Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji amewaomba wadhamini wa klabu hiyo,
kuangalia upya mkataba wa Azam TV, kwani kwake yeye binafsi anauona hauna
manufaa kwa klabu yao ambayo inaingiza zaidi ya mil 300 katika mchezo mmoja
akitolea mfano mchezo kati yao na Watani zao Simba.
Baada ya kusema hayo, Manji
aliwataka wanachama kutoa maoni yao juu ya suala hilo, ambapo Patric Mandewa kutoka
Mwembeyanga aliunga mkono hoja ya Manji na kusema kuwa, hawaoni faida ya
kuchukua mil 100 kutoka Azam TV wakati wao ni klabu kubwa ambayo inauwezo wa
kujisimamia na katika mechi moja ikapata zaidi ya fedha hizo.
Mbali na hayo, wanachama wakiongozwa na
Tuni Bakar ‘Mama Tuni’ walilazimika kumpigia magoti Manji ili kumuomba kupangua
kauli yake ya kutotaka kugombea tena, nafasi ya Uenyekiti ambayo bado
anaishikilia mpaka sasa baada ya aliyekuwa Mwenyekiti Loyd Nchunga kujiudhuru.
Licha ya wanachama hao, kumtaka Manji
kupangua kauli hiyo, Manji aliendelea na msimamo huohuo huku akiwataka
wanachama kuachana na hoja hiyo kwani haina mashiko katika maendeleo ya Yanga
kwa kuwa uongozi ni demokrasia, na kujikuta akiharibu hali ya hewa baada ya
kauli hiyo na wanachama kuanza kuondoka ndani ya ukumbi huo.
Baada ya wanachama kuondoka, Mc wa
Mkutano huo, Bakiri Makere aliwataka wanachama kutulia huku akisema ‘Yanga
Oyeee’ na kujikuta akikosa wa kumjibu kama ilivyokuwa awali kabla ya Manji
kujibu kwa msisitizo kuwa hatagombea tena kiti hicho.
Uongozi wakili kikosi kuwa dhaifu….
UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umekiri
kikosi chao kuwa na uwezo wa mchezaji mmoja mmoja huku wakidai hiyo ndiyo
sababu ya timu yao kutofanya vema katika michezo mbalimbali ambayo imechezwa
hivi karibuni licha ya kuongoza ligi.
Hayo yalisema na Makamu Mwenyekiti wa
Yanga, Clement Sanga, ambaye aliwaweka wazi wanachama wa klabu hiyo, sababu za
kutimua benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu Ernie Brandts na msaidzi wake Fred
Felix ‘Minziro’.
Sanga alisema, walifikia hatua hiyo,
baada ya kuona benchi la ufundi linashindwa kufanya kazi na kujikuta wakipanga
vikosi kwa mazoeza bila ya kutazama uwezo wa mchezaji mwenyewe na kuangalia
majina.
“Timu ina wachezaji wazuri lakini ni
mmoja mmoja, timu haichezi kitimu ni ngumu kufanya vizuri, na ndio maana
tukachukua hatua hiyo, na huu ni mwanzo kwani hata wachezaji wenye utovu wa
nidhamu atautaangalia jina la mtu wala nini tunamwajibisha tu,”alisema Sanga na
kuongeza kuwa, hata wachezaji wanaocheza mchangani watawashughulikia.
No comments:
Post a Comment