Na Arone Mpanduka,Radio Tumaini
MCHEZO wa ngumi ni sanaa ya ulinzi binafsi baina ya
mtu ambaye anatumia mikono yake miwili katika mapigano ambapo kwa lugha ya
kigeni wanasema "the manly art of self-defense"
Mchezo huu ulianza katika karne ya 17 na kuanza
kufahamika katika karne ya 18 huku chimbuko lake likiwa nchini Ugiriki.
Ngumi ulikuwa ni mmoja kati yak michezo ya mwanzo
kuingizwa katika mashindano ya Olimpiki katika miaka ya 688 BC.
Wakati huo mabondia walikuwa wakipigana kiholela
bila sheria na kanuni za kueleweka sanjari na vifaa duni vya kupigania.
Wagiriki waliweza kubuni gloves za aina yake ambapo
walianza kuvaa ngozi za wanyama kwenye mikono yao zilizokuwa zikifahamika kama
cesti.
Lakini kuna mabondia wengine walikwenda mbali zaidi
na kuchomeka vitu vyenye asili yak chuma katika ngozi hizo na kuleta madhara
makubwa kwa wapinzani wao wakati wa mchezo kwani vyuma hivyo vilikuwa
vinajeruhi vibaya na hata kusababisha kifo kwa mpinzani.
Baada ya kugundulika kuwa ni mchezo wa hatari
ililazimika kuufungia kwa muda kabla yak kuibukia katika nchi zingine ikiwemo
Uingereza pamoja na nchi nyinginezo.
Nchini Uingereza bondia James Figg aliweza kutamba
na mkanda wa uzito wa juu kuanzia mwaka 1719 hadi 1730.
Mchezo huo ulizidi kukua na kuenea nchi mbalimbali
duniani huku sheria na kanuni zikitengenezwa na kuboreshwa na baadae kuufanya
kuwa mchezo wa kisasa.
Hivi sasa ngumi imekuwa na majina mengi kama vile
masumbwi, ndonga, ndondi, mkono, vitasa na wengine hudiriki kuita mawe.
AINA
ZA MCHEZO HUO
Mchezo wa masumbwi umegawanyika katika aina kuu
mbili ambapo ni pamoja na ngumi za ridhaa na zile za kulipwa(Amateur and
Professional)
Licha ya kuwepo kwa aina hizo kwa ujumla mchezo huu
una wastani wa kuchezwa katika raundi 12 ambapo kila raundi ina muda wa dakika
tatu na kila baada ya raundi moja mabondia hupumzika kwa dakika moja.
Pia ipo michanganuo mbalimbali ua uzito ambayo
bondia hushindana kulingana na uzito alio nao kama vile Flyweight (50.8 kg);
Bantamweight (53.5 kg); Featherweight (57.2 kg); Lightweight (61.2 kg);
Welterweight (66.7 kg); Middleweight (72.6 kg); Light Heavyweight (79.4 kg)
pamoja na Heavyweight.
ULINGO
WA MASUMBWI
Kama ilivyo katika michezo mingine ambayo lazima iwe
na uwanja wa kuchezea, katika masumbwi nako uwanja wake upo ambao ni ulingo.
Ulingo huwa na pembe nne zenye kuzungushiwa kamba
ngumu pembeni yake na huusisha watu watatu ndani yake yaani mabondia wawili na
mwamuzi.
Nje ya ulingo mwamuzi husaidiwa na majaji watatu
ambao nao huutazama mchezo na kila mmoja kutoa alama zake.
KWANINI
UITWE BOXING RING?
Watu wengi wamekuwa wakitamka neno la Boxing Ring
wakimaanisha ulingo wa masumbwi wakati kimuonekano ulingo huo una pembe nne.
Kama inavyofahamika, maana halisi ya ring ni pete
ambayo mara zote huwa na umbo la duara.
Ukweli ni kwamba katika karne ya 18 na 19 mabondia
wengi walikuwa wakicheza pambano hilo huku wakiwa na vifaa duni ikiwemo ukosefu
wa gloves, sare na hata ulingo wa kuigania.
Kilichokuwa kinafanyika ni kwamba mwamuzi wa mchezo
anachukua kijiti na kisha anachora duara kubwa ardhini na kisha mabondia
huingia ndani yake na kupigana huku watazamaji wakizunguka duara hilo.
Hapo ndipo neno Boxing Ring ilipoibuka kwasababu
mabondia walikuwa akipigana kwenye uwanja wa duara.
Mazoea hayo yaliendelea kuchukua nafasi hata
ilipofika kipindi ambacho ukagunduliwa ulingo wa pembe nne ambapo bado
mashabiki wakaendelea kuuita Boxing Ring.
Ulingo wa kwanza wa pembe nne ulibuniwa na jamii ya
watu wa Pugilist mnamo mwaka 1838 ambao ulikuwa na eneo la ukubwa wa mita 7.3
za mraba.
0786160643
No comments:
Post a Comment