KILA
kocha ana taratibu na aina ya ufundishaji ambao anaamini ni bora na wenye
manufaa kwa timu husika. Ufundishaji huo huenda sambamba na mazingira na
ufahamu wa kocha.
Siku
moja nilipata nafasi ya kulonga na kocha Stewart Hall wa Azam FC, raia wa Uingereza anayeamini kutumia mfumo wa
4.3.3 ni bora kuliko 4.4.2 katika kujenga timu bora na imara hasa barani
Afrika.
Hall,
anasema anachotaka ni kuijenga Azam FC kuwa timu yenye kucheza mpira wa
kuvutia, kuburudisha utakaotumia zaidi mtindo wa kulinda na kushambulia.
“Nataka
timu icheze mchezo wa kasi, mabeki imara watakaotoa mipira kwa viungo
itakayokwenda moja kwa moja kwa washambuliaji,” anasema Stewart.
Anasema
kupitia mfumo wa 4.3.3 utajenga kasi ya mchezo itakayosaidia timu kufanya
vizuri, akiamini ni mfumo anaoutumia siku zote anazofundisha timu na umeweza
kubadili timu zote alizozifundisha.
“4.3.3
ni mfumo mzuri na wenye mafanikio, mfumo nilioutumia nikiwa na Zanzibar Heroes,
ni mfumo unaowapa nafasi wachezaji wote uwanjani kucheza mpira bila kumtegemea
mchezaji mwingine,” Stewart.
Akizungumzia
uwezo wa wachezaji kwenda sawa na mfumo huo, anasema, wachezaji ni watu wa
kufundishwa na wanafuata mfumo wa mwalimu, anawapa mazoezi ya kutosha kucheza
mfumo huo.
“Ni
vigumu kwa mchezaji aliyezoea 4.4.2 kucheza 4.3.3, nawapa mazoezi mengi, kila
siku wanacheza mechi kujifunza mfumo huo, wameshaanza kuuelewa na kuufurahia.”
Stewart.
Kocha
Stewart anasema uhusiano mzuri wa wachezaji na kocha ni nguzo bora ya kukuza
uelewa kwa wachezaji wake, anatumia muda mwingi kuwa karibu na wachezaji wake
ili kurahisisha kazi yake na kuwabadilisha wachezaji kuwa professional.
No comments:
Post a Comment