Na Baraka Mpenja , Dar es sakaam
Maafande wa JKT Ruvu wamesema kwasasa malengo yao
makubwa ni kusalia ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kufanikiwa kuwafumua
Rhino Rangers mabao 3-1 wikiendi ya wiki iliyopita uwanja wa Azam Complex, uliopo
Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Kocha mkuu wa klabu hiyo, Fredy Felix Minziro
ameuambia mtandao huu kuwa sasa nguvu zao wanaelekeza katika mechi tatu
zilizosalia kuhakikisha wanavuna pointi sita na kubakika ligi kuu.
“Mchezo uliopita ulikuwa mgumu kwasababu timu ya
Rhino bado ilikuwa inapambana isishuke daraja, nadhani sasa wameshuka rasmi. Kama
nilivyosema malengo yetu ni kuhakikisha timu inabakia. Tuna imani katika
michezo iliyobaki tutafanya vizuri”. Alisema Minziro.
Minziro aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga mzunguko
wa kwanza msimu huu akiwa chini ya kocha mkuu, Mholanzi, Erne Brandts aliyetimuliwa
pamoja naye, aliongeza kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa katika mechi ijayoaprili
6 mwaka huu dhidi ya Yanga sc, kwenye
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
“Mechi hii itakuwa ngumu zaidi kwetu kwasababa Yanga
wataingia kwa machungu ya kufungwa na Mgambo JKT na kujiweka katika mazingira
magumu ya kutetea ubingwa wao”.
“Lakini mpira unachezwa uwanjani, hatutaingia
kinyonge bali tutapambana dakika zote kuhakikisha tunapata matokeo mazuri
JKT Ruvu wapo
nafasi ya 9 katika msimamo baada ya
kushuka dimbani mara 23 na kujikusanyia pointi 28.
Hata hivyo wanaonekana kuwa mazingira mazuri ya
kubakia endapo wataweza kuchanga vizuri karaka zao mechi tatu zilizosalia.
Wamebakiza mechi dhidi ya Yanga uwanja wa Taifa, Coastal Union
uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga, na kipute cha mwisho watavaana na vinara Azam fc
uwanja wa Azam Complex.
Katika mechi hizo tatu, michezo miwili dhidi ya
Yanga na Azam fc itakuwa mtihani mkubwa kwa kocha Minziro, kwasababu timu hizo
zinapigana kwa nguvu zote kutwaa ubingwa.
Yanga wenye pointi 46 wapo katika `presha` kubwa
kufuatia kuachwa kwa pointi saba na Azam fc waliopo kileleni kwa pointi 53.
Mechi ijayo wataingia kwa malengo ya kushinda,
lakini lazima wawe na tahadhari ili kutokumbana na mambo ya Mgambo JKT kule Tanga, `waja leo waondoka leo`.
No comments:
Post a Comment