Search This Blog
Monday, February 10, 2014
NIONAVYO MIMI:KUNA MUDA WAAFRIKA TUNAJIANGUSHA WENYEWE KWENYE SOKA
Na Oscar Oscar Jr
Mataifa 8 pekee ndiyo yamewahi kutwaa ubingwa wa Duniani na kila kocha aliyetwaa kombe la Dunia,alikuwa mzawa wa Taifa hilo.Ingawa soka ni mchezo wa maajabu lakini ukweli utabaki pale pale,unaposhiriki kombe la Dunia na kocha wa kigeni kihistoria,tayari ulishalikosa kombe hilo!
Juzi nimepata taarifa za kufukuzwa kazi kocha mzawa wa Ethiopia,Sewnet Bishaw nilishang'aa na kuhuzunika! Bishaw alipewa timu mwaka 2011 na katimuliwa mwaka 2014.Ethiopia walishiriki mara ya mwisho AFCON mwaka 1982,hawajawahi shiriki kombe la Dunia wala CHAN.
Ndani ya muda mfupi,Bishaw ameibadilisha Ethiopia.Amewafanya wacheze AFCON kule Afrika kusini 2013,ameifikisha Ethiopia hatua ya mtoano kuelekea kombe la Dunia Brazil ingawa alitolewa na mabingwa wa Africa Nigeria na pia,amewafanya wacheze CHAN 2014 kwa mara ya kwanza kule Afrika ya kusini.Hivi walitaka afanye nini zaidi?
Sina ugomvi na makocha wa kigeni lakini,kocha mzawa kwenye timu ya Taifa inamantiki zaidi.Jamal Malinzi Rais wa TFF kateuwa jopo la wazawa kwa lengo la kuibui vipaji ili baadae tuwe na timu imara ya Taifa,nakubaliana na hili lakini vipaji tuviibue wazawa then kazi akatufanyie mgeni??
Misri ni wafalme wa soka la Afrika,wameshinda AFCON mara 7 na ushindi wao wa kifalme ni wa hivi karibuni tu mara 3 mfululizo 2006,2008 na 2010 wakiwa na kocha mzawa Hassan Shehata.Ghana wameshinda mara 4 AFCON wakiwa na makocha wazawa.
Malawi hawajawahi kushiriki Kombe la Dunia lakini wamewahi kushiriki AFCON mara 2 na awamu zote,walikuwa chini ya makocha wazawa.Mafanikio ya siku za hivi karibuni ya Nigeria ni matunda ya Stephen Keshi na Daniel Amoukach na benchi lao la ufundi lililojaza wazawa.
Mecky Mexime,Juma mwambusi,suleyman Matola,King Kibaden,Charles Mkwasa n.k ni makocha wazawa ambao wakipewa mikakati,wakaaminiwa,wakapewa muda,wakawezeshwa kama wageni wanavyotunzwa,ninaamini tunaweza kusogea mbele.
Nakubali kwamba hata nchi za Ulaya zipo zinazotumia makocha wa kigeni lakini je,wamefanikiwa nini kwenye kombe la Dunia? unadhani ubora wa makocha wa kigeni wanaofundisha nchi za Ulaya ni sawa na hawa wanaokuja kwetu Afrika?
Naheshimu mchango wa kocha Mrusi Valeri Nepomniachi kwa kuifikisha Cameroon robo fainali ya kombe la Dunia 19990,Mfaransa Bruno Metsu aliifikisha senegal 2002 na Msebia Milovan Rajevac aliifikisha Ghana 2010.
Mafanikio makubwa ya Simba CAF 1993 yaliletwa na mzawa King Kibaden,mafanikio ya Taifa Stars kushiriki AFCON 1980 yaliletwa na mzawa Joel Bendera.Ukimpatia timu ya daraja la kwanza Kim Poulsen na ukampatia bajeti yakawaida sawa na Suleyman Matola,kuna uwezekano timu ya Matola ndoitakayoanza kupanda daraja,i'm sorry!
Asante Marcio Maximo kwa kuipeleka Taifa Stars CHAN lakini,ukweli utabaki pale pale makocha wakigeni wanasikilizwa ziadi na viongozi wa klabu na Taifa kuliko wazawa.Mpe kocha wa kigeni wa Yanga Jkt Oljoro au yule wa Simba Tanzania Prisons uone watakavyojikanyaga.i'm sorry
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kocha aliyeiwezesha Taifa Stars kufuzu AFCON 1980 siyo Joel Bendera bali ni Slawomir Wolek wa Poland na Msaidizi wake marehemu Raymond Gama.Kocha Wolek ndiye alikuwa kocha mkuu wakati Taifa Stars inazitoa Mauritius na Zambia na kufuzu kwa fainali hizo.Joel Bendera alipewa timu hiyo wakati inakwenda kushiriki fainali hizo Lagos
ReplyDeleteHiki ni kichekesho kwamba wataalamu 40 watakwenda kuibua vipaji vya kuja kuchezea timu ya Taifa.Hakuna kitu kama hicho duniani sababu mwisho wa siku kocha wa timu ya taifa ndiye anayetua kikosi kwa kuzingatia aina ya mfumo anaotaka kuutumia.
ReplyDelete