Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa iliyouvunja rekodi inayokadiriwa kufikia kiasi cha 50
million Euros. Kiungo huyu mchezeshaji bila mashaka ni mmoja wachezaji wenye viwango vya juu zaidi duniani na watu wengi wameshangazwa na klabu ya Real Madrid kumruhusu aondoke kwenye klabu hiyo. Hivyo Je usajili wa wa Ozil unatoa picha kwa gani kwa Arsenal katika mbio za kushinda ubingwa wao wa kwanza ndani ya kipindi cha miaka nane?
Kitu gani Ozil atakileta ndani ya Arsenal?
Mesut Ozil ataleta kiasi kikubwa za ubunifu mkubwa katika kikosi cha Arsenal. Tangu ajiunge na Real Madrid Ozil aliweka rekodi ya kutoa assists 47 assists akiungana na Lionel Messi kuwa wachezaji waliotoa pasi nyingi zilizoaa magoli katika kipindi cha miaka mitatu. Ozil pia alitengeneza nafasi 92 za mabao kwa timu yake kwenye La Liga, namba ya pili kwa ukubwa akimfuatia Andres Iniesta. Mjerumani huyo pia alifunga mabao 9 katika michezo 31 aliyocheza msimu uliopita - akianza kwenye mechi 23.
Umuhimu wa hili ni kwamba pamoja kwamba Arsenal wana sifa nzuri ya ku jua kushambulia na kutengeneza nafasi lakini walihangaika sana msimu uliopita walipokutana na timu zenye ukuta mgumu, hasa kwenye mechi za ugenini. Msimu uliopita Arsenal walishindwa kufunga katika 21.4% ya mechi zao, namba kubwa zaidi ya idadi ya mechi bila kufunga kutoka mwaka 2009-2013. Kwa kifupi katika msimu wa 2011-12 klabu ilishindwa kufunga katika 13.2% ya mechi zao, hii ilionyesha wazi kuporomoka kwa klabu katika sekta ya utengenezaji wa mabao kadri siku zinavyokwenda.
Pia kwa kuongezea hapo Arsenal haikuwa timu iliyokuwa ikifanya uharibifu mkubwa kwenye magoli ya wapinzani wake kama walivyokuwa zamani. Kutoka 09-12 Arsenal ilifunga wastani wa mabao 2.5 kwa zaidi ya 60% ya mechi zao katika misimu mitatu mfululizo, lakini msimu uliopita walipata idadi ya mabao 2.5+ katika 46.4% ya mechi zao.
Hii inaonyesha Arsenal hawatishi kwenye lango la wapinzani kama walivyokuwa huku nyuma. Ozil sasa, na uwezo wake mkubwa katika kutengeneza nafasi na kutumia nafasi, anaweza kuwa msaada mkubwa katika kuisadia Arsenal kufunga hasa katika mechi ngumu, pia kusaidia timu kuzimaliza timu ambazo mara zimekuwa zikionea Arsenal.
Je Ozil ni mchezaji sahihi wanayemhitaji kwenye kikosi cha?
Jibu ni ndio au hapana. Kama tulivyoona hapo juu Arsenal hawakuwa na makali sana msimu uliopita. Ozil anaweza kusaidia zaidi katika kuiongezea ubora timu hasa kwenye kushambulia. Wasiwasi ni kwamba Arsenal inaweza ikafunguka zaidi ikiwa Santi Cazorla na Ozil
watacheza katika kikosi kimoja - hivi ndivo inavyoonesha katika set up ya kiufundi ya Wenger hivi sasa.
Pia kuna hisia kwamba pamoja na kuwa mchezaji mzuri na usajili mzuri - Ozil anaongeza upungufu fulani katika kikosi cha sasa Arsenal.
Arsenal na
Arsene Wenger na sera yao ya usajili inazua maswali ukifikiria klabu ilikuwa ikimtaka Wayne Rooney, Gonzalo Higuain na Luis Suarez, wote kama vipaumbele vya kwanza kabisa, lakini bado wakashindwa kupata saini ya hawa wote. Kwa kifupi kwenye idara ya ushambuliaji kuna tatizo kubwa ambao halijapatiwa ufumbuzi kwa maana kwamba Nicklas Bendtner anabaki Emirates, pamoja na kuwa hahitajiki.
Klabu pia iliishia kumtaka mshambuliaji wa Chelsea Demba Ba katika jaribio la mwisho ili kuongeza ufanisi katika ushambuliaji. Lakini mpaka sasa tatizo hilo halijapatiwa ufumbuzi na wakati Olivier Giroud kwenye fomu, lakini ni vizuri kugundua kwamba hajafunga bao lolote katika EPL nje mji wa London tangu ajiunge na Arsenal - jambo la kutia shaka kidogo.
Klabu imefanya jambo la msingi katika kumsajili kipa Emiliano
Viviano, ukizingatia matatizo na kutokueleweka kwa kiwango cha Wojciech
Szczęsny. Lakini klabu haijafanya uimarishaji wa kikosi vizuri ukizingatia imewatoa wachezaji 8 kwa mkopo na kuwauza kwenye dirisha hili la usajili - wakiwemo walinzi watatu ambao wanacheza kwenye eneo ambalo Arsenal ndio wana udhaifu mkubwa na walitaka kuliimarisha lakini hawakuweza. Arsenal itaanza msimu mpya na mabeki watatu tu wa kati wa kikosi cha kwanza lakini ukifikiria namna Thomas Vermaelen alivyokuwa akifanya makosa msimu uliopita, inaonekana kutakuwa na tatizo kubwa kwenye eneo hilo. Majeruhi kwa beki yoyote kati ya hao kutaiweka Arsenal katika presha kubwa na hivyo wanaweza wasifanye vizuri.
Hitimisho
Usajili wa Ozil bila shaka ni mzuri mno lakini hautaisadia Arsenal kushinda taji, ukiangalia ukweli kwamba bado kuna mapungufu makubwa kwenye kikosi. Mbio za kugombea nafasi ya nne - ambazo zinaweza zikahusisha timu kama Liverpool, Arsenal na Spurs zitakuwa moto sana, ukizingatia fedha zilizotumiwa na hivi vilabu katika kugombea nafasi ya kwenda kucheza ligi ya mabingwa wa ulaya..
Matatizo makubwa ya Arsenal msimu huu bado yatabaki kwenye ukuta, kwa sababu ya uchache wa wachezaji kwenye eneo hilo, lakini pia bado haijafahamika uzuri na udhaifu wa kipa mpya Viviano - kama ataweza kuziba makosa aliyokuwa akifanya Szczesny.
Usajili wa Ozil ni kitu kikubwa kwa hadhi ya Arsenal na hata kibiashara - kitu ambacho baadhi ya watu wanaamini ni muhimu kuliko kitu atakachokileta mchezaji mwenyewe uwanjani - kwa maana ya kuirudishia sifa klabu kwamba ni timu yenye hamu ya kufanikiwa, kutumia fedha na sio kuingiza tu kwa kuuza wachezaji wao.
Una ushauri mzuri ila wape mda uwaone kama hawatafanya vizuri au la kuwahukumu kabla hawajaanza utakuwa unafanya makosa makubwa sn bila ya kujua maana hata hao ulio waona ktk msimu ulio pita wengine walikuwa ni wageni wa ligi ya uingereza na huwezi kuwafananisha na rvp alie cheza ligi ya uingeleza kwa miaka 8 akiwa na arsenala na umajeruhi wake.jambo la msingi ktk soka ni mda kuna walio tumia fedha na hawakuchuka kombe na hao wasemeje na kuna ambao hawakusajili ila wako ktk timu kwa mda mrefu pamoja na wakachukua ubingwa nahao je wasemeje.kila jambo lipe mda utaona matunda yake
ReplyDelete