WAGOMBEA TUZO ZA FIFA BALLON D’OR 2011 WATAJWA – MESSI, RONALDO WAENDELEZA VITA.
Nominees wa mwisho wa kugombea tuzo za FIFA Ballon d’or 2011 katika category za mchezaji bora wa kiume wa mwaka 2011 na wa kike wametangazwa leo hiikatika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika makao makuu ya jarida ya mpira wa miguu la kifaransa mjini Paris, ambapo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke, France Football CEO Francois Moriniere, na wachezaji wa zamani Emmanuel Petit na Gaetane Thiney walishiriki katika kuwatangaza Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Xavi kama wachezaji waliofanikiwa kuingia katika top 3 ya mchezaji bora wa kiume, huku mbrazil Marta, Homare Sawa(Japan) na mmarekani Abby Wambach wakigombea tuzo mchezaji bora wa mwaka wa kike.
Katika hatua nyingine Sir Alex Ferguson, Josep Guardiola na Jose Mourinho wakigombea tuzo ya kocha bora wa mwaka.
Nominees hawa walipatikana baada ya kufanyika kwa zoezi la kupiga kura lilowahusisha manahodha na makocha wakuu wa timu za taifa za wanawake na wanaume za mataifa yenye uanachama wa FIFA.
Pia katika category nyingine ya goli zuri la mwaka maarufu kwa jina la Puskas Award itagombaniwa na Wayne Rooney, Lionel Messi na Neymar.
Tuzo hizi zitatolewa na kutangazwa mwezi January, 9, 2012.
No comments:
Post a Comment