Search This Blog
Monday, September 9, 2013
MAKALA: TIMU YA TAIFA YA UFARANSA, INATOKEA MLANGO, WALIOINGILIA.
Na Baraka Mbolembole
Ufaransa ilicheza mchezo wa tano mfululizo pasipo kufunga bao lolote. Japo ilimiliki mchezo kwa asilimia 71, wakapiga mashuti matano golini, na mashuti 22 yaliyokuwa ' off target', wakipata mipira 10 ya kona, ila wakajikuta wakibanwa na timu ya Taifa ya Georgia na kulazimishwa suluhu. Matokeo ambayo yanawafanya kuwa nyuma ya vinara wa kundi I, timu ya Taifa ya Hispania kwa tofauti ya pointi tatu, zikiwa zimesalia mechi mbili mbili kwa kila timu.
WANAHITAJI NINI ZAIDI.
“ Kama tunahitaji kupata ushindi ni lazima tubadilike” alisema nahodha wa kikosi cha ‘ Blues’, golikipa Hugo Lloris. Kumbuka kuwa nyakati bora zaidi za Ufaransa zilikuwa ni pale walipotwaa kombe la dunia, mbele ya mashabiki wapatao 75, 000, katika uwanja wa Stade de France. Chini ya kocha, Aimé Jacquet ambaye alitumia mfumo wa 4-5-1, na kuiteketeza Brazil iliyokuwa na safu ya mashambulizi kali ikiongozwa na , Bebeto , pamoja Ronaldo . Nahodha kiongozi alikuwa na Didier Deschamps, ambaye alikuwa akiwaongoza viungo wenzake wane, Emmanuel Petit, Christian Karembeu, Youri Djiorkaeff, na Zinezide Zidane, nyota wa mchezo wa fainali na michuano ya kombe la dunia mwaka 1998.
Ufaransa ilikuwa ngumu kufungika, na haikuwa timu kali katika ufungaji, mshambuliaji wao namba moja na ambaye alicheza dakika zote za michuano hiyo, Stephane Guivarch alimaliza michuano pasipo kuwa na bao lolote. Hakufunga. Katika mfumo wa 4-4-2, Brazil ilikuwa ni timu ya michuano, ilikuwa na safu bora ya kiungo yenye kuupendezesha mchezo wa soka, nahodha kiongozi Dunga katika uchezaji wake hakuwa na vionjo vingi, kama ilivyokuwa kwa Deschamps, lakini timu kubwa ni lazima zipate mafanikio zikiwa na ‘ mihimili’ isiyotikishika, na Dunga aliweza kuwa kiongozi ‘ shupavu’ wa kikosi cha kocha Mario Zagallo, aliwaongoza viungo wenzake, Sampaio, Rivarlo na Leonardo na kuifanya Brazil kuwa timu kali katika ufungaji muda wote wa michuano.
Cafu, upande wa ulinzi sehemu ya kulia, Roberto Carlos, katika upande wa kushoto walitawala nafasi zao kwa miaka zaidi ya kumi duniani na kuwa walinzi bora zaidi wa pembeni kuwahi kutokea nchini Brazil. Walishambulia kwa usahihi na walikaba kwa usahihi. Hivyo waliwapunguzia mashambulizi walinzi wao wa kati, Aldan, na Junior Baiano. Lakini mbele ya Ufaransa walikwama, walikutana na timu imara katika mbinu, na ufundi na wakati wao walikuwa wakitegemea zaidi vipaji vyao, na ufundi wa Zagallo. Wakaikuta Ufaransa ‘ iliyokamilika’ na ngumu kufungika, waliikuta Ufaransa iliyokuwa na safu imara ya ulinzi kuliko timu yoyote katika michuano, Fabien Barthez, kipa bora wa michuano, Lilian Thuram, Bixente Rizarazu, mlinzi bora zaidi wa kushoto kuwahi kutokea nchini Ufaransa, Marcel Dessaily , nahodha ‘ asiye na beji’ , na Frank Leboeuf, ambaye aliingia mahala kwa Laurent Blac aliyekuwa na adhabu. Mechi ikamalizika kwa Ufaransa kushinda 3-0 na kutwaa ubingwa kwa stahili ya aina yake. Ni fainali bora zaidi ya ndani ya uwanja katika kipindi cha miaka zaidi ya 30 iliyopita.
Lakini siku ya Ijumaa, hali ilikuwa ni tofauti kabisa, safu ya mashambulizi katika mfumo wa 4-4-2 ilikuwa ni dhaifu sana, iliishia kuwa na muendelezo mbaya wa ufungaji kwa kikosi hicho kilicho hatarini kukosa nafasi ya kufuzu kwa kombe la dunia, mwaka 1993, Ufaransa ilishindwa kufuzu kwa fainali za Marekani, na inaweza kuwa hivyo kwa mara nyingine safari hii katika fainali zitakazopigwa Marekani ya Kusini.
Kama watashindwa kuifunga Hispania itakuwa ni pigo kubwa kwa kocha, Deschamps ( mshindi wa kombe la dunia, 1998, na uefa euro, 2000 akiwa nahodha’. Ufaransa ya sasa inatafuta namna ya kujiweka sawa na kuisuka upya timu yao hasa baada ya kizazi chao cha dhahabu kufikia mwisho, mwaka 2006. Kizazi kile ambacho kilitwaa mataji yote makubwa duniani kuanzia 1998- 2003, walipotwaa mataji ya dunia, ulaya na lile la mabingwa wa mabara ambalo walitwaa mara mbili mfululizo.
Wakati wa mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia, 2006 dhidi ya Brazil, nchini Ujerumani, aliyekuwa kocha wa Ufaransa, Raymond Domminech aliwaita pembeni ‘ mafaza’ Zinedine Zidane, Patrick Vierra na Thuram na kuwaambia mbinu ambazo alikuwa anakwenda kuzitiumia mbele ya Brazli iliyokuwa na ‘wakali’ kama, Kaka’, Ze Roberto, Ronaldinho Gaucho, Emerson katika safu ya kiungo, huku ikiwa na Ronaldo, na Adriano katika safu ya mashambulizi. Akawambia wachezaji wake hao ‘washindi’ kuwa wajiandae kwenda kucheza mchezo wa kuzuia. Wote, wakamshangaa kocha wao. Wao walikuwa wakijiamini kuwa walikuwa bora kuliko Brazil kwa mambo mengi, walikuwa na safu imara ya ulinzi, na viungo washindi katikati ya uwanja, Claude Makelele, Zidane, Vieira, wakisaidiwa na chipukizi mwenye kipaji, Frank Ribery. Kwa nini waende kuzuia kwa sababu tu Brazil wanao Ronaldo, Adriano, Kaka’ na Gaucho?
Wakamwambia kocha wao kuwa wanahitaji kitu tofauti na mawazo aliyokuwa nayo kichwani kuhusu ubora wa Brazil. Ufaransa ilishinda kwa bao la Thierry Henry dakika 20 kabla ya mechi kumalizika, na kuwafanya Wabrazil waamini kuwa walifungwa mchezo ule kutokana na Carlos kujali kupandisha soksi yake kuliko kumtazama na kumzuia Henry ambaye aliunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Zidane. Ilikuwa ni mbinu ‘ mbadala’ baada ya kushindwa kupata bao, japo walikuwa wamemiliki mchezo kwa muda mwingi, Lucio, na Juan waliziba ‘ mianya yote ‘ ya Ufaransa ambalo walikuwa wakimpitishia Henry, Cafu na Carlos bado hawakuwa ‘ wabaya’ katika upande wa pembeni na ndipo Wafaransa walipoamua kuwaadhibu kwa mtindi wa Stade de France, kuifunga Brazil ngumu kufungika kwa kutumia mipira iliyokufa. Ufaransa ilifika hadi fainali, na kosa moja tu likawanyima taji la pili la dunia, mbele ya ‘ mafia’ wa Italia, pale Arrianz Arena, 2006.
Yote hayo bila shaka yanapita katika kichwa cha Deschamps ambaye naye ameifanya Ufaransa kuwa timu imara kiasi katika ulinzi na kiungo. Walimiliki mchezo kwa asilimia 71, siku ya ijumaa ya wiki iliyopita dhidi ya Gorgia, wakapiga mashuti 22 ‘ off target’, na mengine manne ‘ on target’, wakapata kona 10 lakini hakuna ambayo ilikuwa hatari, Karimu Benzema, na Oliver Giroud, na hata alipikuja kuingia mshambuliaji, Pierre Gignac bado wakaishia kumaliza mchezo wa tano mfululuzo pasipo kufunga bao lolote. Katika kiungo, Moussa Sissoko, Mathieu Valburogua, ambao walicheza kama viungo wa ulinzi, Ribery na kinda, Josou Guilavogui wakicheza kwa viungo wachezesha timu wakitokea pembeni, lakini wakati Fulani wakateswa na kiungo mwenye miaka 21, ambaye alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza akiiwakilisha, Georgia, Tornike Orkriashvili, ambaye alikuwa ‘ sharp’ na kuvuruga mipango yao mingi ya ufungaji.
Bacary Sagna, Patrice Evra, Laurent Koncienly, na Eric Abidal wapo imara katika kudhitibi mashambulizi na kupandisha timu. Wapo nyuma kwa tofauti ya pointi tatu nyuma ya vinara wa kundi I, kanda ya Ulaya, timu ya Taifa ya Hispania. Miaka mine iliyopita walipitia tundu la sindano, na huko ‘ Wakautumia mkono wa Thierry Henry’ kufuzu mbele ya Jamhuri ya Ireland. Lakini sasa wanahitaji kumkumbusha kocha wao, Deschamps kutumia mbinu kama za mwaka 1998, na 2006 dhidi ya timu kali, mbinu ya kutumia mipira iliyokufa na ile ya krosi. Wakati wao wakihaha mbele ya Georgia, Brazil ambao walitwaa taji la mabara, Juni, mwaka huu wakicheza soka la kiwango cha juu walikuwa wakiitekeza timu ya Ausralia kwa mabao 6-0. JO, alifunga mara mbili, Neymar, Luiz Gustavo, Ramirez na Paulinho wakiwa wafungaji, ni unaitazama ni timu gani iliyoshinda. Maicon alichemsha Manchester City, mechi mbili akiwa na AS Roma zimemrejesha, haikuwa na Fred. Ufaransa watatokea katika mlango waliongilia na chini ya Deschamps. Mbinu bora zaidi zitawapeleka Brazil, mwakani.
O714 08 43 08
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment