Kuonesha kipaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania,
Wadau wa soka.
Meneja Mahusiano wa Man United, Michael Higham akizungumza katika hafla ya kuzindua shindano la ‘Airtel Mimi ni Bingwa,’
linaloratibiwa na Airtel Tanzania na Man United.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal
Malinzi akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Michezo nchini Leonard Thadeo ambaye alimwakilisha Waziri wa michezo akizungumza katika hafla ya kuzindua shindano la ‘Airtel Mimi ni Bingwa,’
linaloratibiwa na Airtel Tanzania na Man United.
Mkurugenzi wa Michezo,Leonard Thadeo, akipokea jezi halisi ya Manchester United kutoka kwa Mkuregenzi Mtendaji wa Airtel, Sunil Colaso.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Jamal malinzi akipokea jezi ya Manchester United.
Mkuregenzi Mtendaji wa Airtel, Sunil Colaso akimkabidhi Kibonde jezi ya Manchester United.
DAR ES SALAAM, Tanzania
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi,
ameikaribisha nchini klabu ya Manchester United ya Uingereza kwa ajili ya kambi
za maandalizi ya msimu, akiamini kuwa ujio wao utaamsha morali ya soka kwa
vijana na kukuza pato taifa kupitia utalii.
Malinzi alitoa ombi hilo la mwaliko leo jijini Dar es
Salaam, kwa Meneja Mahusiano wa Man United, Michael Higham, aliyekuwa
mwakilishi wa klabu hiyo katika hafla ya kuzindua shindano la ‘Airtel Mimi ni Bingwa,’
linaloratibiwa na Airtel Tanzania na Man United.
‘Airtel Mimi ni Bingwa’ ilizinduliwa jana na Mkurugenzi wa
Michezo nchini Leonard Thadeo, ambapo watumiaji wa Airtel Tanzania watashindana
kuwania tiketi mbili za kwenda Old Trafford kutazama mechi za Ligi Kuu, pamoja
na pesa taslimu kila siku.
Malinzi aliyeingia madarakani hivi karibu baada ya kushinda
uchaguzi mkuu wa TFF, alisema kuwa wao kama shirikisho, wanayo furaha kuwaalika
Man United nchini, akiamini watafurahia mandhari ya nchi yetu na kuchangia
ukuaji wa soka la vijana.
“Fikisha salamu zetu kwa uongozi wa Man United, waambie wana
mashabiki wengi Tanzania. Hawatojutia ujio wao, kwani utawawezesha kufurahia
mandhari ya nchi yetu kwa kutembelea vivutio vya utalii, mbuga za wanyama na
Mlima Kilimanjaro,” alisisitiza Malinzi.
Aliongeza kuwa, visiwa kama vya Zanzibar ni sehemu ambayo
anaamini itawavutia mno wachezaji na viongozi wa Man United na kwamba ujio wao
utakuwa chachu ya vijana kupenda soka na kuiwezesha serikali yetu pia kukuza
pato la taifa kupitia utalii.
Ili kujiunga katika shindano la ‘Airtel Mimi ni Bingwa,’
mtumiaji wa mtandao huo wa simu za mkononi anapaswa kuandika ujumbe mfupi wa
maneno (sms) yenye neno BINGWA, kisha kutuma kwenda namba 15656, kisha kujibu
maswali yanayompa pointi.
No comments:
Post a Comment