Search This Blog

Tuesday, November 19, 2013

BAADA YA RAGE - JULIO NA KIBADEN WAENDA NA MAJI SIMBA - MATOLA NA MCROATIA KURITHI MIKOBA YAO


Leo asubuhi zilitoka taarifa kwamba klabu ya Simba kupitia kamati ya utendaji imemsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo Ismail Aden Rage kutokana na kamati hiyo kukosa imani nae juu ya utendaji wake.

Muda mfupi baada ya kusimamishwa kwa Rage, viongozi wa klabu hiyo waliandaa mkutano wa waandishi wa habari ambapo pia makocha Abdallah 'King' Kibaden na Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ wameondolewa kwenye timu na nafasi yao itachukuliwa na aliyekuwa kocha Gor Mahia ya Kenya Zdravko Logarusic atakayetambulishwa Desemba 1, mwaka huu akisaidiwa na kocha wa timu B Selemani Matola.

Kuhusu Rage, kaimu makamu mwenyekiti wa Simba Mzee Kinesi amesema kwamba uongozi umekosa imani na Rage na hivyo walikaa kikao jana na kufikia maamuzi ya kumsimamisha, pia hawajaridhishwa na ufundishaji wa Julio na Kibaden ndio maana wanawaondoa. Rage ambaye hakuwepo katika kikao cha jana nafasi yake itakaimiwa na Mzee Kinesi sasa mpaka hapo mbele utakapochukuliwa uamuzi mwingine.

2 comments:

  1. Maskini Thimba Weee, kitakachotokea hapo ni vurugu tupu, maana Aden ana watu wake na wao watawafukuza akina Kinesi.

    Mpira wetu sjui tumerogwa. kwa nini walimuacha katika mkutano mkuuu
    au aliwapa kitu kidogo.

    sasa sijui kama katiba inawaruhusu? Duhhh Tanzania na Thimba na Yanga Hatufiki popote pale.

    Kama ingewezekana zingefutwa hizi timu ili watu wajipange kwenye timu nyingine.

    ReplyDelete
  2. gabriel umeniuaua, japo mimi ni thimba daaamuu!
    Jiniaaz!Popkorn

    ReplyDelete