hawa ndio nguzo ya ulinzi ya timu ya Ureno, Pepe amekuwa kwenye kiwango cha juu kwenye michuano hii akiepuka kujihusisha na matukio ya utovu wa nidhamu ambayo yamekuwa yakimuandama mara kwa mara. Pepe kwa kushirikiana na Perira, Coentrao na Bruno Alves wamekuwa wakiunda ngome ngumu ya Ureno ambayo imeiwezesha timu hiyo kuwemo kwenye hatua ya nusu fainali ambapo watacheza dhidi ya Spain.
PEPE amefunga goli 1.
Kwa upande wa Fabio Coentrao nae amekuwa kwenye kiwango cha hatari akikaba na kupandisha vizuri mashambulizi kumsaidia Cristiano Ronaldo kuwanyanyasa mabeki wa timu pinzani.
KHEDIRA
Performance ya Ujerumani kwenye michuano imekuwa nzuri sana, pamoja na mwanzoni kuonekana kama kwenye safu ya ulinzi kuna matatizo lakini chini ya ulinzi wa Sami Khedira safu ya mabeki wa Ujerumani wamekuwa wakicheza kwa kiwango kizuri.
Khedira amecheza vizuri kwenye mechi zote za Ujerumani na aliisadia timu yake kuvuka kwenye hatua ya robo faianali baada ya kufunga goli nzuri dhidi ya Ugiriki.
Amefunga goli 1
No comments:
Post a Comment