MLEZI wa mchezo wa ngumi 'Masimbwi 'Mawe' Tanzania kamanda wa Polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova anatarajia kuwa mgeni rasmi katika pamabano kati ya Rashid Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Osward ‘Mtambo wa Gongo’ linalotarajia kufanyika Desemba 25 katika ukumbi wa Heinken, Mtoni Kijichi Dar es Salaam.
Pambano hilo lisilo la ubingwa linatarajia kuwa katika uzito wa middle
weihgt raundi 10.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Maneno Osward alisema atahakikisha
anamtwanga mpunzani wake ili kufuta machungu ya kumzidi kwa pointi
katika pambano lao walilocheza hivi karibuni.
"Matumla alinizidi kwa pointi sasa nataka kumonyesha kama ninauwezo wa
kumuangusha katika hatua za awali za pambano letu kwani nimejiandaa na
bado naendelea kujifua kwa ajili ya pambano hilo," alisema Maneno.
Naye kwa upande wake Rashid alisema, anaendelea kujifua ili kuweza
kuwapa raha mashabiki wake ikiwa na kuwapa zawadi ya Christimas kwa
kumtwanga kwa mara nyingine Maneno.
"Ushindi wangu ndio utakuwa zawadi kwa mashabiki wangu kwani
sinachazaidi cha kuwapa," alisema Rashid.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Adios Promotion, Shabani Adios 'mwayamwaya'
ambaye ndiye muandaaji wa pambano hilo, alisema kabla ya kufanyika kwa
pambano hilo mabondia hao watapima vipimo mbalimbali vikiwemo ukimwi
na madawa ya kuongeza nguvu ili kuweza kuwatayari kwa ajili ya
mpambano.
Mapambano ya utangulizi yatakuwa kati ya mabondia Venas Mponji
atakayezichapa na Tumaini Maguno 'SMG' na bondia Rashidi Ally
atazichapa na Kulwa Mbuchi, Selemani Jumanne na Ibrahimu Madeusi
wakati Shabani Zunga atavaana na Mohamedi Kashinde, na bondia Sweet
Kalulu na Saleh Mtalekwa
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki
kujua sheria za masumbwi.
Search This Blog
Wednesday, December 7, 2011
MATUMLA NA MTAMBO WA GONGO KUMALIZA UBISHI KRISIMASI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment