Search This Blog

Friday, September 27, 2013

HATIMAYE LEWANDOWSKI KUSAINI BAYERN MUNICH MWEZI JANUARY - MWENYEWE ATHIBITISHA


Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Robert Lewandowski amethibitisha rasmi kwamba atasaini mkataba wa kwanza wa makubaliano wa kujiunga na Bayern Munich katika soko la usajili la mwezi wa  January kisha kujiunga na mabavaria mara tu mkataba wake utakapoisha mwishoni mwa msimu huu.


Baada ya tetesi za muda mrefu kuhusu mshambuliaji huyu wa kipoland, hatimaye hivi sasa ipo wazi Pep Guardiola atamuongeza mshambuliaji katika kikosi chake  2014.

Kwa mara ya kwanza mchezaji amekiri kwamba atajiunga na Bayern mwishoni mwa msimu wakati alipokuwa akihojiwa na Sport 1, alisema: ‘Ndio, nathibithisha nitahamia Bayern kwa sababu sasa hivi nikasaini mkataba wa makubaliano.’

No comments:

Post a Comment