RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) Jamal Malinzi, amezitaka klabu hapa nchini, ambazo zitatoa wachezaji wa
timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya AFCON zikubaliane na hali
halisi ya mabadiliko ya ratiba ya michuano hiyo.
Malinzi aliyasema hayo katika Mkutano
wa Yanga akiwa kama Mgeni Rasmi alisema, ni vyema klabu zikafahamu ratiba hiyo
ambayo kwa namna moja ama nyingine inaweza kuathiri ratiba ya Ligi Kuu Tanzania
Bara inayotarajia kuanza Januari 25 mwaka huu.
Alisema, kuna uwezekano wa wachezaji
kuchukuliwa wakati timu zao zinacheza Ligi, hivyo basi akizitaka klabu zote
kujiandaa kwa usumbufu huo wa kuwaruhusu wachezaji endapo watafanikiwa kuitwa
katika timu hiyo ya Taifa.
Katika hatua nyingine, Malinzi
amewataka wanachama wa klabu mbalimbali hapa nchini kuheshimu katiba za klabu
zao na kuwaacha viongozi waliowateua kuwatumikia mpaka muda wao
utakapomalizika, kwani migogoro ni ngumu kujenga timu na ndio sababu ya
kutokuwa na wachezaji wazuri wa timu ya Taifa kutokana na migogoro hiyo.
“Klabu muache migogoro, kaeni mjenge
timu zenu, kuanzia timu za vijana kwani programe ya TFF kwa sasa ni vijana
kwanza, nawaomba Yanga na wadau wote wa Soka mlioko hapa tushirikiane katika
hilo,”alisema na kuongeza kuwa, wameamua kuanzisha tiketi za kierektroniki ili
kuzifanya klabu kunufaika na mapato ya viwanjani huku pia akizitaka klabu
kutafuta vyanzo vyao vya mapato.
No comments:
Post a Comment