Marouane Fellaini alilazimika kumsaidia kocha wake David Moyes kuepukana na aibu ya kushindwa kumsajili mchezaji yoyote katika siku ya mwisho ya usajili katika klabu ya Manchester United kwa kukubali kupoteza kiasi cha £4 million za bonasi kutoka Everton ili aweze kukamilisha uhamisho wake wa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu ya England.
Mamuzi ya Everton kukataa kumuuza Baines na Real Madrid pia kusitisha usajili wa mkopo wa Fabio Coentrao dakika ya mwisho, baada ya kukwama kwa usajili wao wa beki wa kushoto wa Granada Guilherme Siqueira, ulimfanya David Moyes kukosa mbadala wa Patrice Evra katika nafasi ya beki wa kushoto.
Huku Everton wakihitaji kiasi cha £27.5million na Moyes
akiwa hayupo tayari kulipa kiasi cha fedha zaidi ya £23.5million kwa ajili ya Fellaini ambacho kilikuwa ndio kivunjia mkataba, kipengele ambacho kilikwisha muda wake mnamo July 31 - na Fellaini alikuwa anapaswa kulipwa kiasi cha £4million za bonasi - lakini ili aweze kukamilisha uhamsiho wake ikabidi kiungo huyo akubali kuzikosa fedha hizo kwa kupeleka maombi ya kuuzwa kabla ya saa 2 usiku, na kuhakikisha kwamba Everton hawaolazimika kumlipa £4million za bonasi - hivyo kurahisisha vilabu viwili kufikia makubaliano ya dili lenye thamani ya £27.5million..
No comments:
Post a Comment