Hatma ya klabu mbili kubwa za jiji la Manchester kwenye michuano ya klabu bingwa ya ulaya itajulikana leo wakati vikosi vya Roberto Mancini na Sir Alex Ferguson vitakuwa vikicheza mechi zao za mwisho za makundi huku vikihitaji kupata matokeo chanya ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kuweza kupata nafasi ya kuingia katika 16 bora ya ligi ya mabingwa wa ulaya.
Kwa upande wa Man City wenyewe wapo katika hali mbaya zaidi ya kuweza kuingia 16 bora, kwani wanahitajika kuifunga Bayern Munich iliyo katika form nzuri huku wakiomba Villareal amfunge Napoli ili waweze kushika nafasi ya pili katika kundi lao.
Vijana wa Sir Alex Ferguson wenyewe wanahitaji japo pointi moja ili kuweza kupita, lakini watakabiliwa na ugumu wa hali ya juu kutokana na upinzani watakaoupata kutoka kwa FC Basel ambao nao wanahitaji kuifunga United kwa ushindi wowote ili kuweza kuungana na Benfica ku-qualify in the last 16 stage. Timu hizi mbili zilitoka sare ya 3-3 katika uwanja wa Old Trafford katika mechi yao kwanza.
Ikiwa United watafungwa leo basi watakuwa wamefuata rekodi yao waliyoiweka miaka 6 iliyopita baada ya kushindwa kufuzu kuingia hatua ya pili ya champions league walipofungwa na Benfica kushika mkia katika kundi lao.
JE UNITED WATADHARIRIKA KAMA ILIVYOKUWA MWAKA 2005
RATIBA YA MECHI NYINGINE ZA CHAMPIONS LEAGUE LEO
MAN CITY VS BAYERN MUNICH
BENFICA VS OTELUL GALATI
VILLAREAL VS NAPOLI
LILLE VS TRABZONSPOR
INTER MILAN VS CSKA MOSCOW
FC BASEL VS MAN. UNITED
DINAMO ZEGREB VS LYON
AJAX VS REAL MADRID
No comments:
Post a Comment