Jose Mourinho alikaririwa mara kwa mara akisisitiza kwamba Romelu Lukaku alikuwa na jukumu kubwa ndani ya Chelsea na hatotolewa kwa mkopo tena. Lukaku alicheza katika mechi kadhaa za pre-season na ilionekana kwamba anastahili mno kupewa nafasi, akifunga mabao na akiwasumbua mno mabeki wa timu pinzani. Pamoja na kung'ara huku Demba Ba
amebaki Chelsea na Romelu Lukaku ametolewa kwa mkopo kwenda Everton. Je huu ulikuwa ni uamuzi mzuri kwa Chelsea?
Ni muhimu kuona kwamba Lukaku alianza kwenye michezo 20 tu katika 35 aliyocheza, jambo ambalo linafanya mabao yake 17 aliyofunga kuwa na wastani mzuri zaidi. Kama tunavyoona hapo juu Lukaku alikuwa bora zaidi kwenye lango la adui msimu uliopita kuliko aidha Fernando Torres au Demba Ba.
Katika Premier League ni vizuri kujua kwamba Fernando Torres alifunga mabao 8 tu msimu uliopita, huku goli moja tu akifunga ndani ya mwaka 2013. Rekodi yake kwenye ligi ya nyumbani na Chelsea ni mbaya sana akifunga mabao 15 tu katika mechi 84 za premier league. Ni kesi ambayo inaonyesha kwamba Lukaku amefunga mabao mengi kumzidi Torres katika michezo 35 tu zaidi ya Torres aliyecheza katika michezo 84.
Demba Ba pia nae alikuwa hana kiwango cha kuvutia sana ndani ya Chelsea. Ba alifunga mabao mawili tu ya ligi tangu alipojiunga na The Blues huku akionekana kutokuwa fiti na katika kiwango kibovu. Umwamba wake wa nguvu haupo kama tulivyotegemea huku akiwa hana ubora mzuri katika kukaa na mpira pamoja na wastani mdogo wa kucheza mipira ya vichwa.
.
Kwanini ametolewa kwa mkopo?
Hakuna ubishi kwamba Lukaku alikuwa bora sana katika washambuliaji wa Chelsea msimu uliopita, jambo ambalo linafanya uamuzi wa kumtoa kwa mkopo usiwe na tija. Chelsea ingeweza kumto kwa mkopo Demba Ba, ambaye tayari alishaonekana kuwa ni kitu cha ziada katika mahitaji. Chelsea haikuweza kuanza msimu ikiwa na washambuliaji wa wanne wakigombea nafasi ya kucheza katika nafasi moja na hivyo ikaamuliwa kwamba Lukaku angetolewa kwa mkopo ili aweze kucheza mara kwa mara katika msimu unaoenda kwenye michuano ya kombe la dunia.
Kuwasili kwa Eto’o pia inaweza ikawa sababu. Mkataba wa mwaka mmoja ndio alionao Etoo na kwa maana mcameroon anaweza asiwepo Stamford Bridge msimu ujao na suluhisho la muda katika matatizo ya safu ya ushambuliaji kabla ya Lukaku hajarudi kutoka Everton. Kuna hisia kwamba Lukaku hajakomaa vizuri na hivyo msimu mwingine wa mkopo utamsaidia kujiendeleza vizuri zaidi.
Hitimisho
Huku mpira wa kiufundi ambao Roberto Martinez anajaribu kuuleta Everton inaweza klabu nzuri sana kwa Lukaku kujiendeleza katika kuwa na ufundi mzuri dimbani. Lakini pia kumtoa kwa mkopo mchezaji ambaye alifunga mara nyingi kuliko washambuliaji wote wa Chelsea ukiwachanganya bado uamuzi huo unaonekana umekaa visivyo. Demba Ba ni mtu ambaye bado anasisitiza ndio alipaswa kuondoka - anaonekana hatokuwa na msaada mkubwa kwenye timu, wakati Fernando Torres siku zote huwa anatishia kwamba anarudi kwenye fomu, lakini anakosa consistency. Mategemeo makubwa yapo kwa Samuel Eto'o ambaye ana rekodi nzuri za ufungaji wa mabao lakini sasa akiwa na miaka 32 inawezekana ubora wake utakuwa umeshuka kidogo. Hivyo Chelsea wanaweza mwishoni wakajutia kumtoa kwa mkopo mshambuliaji Romeru Lukaku.
No comments:
Post a Comment