Na BARAKA MBOLEMBOLE
Kiungo- mlinzi wa timu
ya soka ya Coastal Union, Abdi Banda, amesema kuwa timu yao ni nzuri kila
idara, lakini wamekosa bahati tu katika ufungaji wa mabao. Banda aliyasema hayo
kabla ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania Bara,
ambao klabu yake ilipoteza katika uwanja wa Chamanzi, dhidi ya timu ya JKT
Ruvu.
Coastali ilifungwa bao 1-0,
huku kwa mata nyingine wakionesha kiwango cha chini katika ufungaji. Wakiwa
wamefunga mabao 10 tu katika michezo 13, Coastal imeonekana kuwa na safu
ngangari ya ulinzi katika mzunguko wa kwanza kuliko timu nyingine zote,
wameruhusu mabao saba tu hivyo kuwa na wastani wa mabao matatu katika michezo
yote ya mzunguko wa kwanza.
" Coastal ni timu nzuri
tu. Tumejipanga kuanzia idara ya linzi, kiungo na ushambuliaji ila kwa safu ya
mashambulizi kwa sasa tumekosa bahati ya kufunga. Tutakaa sawa tu" anasema
mlinzi huyo wa kushoto, na mtoto wa mchezaji wa zamani wa timu za Africans
Sports ya Tanga, Simba, Malindi ya Zanzibar, TPC Moshi, na timu ya Taifa ya
Tanzania, Hassan Banda ambaye alikuwa mlinzi mahiri wa kati hasa katika nafasi
za namba nne, na tano.
Wakati akifanya mahojiano na tovuti
hii, Banda ambaye ameweza kucheza michezo 11 kati ya 13 ya klabu yake msimu
huu, na kutengeneza mabao zaidi ya matao huku akifunga bao moja. Mlinzi huyo wa
kushoto anaseme kuwa siri kubwa ya mafanikio yake ni kufuata maelekezo ya
walimu wake, huku akitumia muda mwingi kuchunguza wachezaji wa timu nyingine
kabla ya kukutana nao uwanjani na anakumbushia namna alivyokuwa makini na
kiungo mashambuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga, Saimon Msuva na kusema kuwa
alimchunguza mara tu alipojua kuwa atakabiliana naye.
" Mimi napojua tu
kuwa tunacheza na timu fulani, basi huwa napendelea kujua mawinga wao ni hatari
katika kipi. Ndiyo maana hata nilipokutana na Msuva naamini hakujua kama
tayari nilikuwa nimemfuatilia muda mrefu. Nilipunguza kupanda mbele sababu
ukimuacha kidogo tu ni hatari, ana spidi na ujanja mwingi. Napendelea kupanda
mbele na kuongeza mashambulizi kama naona kuna udhaifu kwa timu pinzani, naweza
kufunga mwenyewe au kutoa pasi ya mwisho napofanya jaribio la kusonga mbele.
Kama uliona gemu yetu na Yanga sikupanda sana kwa kuwa nilikuwa
nikifahamu madhara ya kumuacha Msuva kuwa huru"
Banda alianza kuupenda mchezo
huu akiwa na umri wa miaka 14, na hapo akatumia nafasi ya kuwa katika familia
ya soka kuuprnda zaidi mchezo huu. Mtoto wa Nyoka ni Nyoka tu. Aliibukia timu
ya Vijana ya Kombozi na baadae akapata nafasi ya kuichezea Sports timu hasimu
na Coastal na aliyowahi kuichezea baba yake mzazi, Hassan miaka ya nyuma na
hapo ndiyo akasajiliwa na timu ya Coastal kama mchezaji wa timu ya vijana U20.
" Nilianzia soka langu
katika timu ya Vijana, nikachezea Africans Sports kwa nusu msimu ndipo
nikasajiliwa na Coastal. Sikuwa na jinsi mimi kucheza Coastal ( akikumbushia
uhasimu wao na Sports), nahitaji kusonga mbele zaidi katika mchezo wangu. Na hii
ilikuwa ni nafasi maalumu kwangu. Kutoka ligi daraja la chini hadi kusajiliwa
na timu ya ligi kuu ni bahati kubwa sana kwangu, namshukuru Mungu."
Anasema mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 18 kwa sasa ambaye tayari amecheza michezo 21 ya ligi kuu, katika
muda wa miezi isiyozidi 12.
" Nilijiunga na Coastali
msimu uliopota, wakati huo kama mchezaji wa timu ya U20. Nilifanikiwa kucheza
michezo 10 msimu uliopita, na hadi sasa msimu huu nimecheza michezo 11. Na
tayari nimechukua namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza"
Wakati kocha wa timu ya Taifa,
Kim Poulsen akitangaza orodha ya wachezaji wa vikosi vya Future Taifa Stars na
kile cha timu ya Taifa Stars, makipa wawili wa timu ya Azam, Aishi Munula na
Mwadini Ally wameitwa, huku kipa aliyepoteza umakini na kujiamini Ally Mustafa
wa klabu ya Yanga pia ameitwa. Zaidi ni pale ambapo katika orodha ya makipa
zaidi ya watani jina la kipa Shaaban Kado halipo katika orodha hiyo. Kado
amekuwa ni sababu ya Coastal kuwepo hapo ilipo kwa sasa kutokana na uhodari wake
wa kuzumia mashambulizi ya timu pinzani.
Pia wakati beki majeruhi wa
Simba, Miraji Adam akiitwa katika moja ya vikosi hivyo, jina la Banda halipo
katika orodha hiyo. Banda anasemaje kuhusu hilo.
" Kado ni kipa mzuri sana,
anajua sana kutupanga mabeki wake. Kitu ambacho kinaniumiza kichwa ni kwa nini
sipati nafasi ya kuchaguliwa timu ya taifa. Ila naamini wamenishikia nafasi
yangu tu. Mimi ndiyo namba tatu wa timu ya taifa. Muda ukifika nitaitwa tu si
shaka yoyote" anasema na kuongeza kuwa yeye ni mchezaji hatari.
" Mimi ni mchezaji ambaye
nina uwezo wa kupiga pasi za mwisho nikiwa nyuma kabisa, kufunga mabao na
kusaidia wenzangu kufunga. Ninauwezo wa kupiga mashuti ya umbali mrefu, mipira
ya faulo na kuisadia timu katika mashambulizi na kujilinda pia"
Simba na Yanga zipo katika
fikra za wachezaji wengi nchini na pengine wa Afrika ya Mashariki yote kutokana
na historia ya klabu hizo. Ni kama tu kwa wachezaji nyota duniani wanapokuwa na
ndoto za kuichezea klabu kama Real Madrid ya Hispania, na hata hapa kwetu
wachezaji wengi wana ndoto hiyo vipi kwa Banda?
" Mimi nataka kusonga
mbele na pengine kucheza ng'ambo,. Nina miaka mitatu katika mkataba wangu na
Coastal ila kuna kipengele ambacho kinaruhusu mimi kuhama endapo kuna timu
itakuwa imenivutia na yenyewe kunipatia dau kubwa na kuhitaji huduma yanga.
Simba na Yanga? Siwezi kusema, ila Azam na hata Mtibwa popote naweza kucheza
kama watafikia makubaliano na meneja wangu, Abdul Bosnia"
Huyu, Bosnia ni nani hasa....
" Ni meneja wangu. Amewahi kucheza na baba yangu katika timu ya Sports.
Amekuwa akinisapoti muda mrefu ni mtu muhimu sana kwa maendeleo yangu
"
"
Anawazungumziaje, Juma Nyosso, Jerry Santo na Haruna Moshi?
" Kucheza na
wachezaji hao katika timu moja kumenifanya nijiami zaidi. Wamekuwa wanikiambia
nifanye mambo yenye malengo kwa ajili ya mpira wangu katika siku za usoni.
Wametokea kuniamini sana na kila mchezaji kijana kama mimi katika timu
anajivuania kucheza kando yao. Ukitazama ushindani uliopo msimu huu utaona
umuhimu wao kwetu ni wachezaji ambao wametufanya kuweza kuhimili vishindo vya
ligi kuu msimu huu"
Pia mlinzi huyo anamtupia sifa nyingi kocha aliyemaliza muda
wake, Hemed Morocco na kumuita kama mtu wa muhimu sana kwake. "
Nawashukuru wazazi wangu kwa kunisapoti hadi hapa nilipo sasa, meneja wangu na
kocha Hemed Morocco, aliniamini sana sitamsahau"
No comments:
Post a Comment