Search This Blog

Thursday, December 8, 2011

ROONEY APOOZWA MACHUNGU: APUNGUZIWA ADHABU YA KUFUNGIWA NA UEFA


Mshambuliaji wa England na Manchester United Wayne Rooney leo amepunguziwa na UEFA kifungo chake cha mechi 3 na sasa atatumukia kifungo cha mechi mbili tu kufuatia rufaa yake iliyosikilizwa hivi leo huko Nyon, Uswisi huku mwenyewe akihudhuria.
Rooney, Miaka 26, alifungiwa mechi 3 na UEFA baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumpiga teke Beki wa Montenegro Miodrag Dzudovic England ilipocheza na nchi hiyo mwezi Oktoba na kutoka sare 2-2 na kufuzu kuingia Fainali za EURO 2012 zitakazochezwa Juni Mwakani huko Nchini Poland na Ukraine.
Kupunguziwa kwa adhabu hiyo kutamfanya Rooney aweze kucheza mechi ya mwisho ya Kundi D dhidi ya wenyeji Ukraine hapo Juni 19 na kuzikosa mechi mbili za kwanza dhidi ya France na Sweden,
MECHI ZA ENGLAND Kundi D EURO 2012:
Continue reading the main story
11 Juni - France (Donetsk)
15 Juni - Sweden (Kiev)
19 Juni - Ukraine (Donetsk)
Msemaji wa UEFA amesema adhabu ya kufungiwa kwa mechi ya 3 imesimamishwa kwa Miaka minne kuangalia mwenendo wake na itarudi ikiwa tu atafanya kosa kama hilo tena kwenye michuano ya UEFA inayohusisha Timu ya Taifa tu.
Pamoja na kusimamishwa adhabu hiyo Rooney itabidi atumikie kazi ya kijamii kwa Siku nzima kwenye miradi ya UEFA.
Rufaa ya Rooney ilisikilizwa na Jopo la Watu watatu na ilichukua muda wa Saa moja na Nusu huku Rooney akiwa pamoja na Kocha wa England Fabio Capello na Mawakili wao.

ASANTE KOTOKO KUWASILI NCHINI KESHO

Mkurugenzi wa Future Century Albert Albano akizungumzia ujio wa Asante Kotoko.

MAGWIJI wa soka Ghana, Asante Kotoko sasa itacheza na timu ya Simba peke yake katika mechi maalum ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Awali Asante Kotoko ilipanga kucheza na timu ya kombaini ya Simba na Yanga, hata hivyo Yanga wakabadili maamuzi na kuamua kutotoa wachezaji katika mchi hiyo muhimu ya historia.Mkurugenzi wa kampuni ya Future Century, Alberto Albano alisema jana kuwa hakuna taarifa za kimaandishi ambazo timu hiyo ya Jangwani imetoa kwao zaidi ya kutumia vyombo vya habari pekee.“Ni taarifa ambazo hazikuwa rasmi, lakini kutokana na hali ilivyokuwa, tumeamua bora kuachana nao na siku hiyo kuwapa nafasi Simba kuonyesha uwezo wao ikiwa pamoja na kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara,” alisema Albano.Alisema kuwa maandalizi yamekamilika na Asante Kotoko inatarajia kuwasili nchini kesho kwa ajili ya mchezo huo ambao umedhaminiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa PPF. Wadhamini wengine ni….Abano pia alisema kuwa mchezo huo ni sehemu ya kumtambulisha kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Simba, Mserbia, Cirkovic Milovan ambaye amechukua mikopa ya kocha wa Uganda, Moses Basena.Viingilio vya mchezo huo ni sh. 30,000 for VIP A, shs. 15,000 (VIP B), Shs. 10,000 for VIP C and shs. 7,000 kwa viti vya orange. Viti vya kijana ni shs. 3.000.Tiketi kwa ajili ya mchezo huo zinapatikana Steers, Big Bon, Oilcom, Benjamini Mkapa secondary school, Zizou fashion na Uwanja wa Taifa.

MSIBA: MANCHESTER UNITED YATOLEWA CHAMPIONS LEAGUE SASA KUCHEZA MECHI ZA ALHAMISI

Wednesday, December 7, 2011

SIKU KAMA YA LEO: MAN UNITED YAIFUNGA 4-0 GALATASARY LAKINI YASHINDWA KUFUZU 16 BORA-BECKHAM'S UCL DEBUT

NINI HATMA YA JIJI LA MANCHESTER LEO KATIKA CHAMPIONS LEAGUE

Hatma ya klabu mbili kubwa za jiji la Manchester kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya itajulikana leo wakati vikosi vya Roberto Mancini na Sir Alex Ferguson vitakuwa vikicheza mechi zao za mwisho za makundi huku vikihitaji kupata matokeo chanya ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kuweza kupata nafasi ya kuingia katika 16 bora ya ligi ya mabingwa wa ulaya.

Kwa upande wa Man City wenyewe wapo katika hali mbaya zaidi ya kuweza kuingia 16 bora, kwani wanahitajika kuifunga Bayern Munich iliyo katika form nzuri huku wakiomba Villareal amfunge Napoli ili waweze kushika nafasi ya pili katika kundi lao.

Vijana wa Sir Alex Ferguson wenyewe wanahitaji japo pointi moja ili kuweza kupita, lakini watakabiliwa na ugumu wa hali ya juu kutokana na upinzani watakaoupata kutoka kwa FC Basel ambao nao wanahitaji kuifunga United kwa ushindi wowote ili kuweza kuungana na Benfica ku-qualify in the last 16 stage. Timu hizi mbili zilitoka sare ya 3-3 katika uwanja wa Old Trafford katika mechi yao kwanza.

Ikiwa United watafungwa leo basi watakuwa wamefuata rekodi yao waliyoiweka miaka 6 iliyopita baada ya kushindwa kufuzu kuingia hatua ya pili ya champions league walipofungwa na Benfica kushika mkia katika kundi lao.

JE UNITED WATADHARIRIKA KAMA ILIVYOKUWA MWAKA 2005

RATIBA YA MECHI NYINGINE ZA CHAMPIONS LEAGUE LEO

MAN CITY VS BAYERN MUNICH

BENFICA VS OTELUL GALATI

VILLAREAL VS NAPOLI

LILLE VS TRABZONSPOR

INTER MILAN VS CSKA MOSCOW

FC BASEL VS MAN. UNITED

DINAMO ZEGREB VS LYON

AJAX VS REAL MADRID

MATUMLA NA MTAMBO WA GONGO KUMALIZA UBISHI KRISIMASI


MLEZI wa mchezo wa ngumi 'Masimbwi 'Mawe' Tanzania kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pamabano kati ya Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi Dar es Salaam.

Pambano hilo lisilo la ubingwa linatarajia kuwa katika uzito wa middle
weihgt raundi 10.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno Osward alisema atahakikisha
anamtwanga mpunzani wake ili kufuta machungu ya kumzidi kwa pointi
katika pambano lao walilocheza hivi karibuni.

"Matumla alinizidi kwa pointi sasa nataka kumonyesha kama ninauwezo wa
kumuangusha katika hatua za awali za pambano letu kwani nimejiandaa na
bado naendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo," alisema Maneno.

Naye kwa upande wake Rashid alisema, anaendelea kujifua ili kuweza
kuwapa raha mashabiki wake ikiwa na kuwapa zawadi ya Christimas kwa
kumtwanga kwa mara nyingine Maneno.

"Ushindi wangu ndio utakuwa zawadi kwa mashabiki wangu kwani
sinachazaidi cha kuwapa," alisema Rashid.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya'
ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema kabla ya kufanyika kwa
pambano hilo mabondia hao watapima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi
na madawa ya kuongeza nguvu ili kuweza kuwatayari kwa ajili ya
mpambano.

Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya mabondia Venas Mponji
atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia Rashidi Ally
atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi
wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet
Kalulu na Saleh Mtalekwa

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.

NGORONGORO YATOLEWA COSAFA KUREJEA BONGO KESHO



TIMU ya soka ya vijana ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, inatarajia kurejea nyumbani kesho Ijumaa alfajiri ikitokea jijini hapa ambapo ilikuwa inashiriki kwenye mashindano ya vijana ya COSAFA ambayo leo yanaingia katika hatua ya nusu fainali.

Ngorongoro Heroes iliyokuwa kwenye kundi C ilimaliza hatua ya makundi ikiwa katika nafasi ya pili baada ya kutoka sare na Zambia na Afrika Kusini na ikishinda mchezo mmoja dhidi ya Mauritius uliofanyika juzi.

Zambia ambao ndio mabingwa watetezi wa mashindano haya ndio timu iliyofuzu kutoka kundi C huku yosso wa Afrika Kusini wakimaliza wakiwa kwenye nafasi ya tatu na Mauritius ikishika mkia.

Kocha Mkuu wa Ngorongoro Heroes, Kim Poulsen, alisema jana kuwa ameridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika mashindano haya na kusema kwamba wamejifunza mambo mengi ikiwemo uchezaji wa timu nyingine ambazo wanaweza kukutana nao kwenye mashindano mengine ya kimataifa.

Kim alisema kuwa mechi zote zilikuwa ngumu na wachezaji walijipanga kuhakikisha hawapotezi mchezo jambo ambalo limewasaidia kutofungwa.

Aliongeza kuwa kila mchezaji alionyesha uwezo wake na wale ambao ilikuwa ni mara ya kwanza kushiriki katika mashindano ya kimataifa wamepata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.

Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Issa Rashid, ambaye anachezea klabu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania Bara, alisikitika kuona wametolewa kwenye mashindano hayo na kushaanga kutokuwepo kwa hatua ya robo fainali wakati ni mashindano yanayoandaliwa na shirikisho lenye uwezo.

Wakati huo huo, mechi za hatua ya nusu fainali ya mashindano ya vijana ya umri chini ya miaka 20 yanayoandaliwa na COSAFA inaanza leo jijini hapa kwa wenyeji Botswana kuikaribisha Zambia mchezo utakaofanyika kuanzia saa tisa mchana kwenye uwanja wa Molepolole ulioko nje kidogo ya jiji.

Botswana ilifuzu kutinga hatua hiyo juzi baada ya kuifunga Swaziland magoli 3-0 wakati Zambia yenyewe iliingia hatua hiyo kwa kuipa kichapo cha magoli 5-1 timu ya Afrika Kusini ambayo ndio timu pekee iliyokuwa inajiamini kwamba italibeba kombe hilo.

Nusu fainali nyingine itakayochezwa leo itakuwa ni kati ya Malawi dhidi ya Angola ambayo itaanza kurindima kuanzia saa 11:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.

Mbali na Tanzania timu nyingine zilizotolewa ni pamoja na Swaziland, Afrika Kusini, Msumbiji, Namibia, Madagascar, Mauritius, Shelisheli, Lesotho na Zimbabwe.

Zambia ndio bingwa mtetezi wa mashindano hayo akiushikilia ubingwa huo kwa mara ya pili mfululizo.

VIINGILIO VYA NUSU FAINALI YA CHALLENGE CUP.

NUSU FAINALI CECAFA TUSKER CHALLENGE

Mechi mbili za nusu fainali kuwania ubingwa wa 35 wa michuano ya CECAFA Tusker Challenge Cup inayoandaliwa na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) zinachezwa kesho (Desemba 8 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nusu fainali ya kwanza itakayozikutanisha Rwanda na Sudan itachezwa kuanzia saa 8.00 mchana na kufuatiwa na ile ya pili kati ya mabingwa watetezi Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) na Uganda (The Cranes) itakayoanza saa 10.00 jioni.

Viingilio katika mechi hizo ni sh. 3,000 kwa viti vya rangi ya bluu na kijani, sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B, n ash. 20,000 kwa VIP A.

Mechi ya fainali na ya kutafuta mshindi wa tatu zitachezwa Desemba 10 mwaka huu. Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) atapata dola za Marekani 30,000, makamu bingwa dola 20,000 na mshindi wa tatu dola 10,000.

BARUA YA YANGA KUTHIBITISHA USHIRIKI WA YANGA KATIKA MECHI DHIDI YA ASANTE KOTOKO -KABLA YA KUBADILI MAWAZO.

ARSENAL YAFUNZWA SOKA NA OLYMPIAKOS - YAPIGWA 3-1

DORTMUND YATOLEWA MABINGWA WA ULAYA

BARCELONA YAKAMILISHA RATIBA UEFA NA USHINDI WA REKODI

CHELSEA YATINGA 16 BORA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Mc​hezaji wa zamani wa Prisiner MADESHO MOYE amefariki dunia katika hospitali ya KCMC

Na Dixon Busagaga,Moshi.

TASNIA ya mchezo wa soka nchini imepata pigo kufuatia kifo cha
mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Prisiner Madesho Moye
kilichotokea leo majira ya saa nne asubuhi katika hospitali ya rufaa
ya KCMC.

Madesho aliyekuwa Rais wa timu ya soka ya Moshi Veterani aliugua
ghafla juzi muda mchache baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki
kati ya timu yake ya Moshi veterani na timu ya Wazee kutoka mkoani
Arusha ambayo alicheza kwa muda wote wa mchezo.

Taarifa za awali zilisema kuwa mara baada ya mchezo kumalizika
kulifanyika sherehe ndogo ya kupongezana kwa timu hizo mbili ambapo
mara baada ya sherehe hiyo kwisha Madesho alipanda gari yake na
kuelekea nyumbani ndipo hali ilibadilika ghafla na kusadiwa na
wachezaji waliokuwepo uwanjani hapo.

Baadae Madesho alikimbizwa katika hospitali ya Kilimanjaro hali
ilivyozidi kuwa mbaya alihamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Kcmc
ambako alipokelewa na kulazwa katika chumba cha uangalizi kwa wagonjwa
mahututi(ICU) ndipo hado kufikia leo saa 4 asubuhi taarifa za kifo
chake ndipo zilipotangazwa.

Marehemu Madesho aliwahi kuzichezea timu za Prisner,Boma Fc,Kiboko
Msheli na timu nyingine nyingi kabla ya kuamua kustaafu na kuendelea
na kazi aliyokuwa akifanya mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)katika mkoa
wa Kilimanjaro.

MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI ,AMEEN.

Madesho Moye akiwa amebeba kombe baada ya kufanikiwa kushinda kikombe
hicho katika mashindano ya Pasaka ambayo huandaliwa kila mwaka na
mamlaka ya bandali ya nchini Kenya.

Madesho Moye wa pili kutoka kulia (waliopiga magoti)akiwa na kikosi
cha timu ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro kilipofanya
ziara nchini Kenya April Mwaka huu katika mashindano ya kombe la
Pasaka ambalo timu hiyo ilifanikiwa kunyakua.



Madesho Moye akiwa katika picha ya pamoja na mchezaji wa timu ya soka
ya Standard Chartered ya jijini Nairobi ambaye jina lake
halikufahamika mara moja mara baada ya mchezo wa fainali uliopigwa
katika uwanja wa KPA mwaka huu.



Madesho Moye akiwa amebeba kikombe mara baada ya kukabidhiwa baada ya
kuwa washindi katika mashindano ya Pasaka yaliyofanyika nchini Kenya.

Tuesday, December 6, 2011

KILIMANJARO STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CUP

Timu ya taifa ya Tanzania bara Kilimanjaro Stars imefanikiwa kuingia nusu fainali ya CECAFA Senior Challenge Cup 2011, baada ya kuifunga timu ya Malawi kwa goli moja kwa bila. Goli la Stars lilifungwa na kiungo Nurdin Bakary katika kipindi cha kwanza na kudumu mpaka mwisho wa mchezo.

Kwa matokeo hayo Kili stars sasa itacheza na Uganda katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali siku ya Alhamisi.


MECHI ZA UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO: NINI HATMA YA CHELSEA?


CHELSEA VS VALENCIA

PORTO VS ZENIT

GENK VS LEVERKUSEN

DORTMUND VS MARSEILLE

BARCELONA VS BATE

PLZEN VS AC MILAN

LUIS SUAREZ MATATANI TENA - ANGALIA ALICHOFANYA.


Akiwa bado na kesi ya kumtolea maneno ya kibaguzi Patrice Evra, mchezaji wa Liverpool Luis Suarez anaweza kujikuta yupo kwenye matatizo zaidi baada ya kuwaonyeshea ishara ya kidole cha kati mashabiki wa Fulham baada ya mchezo uliozikutanisha timu zao katika muendelezo wa ligi kuu ya England usiku wa jana.

Suarez jana alikuwa katika wakati mgumu baada ya mashabiki wa Fulham katika uwanja wa Craven Cottage walipokuwa wakimzomea kwa kumuita “mdanganyifu” kutokana na kitendo chake cha kujiangusha katika mechi hiyo.

Kutokana na kitendo alichofanya Suarez ambacho mara nyingi hutatafsiriwa kuwa ni tusi, then anaweza akajikuta katika balaa la kukumbana na adhabu kutoka FA, ikiwa kamati ya nidhamu itaona ana makosa pindi watakapokaa kumjadili leo Jumanne.

MSAADA TUTANI: HUYU NI NANI? ALISHAWAHI KUWA MCHEZAJI GHALI ZAIDI DUNIANI.

Go long: Christian Vieri prepares to launch an American football
On target? Vieri watches his pass

KIBOKO YA TOP 4 LIVERPOOL AKALISHWA NA FULHAM

NANI KUUNDA KIKOSI BORA CHA MWAKA CHA UEFA.


Shirikisho la soka barani ulaya limetangaza majina ya wachezaji 56 pamoja na makocha 5 watakaogombea nafasi ya kuunda timu ya mwaka ya shirikisho hilo katika mwaka huu wa 2011.

Jumla ya wachezaji watano wamechaguliwa katika kila nafasi, huku final line up ikitarajiwa kutangazwa mwezi January 2012, tarehe 18. Mashabiki wanatakiwa kuwapigia kura na kuwachagua wachezaji 11 watakaounda kikiosi cha wachezaji bora wa barani ulaya ndani ya mwaka 2011.


Goalkeepers:
Manuel Neuer (Bayern Munich)
Edwin van der Sar (Retired)
Iker Casillas (Real Madrid)
Victor Valdes (Barcelona)
Joe Hart (Manchester City)

Right-backs:
Dani Alves (Barcelona)
Philipp Lahm (Bayern Munich)
Christian Maggio (Napoli)
Darijo Srna (Shakhtar Donetsk)
Maxi Pereira (Benfica)

Centre-backs:
Gerard Pique (Barcelona)
Nemanja Vidic (Manchester United)
Thiago Silva (AC Milan)
Mats Hummels (Borussia Dortmund)
Sergei Ignashevich (CSKA Moscow)
Benedikt Howedes (Schalke)
Javier Mascherano (Barcelona)
Vincent Kompany (Manchester City)
Rolando (Porto)
Adil Rami (Valencia)

Left-backs:
Eric Abidal (Barcelona)
Fabio Coentrao (Real Madrid)
Marcelo (Real Madrid)
Alvaro Pereira (Porto)
Ashley Cole (Chelsea)

Right midfielders:
Xherdan Shaqiri (Basel)
Arjen Robben (Bayern Munich)
Mario Gotze (Borussia Dortmund)
Gervinho (Arsenal)
Nani (Manchester United)

Central midfielders:
Yaya Toure (Manchester City)
Xavi (Barcelona)
Jack Wilshere (Arsenal)
Joao Moutinho (Porto)
Luka Modric (Tottenham)

Attacking midfielders:
Andres Iniesta (Barcelona)
Mesut Ozil (Real Madrid)
David Silva (Manchester City)
Marek Hamsik (Napoli)
Wesley Sneijder (Inter)

Left wingers:

Gareth Bale (Tottenham)
Eden Hazard (Lille)
Angel Di Maria (Real Madrid)
Juan Mata (Chelsea)
Ashley Young (Aston Villa)

Forwards:
Lionel Messi (Barcelona)
Radamel Falcao (Atletico Madrid)
Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Hulk (Porto)
Javier Hernandez (Manchester United)
Robin van Persie (Arsenal)
Sergio Aguero (Manchester City)
Mario Gomez (Bayern Munich)
Edinson Cavani (Napoli)
Antonio Di Natale (Udinese)

Coaches:
Pep Guardiola (Barcelona)
Andre Villas-Boas (Chelsea)
Jurgen Klopp (Borussia Dortmund)
Alex Ferguson (Manchester United)
Rudi Garcia (Lille)

Monday, December 5, 2011

USHINDI 4-0 WA ARSENAL DHIDI YA WIGAN


5 – Namba ya wachezaji wa Arsenal walio na assists nne au zaidi katika premier league.

37 – Wachezaji wanne wa Arsenal walifunga magoli katika mechi moja kwa mara ya kwanza baada ya mechi 37 tangu walipoifunga Aston 4-2,November 27th 2010.

179 – Goli alilofunga Thomas Vermaelen dhidi ya Wolves ended a run of 179 corners without a goal katika Premier League. Mechi ya mwisho Arsenal kufunga goli la kichwa ilikuwa dhidi ya (Feb. 23 2011 – Arsenal 1-0 Stoke – Sebastien Squillaci)

721 – Namba ya pasi zilizopigwa na Arsenal dhidi ya Wigan.

633 – Namba ya pasi zilizokamilika zilizopigwa na Arsenal dhidi ya Wigan.

11 – Namba ya magoli aliyofunga Thomas Vermaelen akiwa na Arsenal.

6 – Namba ya assists alizotoa Gervinho tangu aanze kuichezea Arsenal in EPL.
4 - Number ya Assists alizopiga Gervinho kumuendea Robin Van Persie.

31 – Career assists za Theo Walcott tangu ajiunge na Arsenal.

13 – Number ya assists za Walcott kumuendea Robin van Persie.

11 – Walcott assists for Arsenal in calendar year 2011.

18 – Namba ya magoli yote aliyoyafunga Robin van Persie katika mashindano yote msimu huu.

4 – Namba ya magoli yote aliyoyafunga Theo Walcott katika mashindano yote katika mashindano yote msimu huu..

3 – Idadi ya magoli waliyofunga Gervinho, Arteta, and Vermaelen katika mashindano yote msimu huu.

14 – Premier League matches played by Arsenal
30 – Magoli waliyofunga Arsenal msimu huu.
23 – Magoli waliyofungwa Arsenal msimu huu in EPL.
8 – Idadi ya mechi walizoshinda Gunners in EPL.
2 –
Idadi ya mechi walizotoa sare Gunners in EPL.

4 – Idadi ya mechi walizofungwa Gunners in EPL.


MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2011: RONALDO, XAVI NA MESSI VITANI


WAGOMBEA TUZO ZA FIFA BALLON D’OR 2011 WATAJWA – MESSI, RONALDO WAENDELEZA VITA.

Nominees wa mwisho wa kugombea tuzo za FIFA Ballon d’or 2011 katika category za mchezaji bora wa kiume wa mwaka 2011 na wa kike wametangazwa leo hiikatika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya jarida ya mpira wa miguu la kifaransa mjini Paris, ambapo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke, France Football CEO Francois Moriniere, na wachezaji wa zamani Emmanuel Petit na Gaetane Thiney walishiriki katika kuwatangaza Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Xavi kama wachezaji waliofanikiwa kuingia katika top 3 ya mchezaji bora wa kiume, huku mbrazil Marta, Homare Sawa(Japan) na mmarekani Abby Wambach wakigombea tuzo mchezaji bora wa mwaka wa kike.

Katika hatua nyingine Sir Alex Ferguson, Josep Guardiola na Jose Mourinho wakigombea tuzo ya kocha bora wa mwaka.

Nominees hawa walipatikana baada ya kufanyika kwa zoezi la kupiga kura lilowahusisha manahodha na makocha wakuu wa timu za taifa za wanawake na wanaume za mataifa yenye uanachama wa FIFA.

Pia katika category nyingine ya goli zuri la mwaka maarufu kwa jina la Puskas Award itagombaniwa na Wayne Rooney, Lionel Messi na Neymar.

Tuzo hizi zitatolewa na kutangazwa mwezi January, 9, 2012.

MUNGU AILAZE ROHO YA SOCRATES MAHALA PEMA PEPONI AMEN.



MSAADA TUTANI,HAWA NI KINA NANI ?



UZINDUZI WA FILAMU YA MR PRESIDENT WAFANA.

KUTOKA KUSHOTO (RAY KIGOSI, STEVE NYERERE NA JB )

ZAIDI ya Milioni 18 zimekusanywa kwenye uzinduzi wa filamu ya Mr President uliofanyika kwenye ukumbi wa Serena hoteli zamani Moven Pick usiku wa kuamkia jana.
Fedha hizo ambazo asilimia 20 zitaelekezwa kwenye hospitali ya Mwananyamala kusaidia Wodi za Wanawake na Watoto
zimepatikana kwa njia ya mnada wa CD za filamu hiyo inayoonyesha maisha halisi ya Rais Jakaya Kikwete.



MGENI WA HESHIMA VICKY KAMATA


Katika mnada huo vibopa na wasanii mbali mbali nchini walijitosa kununua Cd hizo kwa njia ya mnada ambapo wasanii
kama JB, Ray walijitosa kunua CD hiyo kwa shilingi 200,000 wakati mratibu wa Miss Tanzania Hashimu Lundenga alijitosa kwa kununua CD hiyo kwa shilingi 300,000.
Funika bovu ilikuwa kwa wafanyabiashara maarufu hapa nchini ambao walinunua Cd hiyo kwa Shilingi Milioni 1,000,000
mpaka Shilingi milioni 5.5 wakiongozwa na kundi la Freinds of Simba na wale wa Yanga Family.
Awali akizindua filamu hiyo mbunge wa Viti Maalum CCM ambaye alikuwa mgeni rasmi Mwambata, Vicky Kimata alisema
ni muda muafaka kwa wasanii kuungana na kuwa na umoja ili waweze kushinda vita ya maharamia wa kazi zao.


FRIENDS OF SIMBA (KUTOKA KUSHOTO,KIMBAU,JERRY AMBI,SALIM,KIM TENGA )




"Kuna sheria mpya ya haki miliki itatungwa na Bunge ili kulinda kazi za wasanii kutokana na kuibiwa kazi zao muda mrefu,
hii itakuwa na nguvu kuliko ile ya mwaka 99 ambayo imepitwa na wakati,"alisema Kamata
Alisema sanaa ni kazi nzuri ambayo imekuwa ikiwasaidia wasanii wa nje kuishi maisha mazuri, lakini pia kufanya maendeleo
katika maisha yao,tofauti na hapa nchini wasanii wamekuwa ndio mafukara wa kutupwa huku watu wachache wakinufaika na
kazi zao .
Vicky Kamata amezindua filamu hiyo kwa niaba ya Waziri Mathias Chikawe ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo hakuudhuria huku awali kampuni ya Papa-Z ambao ndio waandaaji wa filamu hiyo walitangaza kuwa Rais wa awamu ya tatu Ali Hassan Mwinyi ndio atakuwa mgeni rasmi.

Sunday, December 4, 2011

MAN UNITED DHIDI YA MAN CITY KOMBE LA FA ROUND YA TATU


Manchester City wamepangwa na mahasimu wao wakubwa Manchester United katika round ya tatu ya kombe la FA.

Itakuwa mara ya kwanza kwa vijana wa Sir Alex Ferguson kukutana na mabingwa watetezi wa kombe hilo tangu walipoadhiriwa kwa mabao 6-1 @Old Trafford in October.

United watasafiri kuelekea Etihad Stadium kwa ajili ya mchezo huo katika weekend ya tarehe 7/8.

Ratiba nzima ya raundi ya tatu ya FA Cup ipo kama ifuatavyo....


FA CUP: 3 ROUND FIXTURE

Middlesbrough v Shrewsbury

Nottingham Forest v Leicester City

Man City v Man United

Dagenham/Walsall v Millwall

Crawley v Bristol City

Doncaster v Sutton/Notts County

Bristol Rovers v Aston Villa

Tottenham v Cheltenham Town

Sheffield Wednesday v West Ham

Milton Keynes Dons v QPR

Hull v Ipswich

Coventry v Southampton

Brighton v Wrexham

Fulham v Charlton

Birmingham v Wolves

Norwich v Burnley

Arsenal v Leeds

Derby v Crystal Palace

Fleetwood/Yeovil v Blackpool

Swindon v Wigan

Barnsley v Swansea

Chelmsford/Macclesfield v Bolton

Newcastle v Blackburn

Everton v Tamworth

Sheffield Utd v Salisbury/Grimsby

Liverpool v Southend/Oldham

Gillingham v Stoke

Chelsea v Portsmouth

Watford v Bradford

Peterborough v Sunderland

West Bromwich v Cardiff

Reading v Stevenage

BARCELONA YAMTANDIKA MBISHI LEVANTE 5-0

MOURINHO AENDELEZA VIPIGO LA LIGA

CHELSEA YAINYOOSHA NEWCASTLE

PHIL JONES AFUNGA BAO LA KWANZA KWENYE SOKA-AKIIPA UNITED USHINDI DHIDI YA VILLA

ARSENAL HAWAKAMATIKI-YAIBAMIZA 4-0 WIGAN

MAN CITY YAENDELEZA MAUAJI ENGLAND-YAMTANDIKA NORWICH 5-1

TANZANIA 1-2 ZIMBABWE

KENYA were eliminated from the 2011 Cecafa Tusker Challenge Cup, following a dismal performance and 1-0 defeat by Sudan at the National Stadium on Saturday.

Sudan, on the blink of being sent home before the match, played tactfully and the jaded Kenyans had no answer.

Tanzania Mainland were also outplayed by guest team Zimbabwe who won 2-1 in the second match of the afternoon, but the home team, defending champions at the 12-team tournament, managed to qualify for the quarter finals as the second of two best runners-up sides from the three pools.

Zanzibar, who awaited the results of the final day to know their fate, were in the quarters as the best runners-up team.

The quarter finals pairings are:

Monday: Burundi v Sudan; Rwanda v Zanzibar

Tuesday: Zimbabwe v Uganda; Malawi v Tanzania Mainland

Kenya 0 Sudan 1

Kenya put up a gloomily poor performance losing 0-1 in their last Group ‘C’ against Sudan on Saturday. Later in the afternoon, Harambee Stars hoped they squeak into the quarter-finals if Tanzania Mainland beat Zimbabwe 2-0 in the last Group ‘A’ match.

If that happened, with Kenya and Zimbabwe on three points each, Harambee Stars with a -1 goal difference would have edged Zimbabwe [-2] as the second of the qualified third placed teams.

However, Zimbabwe trashed this computation early in the match when Daniel Ngoma scored in the first minute to give Zimbabwe a 1-0 lead. Then Said Maulid scored in his own goal to give the Zimbabweans a 2-0.

At that point, Kenya still held on to hopes if Zimbabwe went on to thrash Tanzania by a 4-0 margin. But it was the hosts who fought to pull back a goal through Mwinyi Kazimoto who converted an 85th minute penalty, shutting out the Harambee Stars.

In the encounter with Kenya, Sudan’s Bashir Koko rose unmarked in the six-yard box to head in powerfully in the 26th minute from a right flank corner.

There was earlier talk of disciplinary problems in the Kenya camp that ended with Jamal Mohammed and Paul Were being left out of selection altogether.

Also, since coming to the tournament, the Kenyans seemed unmotivated, murmurs indicating that Football Kenya Federation [FKF] had not paid player wages since they assembled in Nairobi preparing for the Challenge Cup.

The FKF chief executive officer, Lordvick Aduda, was in Dar es Salaam during the early stages of the tournament before leaving for Nairobi, promising that he would return with money for the players.

The FKF official left behind with the team, vice-chairman Sammy Shollei, is known to have made several frantic calls to Nairobi, reminding the aficionado there the need to live up to their promise or else morale among coach Francis Kimanzi’s team would continue to plummet.

TEAMS:-

KENYA - 1. Duncan Ochieng’: 5. Pascal Ochieng’ (captain), Yusuf Juma, 8. James Mulinge, 8. Brian Mandela, 13. Collins Okoth (12. Stephen Ochola, 79’), 7. Titus Mulama, 16. Humphrey Ochieng’ Mieno (10. Kevin Kimani, 45’), 9. Bob Mugalia, 20. Victor Ochieng’, 17. Stephen Waruru (14. James Situma, 64’)

Reserves not used - 18. Jackton Odhiambo, Gk; 19. Jockins Atudo, 3. Dennis Odhiambo

Coach - Francis Kimanzi [Kenya]

SUDAN - 16. Ilmoiz Maghoub (captain): 17. Muawia Bashir Koko, 14. Mageldin Abdalla, 9. Saif Eldin Ali, 5. Gulam Ali Kugour (18. Abuelgasim Saeed, 47’), 15. Khalifa Ahmed Bakhit, 7. Ramadan Agab, 20. Abdelrahman Ishag (6. Musaab Omer Maaz, 65’), 19. Amir Kamal Suliman, 13. Nazar Hamid Nassir, 12. Mohamed Musa (10. Mohamed Tahir Osman, 75’)

Reserves not used - 1. Rahaeldin Mohamed, Gk; 3. Amir Rabei Abdelnabi, 8. Mohamed Shaik Eldin, 4. Mohamed Ahmed Bashir

Scorer - 17. Muawia Bashir Koko (25’)

Coach - Mubarak Suliman

[Sudan]

Referee - Wiish Yabarow [Somalia]

Assistant ref - Equeh Yacin Hassan [Djibouti]

Asst ref - Hamis Changwalu [Tanzania]

Reserve ref - Eric Gasinzigwa [Burundi]

Match commissioner - Soulayman Hassan Waberi [Djibouti]

b>Tanzania 1 Zimbabwe 2

TEAMS:-

TANZANIA - 1. Juma Kaseja Juma (captain); 17. Godfrey Taitta, 3. Juma Jabu, 4. Juma Nyoso, 20. Shomari Kapombe (12. Erasto Nyoni, 29), 13. Ibrahim Mwaipopo, 7. Maulid Said (5. Nurdin Bakari, 57’), 6. Mwinyi Kazimoto, 9. Thomas Ulimwengu (14. Hussein Javu, 55’), 8. Mrisho Ngassa, 16. Ramadhani Chombo

Reserves not used - 18. Shaban Kado, Gk; 19. Shaban Nditti, 11. Musa “Mgossi” Hassan, 2. Haruna Moshi,

Scorer – 6. Mwinyi Kazimoto (87’, penalty)

Coach - Charles Boniface Mkwassa [Tanzania]

ZIMBABWE - 16. George Chigona: 2. Daniel Veremu (captain), 3.Qadir Amini, 5. Rahman Kutsanzira, 6. Eric Mudzingwa, 8. Timire Mamvura, 10. Donald Ngoma, 11. Benjamin Marere, 17. Charles Sibanda, 18. Joel Ngodzo, 7. Tapiwa Kumbuyani

Reserves not used - Ariel Sibanda, Gk; 4. James Jam, 9. Leonard Fiyado, 12. Tinashe Masika, 13. Thokozo Tshuma, 14. Cliff Sekeye, 19. Honest Moyo

Scorers - 10. Donald Ngoma (1’), 13. Ibrahim Mwaipopo (11’, own goa)

Coach - Norman Mapeza [Zimbabwe]

Referee - Davies Omweno [Kenya]

Assistant ref - Mark Ssonko [Uganda]

Asst ref - David Sagero [Kenya]

Reserve ref - Ronnie Kalema [Uganda]

Match commissioner - Tesfaye Gebryesus [Eritrea]

2011 CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP

Dar es Salaam, November 25-December 10

Defending champions: Tanzania Mainland

GROUP ‘A’:

Tanzania Mainland

Rwanda

Zimbabwe

Djibouti

Results:

Tanzania Mainland 0-1 Rwanda

Zimbabwe 2-0 Djibouti

Rwanda 2-0 Zimbabwe

Djibouti 0-3 Tanzania

Rwanda 5-2 Djibouti

Tanzania 1-2 Zimbabwe

GROUP ’B’:

Uganda

Burundi

Zanzibar

Somalia

Burundi 4-1 Somalia

Uganda 2-1 Zanzibar

Zanzibar 0-0 Burundi

Somalia 0-4 Uganda

Somalia 0-3 Zanzibar

Burundi 1-0 Uganda

GROUP ‘C’

Sudan

Malawi

Kenya

Ethiopia

Results:

Sudan 1-1 Ethiopia

Kenya 0-2 Malawi

Ethiopia 0-2 Kenya

Malawi 0-0 Sudan

Ethiopia 1-1 Malawi

Kenya 0-1 Sudan

RESULTS & FIXTURES:

Friday, November 25:

1. 2.00pm: Burundi 4-1 Somalia, Gp ‘B’

2. 4.00pm: Uganda 2-1 Zanzibar, Gp ‘B’

Saturday, Nov 26:

3. 4.00pm: Tanzania 0-1 Rwanda, Gp ‘A’

Sunday, Nov 27:

4. 2.00pm: Zimbabwe 2-0 Djibouti, Gp ‘A’

5. 4.00pm: Zanzibar 0-0 Burundi, Gp ‘B’

Monday, Nov 28:

6. 2.00pm: Sudan 1-1 Ethiopia, Gp ‘C’

7. 4.00pm: Kenya 0-2 Malawi, Gp ‘C’

8. 4.00pm: Somalia 0-4 Uganda, Gp ‘B’ [Azam FC Stadium, Chamazi]

Tuesday, Nov 29:

9. 2.00pm: Rwanda 2-0 Zimbabwe, Gp ‘A’

10. 4.00pm: Djibouti 0-3 Tanzania, Gp ‘A’

Wednesday, No 30:

11. 2.00pm: Ethiopia 0-2 Kenya, Gp ‘C’

12. 4.00pm: Malawi 0-0 Sudan, Gp ‘C’

Thursday, December 1:

13. 2.00pm: Somalia 0-3 Zanzibar, Gp ‘B’

14. 4.00pm: Burundi 1-0 Uganda, Gp ‘B’

Fri, Dec 2:

15. 2.00pm: Rwanda 5-2 v Djibouti, Gp ‘A’

16. 4.00pm: Ethiopia 1-1 Malawi, Gp ‘C’

Sat, Dec 3:

17. 2.00pm: Kenya 0-1 Sudan, Gp ‘C’

18. 4.00pm: Tanzania 1-2 Zimbabwe, Gp ‘A’

Sun, Dec 4: R E S T D A Y

QUARTER FINALS

Mon Dec 5:

19. Burundi v Sudan

20. Rwanda v Zanzibar

Tue, Dec 6:

21. Zimbabwe v Uganda

22. Malawi v Tanzania Mainland

Wed, Dec 7: R E S T D A Y

SEMI FINALS

Thur, Dec 8:

23. Winner 19 v Winner 20

24. Winner 21 v Winner 22

Fri, Dec 9: R E S T D A Y

Sat, Dec 10:

BRONZE MEDAL:

Loser 23 v Loser 24

FINAL:

Winner 23 v Winner 24