Na Baraka Mbolembole
Mabepari wapo kila mahali, pia wana
misingi mikubwa ya kifedha, na mahusiano makubwa na vyombo vya umma. Kwa
mfano wana uhuru wa kutumia vyombo vya habari. Ila kama kiongozi
anakuwa akiwavutia watu, basi ni kwa sababu ni kwa sababu yeye mwenyewe
amavitiwa na hiyo kazi iliyo mbele yake. Watu ndiyo nguvu pekee
inayoweza kusaidia mabadiliko. Hivyo kiongozi anatakiwa kuwaunganisha
watu na kuwafahamisha kwamba umoja wao utasaidia kupata wanachotaka. Ila
watu nao wanatakiwa kuamka.
Katika soka la Tanzania, tunaweza kusema kuwa tumempata
mtu ambaye tulikuwa tukimuhitaji, kwani rais wa sasa wa Shirikisho la
Soka Nchini, TFF, Ndugu, Jamal Malinzi anaijua Jiografia ya Tanzania,
na analifahamu vizuri soka la nchi hii. Hivyo atakuwa anafahamu
mahitaji na mawazo yanayotakiwa ili kukuza mpira wa Tanzania. Malinzi
licha ya kutajwa kama kiongozi hodari baada ya kupita kwa zaidi ya siku
100 za utawala wake, ameonesha kuwa muhubiri hodari shupavu, na bila
shaka atakuwa mwanafunzi hodari pia. Na hili litawezekana endapo ataamua
kutumia muda wake kutazama na kujifunza zaidi kuhusu nini hasa
kinachotakiwa kuanza ili kupata msingi imara wa mpira wetu.
Soka mara zote linakuwa na mahitaji ya muda mfupi na
muda mrefu. Malinzi ameingia na mipango yake, huku soka la vijana
likiwa kipaumbele kikubwa kwake, na hapo Academy za soka anaamini ndiyo
suluhisho la kwanza. SAwa ni jambo zuri kwa kuwa ameingia huku akiwa na
kiu ya kufanikisha mipango aliyojiwekea. Sera yake kuhusu soka la vijana
ni nzuri, na ziara yake aliyoifanya siku za nyuma katika Academy ya
Allience Sports ya jijini Mwanza, ilirutubishwa na maneno mazuri kuwa
hapo ndiyo kutakuwa kitovu cha mpira wa Tanzania. Hadi sasa Malinzi
ameonesha kuwa mtu anayependa sana kazi yake, ila mikakati yake ni
lazima iendane na uhimarishaji wa soka la mitaani.
Jiografia ya Tanzania, bado mchezo wa soka unahitaji
unahitaji kuwekewa mkazo mkubwa sana katika ngazi za chini, kata,
tarafa, wilaya na mikoani, kwa kuwa uchumi wetu hauwezi kuendana na
mkakati wa Academy kwa nchi nzima. Vipaji ni vingi sana nchini. Labda
huu ni wakati wa kuanzisha ligi za vijana ambazo muendelezo wake utakuwa
hadi ngazi ya Kitaifa, kwa kuwa na michuano inayotambulika na si hii ya
muda mfupi kama ilivyo Copa Coca Cola. Mfano michuano hiyo ya Copa,
inaweza kufanyika kwa kipindi cha mwaka mzima kwa mtindo wa ligi. Ni
ghali sana, ila udhamini ambao makampuni yanapewa katika soka la
Tanzania unatakiwa kuendana na hali halisi.
Mitaani, ndipo soka linapotoka. Ndiyo maana
WAingereza wanataka kuhamia na kuweka nguvu zao zaidi katika soka la
mitaani kuliko lile la mfumo wa Academy. Muundo mzuri wa mfumo wa soka
uhusishe pia namna ya kuendeleza vipaji ambavyo kimsingi haviwezi kupata
nafasi katika Academy kuwa kuwa mambo ya uchaguzi huendana na
ukiritimba mkubwa kila mahali. Uzuri wa Academy ni kwamba vijana
watakuzwa na kuendelezwa katika mwendo mzuri wa kinidhamu, kutambua
majukumu na kuwajibika, ila siku zote ni lazima tutambue kuwa, kila
mtoto huzaliwa na tabia njema, tabia mbaya huja baadae. UNaweza
kuzalisha wachezaji 100 bora katika nchini na kujona umefanikiwa sana,
ila tabia zao kadri wanavyokuwa wakikua zinakuwa zikibadilika. Soka la
Academy ni muhimu, ila soka la mtaani ni tumaini la muda wote kwa mpira
wa Tanzania.
Majuzi nilikuwa nikiwasiliana na James Julius,
Mtanzania ambaye yupo nchini Afrika Kusini, akifanya kazi katika
Academy ya ' Stars of Africa'. Naye ameanza na mikakati ya kufanya
uwekezaji katika soka. Ameomba ekali zaidi ya 20 katika mji wa Mwanza
ili kuanza ujenzi wa ' Mandozi Sports Academy', maombi yake hayo
anataraji kupata majibu mwezi huu. Huyu ni kijana mdogo tu na tayari
ametumia zaidi ya millioni 20 kwa kuanzisha timu nne za vijana, U20,
U17, U14, na U12. Mimi alinipatia CD za hiki ninachokisema hapa na
nimeona mikakati yake. Hivyo kwa Malinzi, bila shaka tayari ametoa
mwamko na matumaini kuwa watu wamemuelewa na tayari wanatumia nguvu zao
kusaidia soka la Tanzania
Hapa ni makampuni yanayotakiwa kusaidia katika ili
na si kusubiri kujitokeza hapo baadae wakati wakiona kuna matunda ya wao
kutangaza biashara zao. Makampuni mengi yamekuwa yakijinifaisha kupitia
ufadhili wao katika soka la Tanzania, Hata udhamini wanaoupata timu
zetu mbili kubwa kwa sasa hauendani na thamani ya klabu hizo. Simba na
Yanga zinawaingia faida kubwa wadhamini wao kuliko kile wanachoingiza
wao kutokana na ufadhili au udhamini walionao. Makakati, wa Mandozi,
Sports Acacemy, Allience Sports Academy unatakiwa kusapotiwa kwa nguvu
na makampuni yaliyopo nchini. Yatafikaje, ni kwa wahusika wenyewe
kujitokeza na kuonesha kuwa wapo tayari kufanya kitu kikubwa hivyo
wanatakiwa kuyafuata makampuni hayo na kuyaomna yaende kuwasaidia.
WANAOSEMA TFF IMEJAA, U- SIMBA NA U-YANGA NAWASHANGAA
Hivi
ni nani anayeweza kuishi nje ya fikra za Simba na Yanga? Labda kwa yule
ambaye si mpenzi wa soka. Wakati mwingine sisi binadamu tunakuwa
wanafiki kweli. Nani hajui kuwa Jamali Malinzi amewahi kuwa kiongozi wa
juu wa klabu ya Yanga? Nani hajui kuwa Geofrey Nyange Kaburu amewahi
kuwa kiongozi wa juu wa klabu ya Simba> Vipi kwa kina Abbas Tarimba,
Seif Ahmed, David Mosha, Zacharia Hans Poppe, Clement Sanga, mimi
ninafikiri muhimu ni kuwashauri kuwa mpira wa Tanzania unawategemea sana
wao hivyo wanatakiwa kufanya kazi zao kutokana kanuni na taratibu
zilizopo. Wasiweke mapenzi ya vilabu vyao katika mambo muhimu.
Mimi, wewe, sote tumekuwa na upenzi wa soka.
Inategemea tu, wewe utakuwa unaangukia wapi katika mapenzi yako, inaweza
kuwa Simba, au Yanga ama timu nyingine yoyote ile. Ndiyo, Malinzi
amewavuta watu wengi wa Simba na Yanga katika kamati zake, ila si kwa
lengo la kuharibu mpira bali kupanga na kusimamia vuzuri mikakati
inayoweza kusogeza soka la Tanzania mbele zaidi. Ni makosa kumuhukumu
kwa sasa ila hatutosota kumsema vibaya endapo tunashuhudia kamati zake
zikifanya mambo kwa kuvutana kisa mapenzi ya u- Simba na u- Yanga. Kwa
sasa tuwasisitize wafanye kazi zao vizuri bila kusukumwa na ushabiki na
si kuwahuku kwa makosa yasiyokuwepo. Kama hatuwataki hao, kisa ni Simba
na Yanga, mleteni basi Sir Alex Ferguson aje kuwa rais wa TFF, kwa kuwa
watu wengi wa soka wanatoka katika mapenzi ya dhati ya Simba na Yanga.
Itakuwa ni makosa makubwa kwa Malinzi, endapo watu
aliowaamini na kuwapatia nafasi watamuangusha kisa ushabiki wa klabu
zao. Itakuwa ni sawa na muwindaji ambaye aliamua kuchukua mtoto wa Simba
na kumpeleka nyumbani kwake. Huyu atakuwa amejipelekea maangamizi yeye
mwenyewe na familia yake. Soka la Tanzania halihitaji wafanyakazi wa
mapenzi, ila ukweli ulio wazi linawahitaji watu waliopita Simba au
Yanga, iwe kiuongozi au kiuchezaji. Mkakati wa Malinzi na soka la
Tanzania unahitaji fikra zetu sote. Kulaumu kupo tu kila mahali, ila
nasi tutoe ushauri mzuri kwao ili kwenda sambamba na matarajio
yanayokusudiwa. Nimewasilisha tu. Karibuni pia Mandozi Sports Academy...
Kuwashangaa wanaokosoa soka la nchi hii hasa uongozi wake kujaa usimba na uyanga; sio tu unawashangaa, bali, ni lazima uwashangae kwani akili na mawazo yako yameumbiwa katika mkondo wa fikra mfungo, ambao moja ya tabia zake ni kushangaa hata lilo na uhakiaka ama ukweli. Nadhani fikra zinalenga kutetea kile ambacho kwa uwezo wake inaonekana ni sahihi hata kama si sahihi. Sio kweli kwamba kila mtanzania mwenye kupenda soka kaumbiwa katika fikra za usimba na uyanga. Kwa kauli hii ni kitu ambacho kitaalamu kinaitwa "fallacy of generalization". Wapo wadau wengi wa soka katika nchi hii ambao kwao ukiwagusia suala la simba au yanga, hakika wanaweza kukutandika vibao, kwani vilabu hivi viwili ndivyo vinavyoharibu soka la nchi hii. Kwa mtu mwenye kupenda maendeleo ya soka yu lradhi kuona vilabu hivi pengine vikipotea katika ulimwengu wa soka nchi hii. Soka la nchi hii limegubikwa na tabia mbovu za usimba na uyanga ambao ndio kaburi la kandanda letu. Hakika unapomchagua kiongozi au mchezaji aliyewahi kuwa sehemu ya jamii ya vilabu hivi, hakika unazidi kulichimbia kaburi soka letu na hata siku moja hawatakuja kufanya maamuzi pasipo kuathiriwa na lahana ya timu hizi. Vipo vilabu vidogo vidogo na hata vingine viko ligi kuu, ambavyo viongozi wake wanauwezo mkubwa wa kuliongoza taifa hili pasipo kuwa na dhana ya usimba au uyanga, lakini jambo la kushangaza, kiongozi huyu ambaye anachagizwa na watanzania wengi hakujaribu kuwaona watu hawa zaidi alichokifanya ni kuleta wale ambao amezoeana nao na pengine kufanya nao kazi. Kinachotegemeawa ni nini kama si kuliangusha soka la nchi hii na siku zote tutazidi kupiga kelele lakini mchawi tunamjua wenyewe lakini tuna mfumbia macho. Tazama marefa wengi wa nchi hii wamekuwa wakiamua mechi za ligi kwa ushambiki wa simba na yanga. na hilo ni wazi kabisa kwani wameonekana kupindisha kanuni au kufanaya makosa mengine yanashangaza, hasa kwenye mechi za timu hizi mbili. Lakini marefa haohao, wanafanya vizuri wanapochezesha mechi ambazo simba na yanga hawahusiki.TFF hao wakawakoromea watu ambao wanawalaumu waaamuzi lakini bado hawawaonyi waamuzi hao hao. Kama si usimba na uyamga ni nini?
ReplyDeleteUtakuwa ni unafiki kusema tuwaamini malinzi na hao washikaji zake ambao walishika nyazifa mbalimbali katika simba na yanga.hao wote wapo hapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi na si kwa ajili ya maendeleo ya soka la bongo,najua kwanini wanaojiita wadau wa soka la bongo hawataki kuona simba na yanga zinapata changamoto katika ligi kuu ya bara,kuanzia viongozi wa TFF hadi baadhi ya WAANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO hapa bongo ambao wamekosa nia ya dhati katika kuripoti hali halisi na upuuzi tunaoletewa miaka yote na hizi klabu mbili ambazo binafsi naziona ndo kiini cha kudidimia soka letu,Ebu tujiulize huyo malinzi na hao wasanii wenzake aliowajumuisha kwenye kamati mbalimbali za TFF kipindi ambacho wapo simba na yanga walileta mabadiliko gani katika kuendeleza hizo klabu za kishamba? wakati umefika sasa tuache ujinga wa kuwaamini watu kama hao kizembezembe,ni jambo la kushangaza watu walioongoza simba na yanga miaka mingi iliyopita ambapo bado simba na yanga hadi leo hazina maendeleo yoyote ya kujivunia zaidi ya mataji ya ligi kuu bara ambayo tukiacha unafiki wamekuwa wakionga wachezaji wa timu pinzani pamoja na marefa,wakifika kwenye michuano ya klabu ya kimataifa ni aibu tupu,HIVI TFF HAIWEZI KUONGOZWA NA WATU WENGINE MAKINI HADI TUWACHAGUE HAO WALIOTOKA KUVURUNDA KWENYE KLABU ZA WASHAMBA ZA SIMBA NA YANGA? Binafsi naona hakuna umakini wowote kwenye hili na hao wajumbe wa TFF ni tamaa za kipuuzi tu zinazowafanya watuchagulie viongozi mizigo.siungi mkono hata kidogo kuturudishia akina ABBAS TARIMBA kwenye zama hizi ambazo wapo watu makini wanaoweza kutufikisha pale tunapohitaji,TFF IMEJAA USIMBA NA UYANGA NA SISI WAPENDA MAENDELEO YA SOKA LA BONGO TUNAKUSHANGAA WEWE AMBAYE UTAKI KUKUBALI UKWELI KWAMBA SIMBA NA YANGA NI GONJWA SUGU KWENYE SOKA LA BONGO,mabadiliko na maendeleo yatapatikana mkiacha kulazimisha kuzisifia kijingajinga.
ReplyDeleteNmekuelewa baraka. To tell the truth, hiwezi kutenganisha soka la nchi hii na simba na yanga. Anyone antajie just kiongoz mmoja ambaye hayupo upande wowote... Na ukickia kiongoz anasema yupo neutral, utagundua ni mnafki 2. Waulize watu wake wa karibu watakwambia... Itz hard truth 2 swallow bt u hav 2.. Kinachotakiwa ni kwa hao viongoz kuelewa kuweka boundaries kati ya kazi na mapenzi binafsi, na inawezekana coz sidhan kama sepp blatter hapend mafanikio ya sweden national team. Bt ni lazma afanye kaz yake... Watu wa mpira ndo hao hao, unamteua nan mwngne? May b tuchukue watu wa basketball waongoze mpira wetu.
ReplyDeleteYani katika watu wanaojisemea ovyo ni pamoja na huyu jamaa mchangiaji wa kwanza anayesema eti Simba na Yanga ndo wanaharibu soka la tanzania. Haya ni maneno ya kijinga ambayo yamezoeleka kutamkwa na watu wa hovyohovyo bila kuzingatia ukweli halisi. Nawachukia sana vilaza wa namna hii. Wengi wao wanaugonjwa unaojulikana kitaalamu kama "cognitive disonance"
ReplyDeleteMwalimu Nyerere aliwashangaa viongozi aliowaachia nchi kwa kuchukua mambo mabaya aliyoyafanya katika uatawala wake na kuyaacha yale mazuri.Mfano huu unamhusu Malinzi ambaye badala ya kuchukua mazuri yaliyofanywa na Tenga ameamua kukumbatia makomandoo wa Simba na Yanga na kuwajaza kwenye kamati zake na sasa wameanza kumpa ushauri wa kipuuzi na yeye kuukubali kama ule wa kuacha kutumia tiketi za elektroniki.Sio kweli kwamba nchi hii watu wanaojua mpira ni wale waliowahi kuongoza Simba na Yanga tu.Wako watu wengi wameongoza vilabu na vyama vya mpira nje ya simba na yanga kama Mbeya City,Kagera Sugar,Majimaji,Coastal Union,JKT Ruvu,Mtibwa n.k na unahitaji kuwa makini lil kuwapata vinginevyo utakurupu
ReplyDeletekia watu wale wale wa kila siku kama Tarimba,Dalali,Hanspope,Madega,Sauko n.k ambao hakuna lolote walilofanya la maendeleo ya soka kwenye klabu zao.Hawa ndio wameharibu huko na sasa wanaaminiwa kwamba eti watalikomboa soka la nchi hii kupitia kamati za TFF.Malinzi mwenyewe sio mtu wa soka ni mbabaishaji(opportunist) aliyetokea kwenye upromota wa ngumi za kulipwa aka"chance" kuingia kwenye soka mwanzoni mwa miaka ya 2000 kwa nguvu ya fedha zake na kupitia makomandoo wa Yanga lakini leo hii anaonekana ndiyo suluhisho la soka la Tanzania akiwazidi watu aliowakuta kwenye soka kama kina Tenga,Nyamlani,Angetile n.k.HIVI UNATARAJIA MAENDELEO GANI YA SOKA KUTOKA KWA MADEGA AMBAYE MWAKA 2008 ALIDIRIKI KUZUIA TIMU ISENDE UWANJANI KUCHEZA MECHI YA KOMBE LA KAGAME KWA SABABU ZA KIPUUZI,LEO HII NI KIONGOZI WA KAMATI MUHIMU YA TFF.Hivi huyo Dalali na Hanspope si walizuiwa kugombea uongozi Simba kwa kukosa siafa za kikatiba lakini leo hii ni viongozi wa soka wa kitaifa kupitia kamati za TFF.Haya hao kina Tarimba,Sauko n.k si ndio hao hao miaka nenda miaka rudi wamevuruga soka la Tanzania kwenye ngazi ya klabu? Malinzi aliahidi kuileta mabadiliko kwenye uendeshaji wa soka lakini KAANZA NA MGUU MBAYA kwa kujaza makomandoo walewale wa simba na yanga kwenye kamati zake huku wakimpa ushauri wa hovyo na yeye anakubali
Bw. J. Malinzi anaonekana kua kiongozi bora, na anaonekana kua na nia dhati kabisa ya kuukwamua ama kuuendeleza mchezo wa mpira wa miguu Tanzania. Ombi langu ni kua aache kusikiliza ama kufuatilia maneno maneno ya watu, afanye kazi na sio kusikiliza nani kasema lipi na yupi kasema lipi juu yake.mfano mbona Mheshimiwa raisi wa nchi amekua akishutumiwa kila kona anawatoto ama ata akiteua mwanamke ktk nyadhifa za uongozi watu wamekua wakidai kua ni awala yake ama aliwai kua kimada wake, lkn je ashawahi kujibu shutuma hizo...ukweli sijawahi sikia akijibu na hii imekua ikimfanya awe huru na kusonga mbele.
ReplyDeleteNakusihi Malinzi waache wapige mayoe wakichoka waataacha, na hakika hata ukitaka kuwaweka sawa hutoweza maana wapo wengi wasio penda mafanikio ya mtu aliye onesha nia. alishindwa yesu utakua wewe bwana. Piga kazi tubadilishe soccer ya nchi yetu.
Malinzi na Kikwete wapi na wapi?,Malinzi hajui mpira na anaongozwa badala ya kuongoza.Kila ushauri wa kijinga anaopewa anaufanyia kazi matokeo yake kamaliza siku 100 hana cha kujisifu zaidi ya kuanza kuwalaumu kina Tenga kwa kumuachia madeni
ReplyDelete