Search This Blog

Monday, September 9, 2013

TAARIFA: SAMUEL ETO'O ASTAAFU SOKA LA KIMATAIFA - KOCHA WAKE ASHINDWA KUTHIBITISHA KAMA KWELI AU HAPANA

Cameroon striker Samuel Eto'o (R) celebrates with midfielder Eyong EnohKocha mkuu wa Cameroon Volke Finke amekataa kuthibitisha kwamba nahodha wa timu hiyo ya taifa Samuel Eto'o amestaafu kuichezea timu hiyo.
Mchezaji huyo mpya wa Chelsea ambaye ni mshindi wa mara nne wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, ameripotiwa kuwaambia wachezaji wenzake kwamba mechi ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Libya ndio ilikuwa ya mwisho kwake.
Ushindi dhidi ya Libya umewafanya 'Simba Wasioshindika' kufuzu kwenda kucheza play off kwa ajili ya kufuzu kucheza michuano ya kombe la dunia 2014.
"Samuel Eto'o ni mchezaji mzuri na ni vizuri ingekuwa yeye ambaye angezungumzia habari hizi. Yeyey ndio anaojua maamuzi yake," Finke alisema.

"Ameitumikia vizuri timu ya taifa na ndio maana ingekuwa vizuri angemzungumza mwenye kuhusiana na suala hili."
Eto'o, ambaye alijiunga na Chelsea kutoka klabu ya Anzhi Makhachkala mwezi uliopita, hakuhudhuria mkutano wa baada ya mechi kuthibitisha juu ya taarifa za kustaafu kwake.Lakini kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika vya mchezaji huyo ni kwamba Eto'o anataka kuweka umakini wake katika kukiendeleza kituo chake cha kufundishia soka.
Eto'o pia kwa sasa ndio analipa fedha matibabu yote ya kocha wa zamani wa timu hiyo ya taifa Jean Paul Akono, ambaye alipata kiharusi mapema mwaka huu.

No comments:

Post a Comment