Search This Blog

Monday, September 9, 2013

MAKALA: WACHEZAJI WA BONGO MSIIGE UNYOAJI WA KIDUKU TU WA RONALDO/ BECKHAM - IGENI NA MBINU ZAO ZA KIBIASHARA HASA KWENYE HAKI ZA TASWIRA ZENU

  
Gareth Bale shirts for sale in Madrid
Thamani ya haki ya taswira/sura na hadhi ya mchezaji imefikia viwango vikubwa ikilinganishwa na enzi zile kabla ya dereva wa magari ya mbio za magari ya Langalanga Eddie Irvine kujinyakulia pauni 25,000 kutoka kituo cha Redio moja iliyotumia picha yake kutangazia biashara bila idhini yake mnamo mwaka 1999.

Enzi hizo picha za wanamichezo maarufu zilionekana kama mali ya umma.
Lakini michezo ilipozidi kua maarufu kote duniani, umuhimu wa hati miliki za michezo na wachezaji wake kama chombo cha kuuzia bidhaa na wahusika wenyewe kunufaika na taaluma yao.
Nyota wa michezo kama David Beckham, Cristiano Ronaldo, na sasa Gareth Bale wote wamefaidi mapato makubwa yanayoweza kupatikana kupitia masoko ya kuuza bidhaa kama chupi na viatu.

"Wanamichezo wamegundua uwezekano walio nao wa kufaidi kupitia haki zao, anasema Nigel Currie wa kampuni ya mauzo ya vifaa vya michezo Brand Rapport.

"Haki za taswira zinaweza kuwa kitu chochote ambacho kinaweza kuhusiana moja kwa moja na mtu binafsi.
"Kitu cha kawaida kabisa ni jina. Ikiwa jina lako ni Gareth Bale, na lipo kwenye jezi ya soka, then unakuwa na haki kupitia jezi ile."
 Bale, 24, amejiunga na Real Madrid hivi karibuni kwa ada ya uhamisho wa £85, anatarajia kutengeneza mamilioni ya fedha kupitia haki za taswira yake, ingawa amewapa 50% ya haki hizi klabuyake ya Real Madrid.
Cristiano Ronaldo playing for Real Madrid  
                       Viatu vya Cristiano Ronaldo vyenye nembo yake ya CR7
 
Madrid wanatambua wazi kwamba mapato watakayoyapata katika shea yao ya haki za taswira zitaisadia katika kupambana na deni la £507m.
Bale pia tayari ameshaisajili nembo ya ushangiliaji wa goli ya alama ya "Eleven of Hearts" katika haki zake za taswira kama ambavyo Cristiano Ronaldo alivyofanya na nembo ya CR7.


DAVID BECKHAM - footwork Production
Inawezekana mfano mzuri katika kuonyesha namna unavyoweza kutumia haki za taswira yako hata baada ya kustaafu - ni David Beckham.
Aliunda kampuni ya Footwork Productions firm ambayo hudili na haki zote za taswira yake mpaka hakimiliki za nembo zake za kibishara.
"Ilikuwa hatua nzuri sana ya kibishara," anasema mchambuzi wa masuala ya kiuchumi Mr Brown. "Ametumia na kuikuza vizuri thamani ya haki za taswira yake, na ushahdi unaonekana kutoka na namba za mapato yake."
xxx 
  David Beckham ataendelea kuvuna fedha nyingi kutokana na taswira yake pamoja na kustaafu.
 
Kwa mfano, wakati akiwa na ukubwa wa maarufu ule alipokuwa Madrid, akaunti za Footwork Productions - zinaripotiwa kuingiza faida ya £15.5m.
Tangu wakati ameendelea kuongeza umaarufu wake duniani kote akijiunga na vilabu vingine vya   LA Galaxy, AC Milan na Paris St-Germain.
"Uhamisho wake wa mwisho wa kujiunga na PSG - ambapo alicheza kuchukua mshahara na kuamua kuupeleka wote kwenye kusaidia jamii, lakini pia alifaidika kwa kiasi kikubwa katika mapato yaliyotokana na kuuzwa kwa bidhaa zilizokuwa na jina lake." anasema Mr Currie Brand Rapport..

WACHEZAJI WA KITANZANIA MNATAMBUA HAKI ZENU? MNAZITUMIA?

Nchini Tanzania soka ni mchezo wenye ufuasi mkubwa sana kuliko mchezo wowote ule. Kwa bahati mbaya mfumo mzima wa soka la kitanzania haujakaa sawa, hasa upande wa kibiashara. Timu nyingi na wachezaji wameshindwa kutumia fursa zinazokuja pamoja na mchezo huu katika kujitengenezea kipato cha ziada kupitia mchezo huo.

Vilabu vikubwa vikubwa vyenye ufuasi wa mamilioni ya washabiki Simba na Yanga vimeshindwa kutumia fursa ya kuuza bidhaa zenye nembo za timu hizo, jambo ambalo linavikosesha mapato makubwa na kushindwa kuzidi kusonga mbele na kujiendesha bila kutegemea udhamini wa mtu mmoja mmoja au makampuni.

Azam FC wamejaribu kuuza jezi zake rasmi katika kipindi kifupi tu walichokuwepo kwenye ramani ya soka.

Upande wa wachezaji inabidi wazitambue haki zao na wajue namna ya kufaidika nazo. Mikataba wanayoingia na vilabu ieleze wazi watafaidika vipi na matumzi ya haki za taswira zao kwa mfano jezi? 

Kama huna uelewa mkubwa wa haya mabo ni vzuri mkawa na mawakala wasomi kama akina Jorge Mendes ambao watakuwa wanawasaidia katika kufanya majadiliano na vilabu katika kuhusu mikataba yenu na namna mtakavyofaidika na mapato mengine tofauti na mishahara mitupu ambayo bado ni midogo. 

Acheni kuiga style tu ya uchezaji na unyoaji wa nywele za mastaa wa ulaya - igeni pia mbinu zao za kibiashara zinazowafanya waingize fedha nyingi kupitia mchezo huu wa soka. MSIRIDHIKE NA KIDOGO MKIPATACHO TUMIENI FURSA.

1 comment:

  1. Safi sana,niliona makala kama hii bbc,lakin umeifanya iwe relevant kwa mazingira ya soka letu,hiyo ndiyo tofauti ya mwandishi na mchambuzi.big up

    ReplyDelete