Search This Blog

Monday, August 26, 2013

MAN UNITED VS CHELSEA: THE BLUES NDIO TIMU PEKEE INAYOONGOZA KUCHUKUA POINTI NYINGI KUTOKA UNITED PREMIER LEAGUE

Fix? Can David Moyes overturn Manchester United's Premier League slump against Chelsea?
David Moyes atauweza mfupa uliomshinda Sir Alex Ferguson

Wakati David Moyes akielekea kwenye mchezo wa leo jumatatu dhidi ya kikosi cha Jose Mourinho cha Chelsea, historia inaonyesha kwamba kocha huyo mpya wa United anakutana na timu ambayo imekuwa ikiionea United sana United katika premier league.  

Katika mechi yake ya kwanza ya kimashindano ndani ya uwanja wa Old Trafford, Moyes ataangalia timu yake ikipambana na klabu ambayo imechukua pointi nyingi sana kwao kuliko klabu yoyote tangu ulipoanzishwa mfumo wa Premier League.

Kipigo cha 1-0 walichopokea nyumbani dhidi ya Chelsea mwezi May - wakati ambao kikosi cha Sir Alex Ferguson kikiwa tayari kimeweka ubingwa kibindoni ubingwa wa 13 wa Premier League - pia kinamaanisha Chelsea ndio timu pekee ambayo imepata ushindi mara nyingi dhidi ya United kuliko timu yoyote tangu mfumo wa Premier league uanze mnamo 1992.


Hata kabla ya kuibuka kwa klabu hiyo ya magharibi mwa london na nguvu ya utajiri wa Roman Abramovich na kuja kwa Mourinho, Chelsea tayari walishajijengea utawala dhidi ya United. 

Vikosi bora kabisa vya Unuted chini ya gwiji Sir Alex Ferguson' viliteleza mbele Chelsea, huku kikosi cha 1993/94 - kilichowahusisha Schmeichel, Bruce, Pallister, Keane, Ince na Cantona - kikipokea kipigo cha 1-0 nyumbani na ugenini dhidi ya Chelsea ambayo ilimaliza ligi ikishika nafasi ya 14.

Kikosi cha United kilichoshinda makombe matatu 1998/99 pia kilishindwa kuwafunga Chelsea katika Premier League, wakitoa suluhu nyumbani na ugenini, kabla ya kuja kufungwa 5-0 katika dimba la Stamford Bridge na timu iliyokuwa ikiongozwa na  Gianluca Vialli - magoli ya Gus Poyet, Chris Sutton na Jody Morris - miezi mitano baada ya United kuifunga Bayern Munich katika Champions League final.

Wakati mwingine mgumu kwa Ferguson ulikuja dhidi ya Chelsea mwaka 2001. Kocha huyu wa zamani wa United alitangaza makusudio yake ya kutaka kustaafu mwishoni mwa msimu wa  2001/02 na timu yake ikaingia kwenye ligi ikiwa katika hali mbaya - wakapigwa 3-0 nyumabani dhidi ya kikosi cha Claudio Ranieri - wakashuka mpaka kushika nafasi ya 7 baada ya vipigo vitano mpaka kufikia December. Ferguson baadae, akabadili msimamo na kuambua kubaki Old Trafford kwa miaka mingine 11.

Mchezo wa kwanza wa Premier League wa Mourinho ulimkutanisha na United katika dimba la Stamford Bridge, na ushindi wa 1-0 kwa Chelsea ukaanzisha utawala dhidi ya mashetani wekundu kwa miaka miwili huko Chelsea ikichukua makombe mawili mfululizo - huku Mourinho akichukua ubingwa mikononi mwa United kwa kuitandika 3-0 mnamo April 2006.

Makocha wapya walikuja baada ya Mourinho lakini United bado walihangaika sana dhidi ya Chelsea, ingawa Ferguson alimtandika  2-0 Avram Grant katika mechi iliyopigwa Old Trafford, kipigo cha 3-0 katika mchezo wa mwisho wa Phil Scolari kwenye benchi la Chelsea January 2009 na ushindi wa 2-1 dhidi ya The Blues ukawapa United ubingwa wa 19 wa Premier League mwezi May 2011.

Ferguson pia aliweza kubeba vikombe mbele ya Chelsea, akishinda kombe la 1994 FA Cup na Champions League jijini Moscow mwaka 2008 - ingawa Mourinho aliweza kuifunga United katika fainali yake ya kwanza ya FA Cup kwenye dimba la Wembley mwaka 2007.

Cha kushangaza zaidi, United haikuwahi kuifunga Chelsea nyumbani na ugenini katika zama za Premier league Chelsea na Sir Alex Ferguson mara moja tu alifanikiwa kuifunga klabu hiyo ya London nyumbani na ungenini katika wakati wote aliofanya kazi Old Trafford.

Mwanga wa mafanikio kwa David Moyes unaweza kuwaka kutokana na ukweli kwamba mscotland mwenzie Ferguson aliweza kuifunga Chelsea nyumbani na ugenini kaika msimu wake wa kwanza kwenye klabu hiyo 1987-88.

Katika Premier League, imekuwa ni Chelsea juu ya United, kiwastani, United imekusanya pointi chache kutoka kwa Chelsea ikiwa na wastani wa kushinda wa 30.95% ambao ni wa chini kwao ukilinganisha na mechi zao na timu nyingine za juu.   


Chelsea ilikuwa ndio timu ya mwisho kumfunga Sir Alex Ferguson katika mashindano manne tofauti - kipigo cha 1-0 ndani ya Old Trafford katika Premier League mwezi May, kipigo kingine cha 1-0 katika raundi ya 6 ya FA Cup mwezi March, kipigo cha 5-4 katika kombe la Capital One mwezi October 2012 na Chelsea ilikuwa ndio timu ya mwisho kuifunga United katika ngao ya hisani - kwa penati mnamo mwaka 2009.

Kuelekea mchezo leo, United imeweza kumfunga Jose Mourinho mara mbili tu katika mechi 16 - dhidi ya Chelsea mwaka 2005 na dhidi ya Inter Milan 2009 - matokeo ambayo yalimfanya Sir Alex Ferguson kukiri mwezi March mwaka huu kwamba hata yeye hakuweza kushindana na Mourinho katika mind games.


Rekodi ya Moyes dhidi ya Mourinho ndio mbaya kabisa, akifunga mechi 4 kati ya 6 ambazo timu yake ya Everton ilikutana na Chelsea katika ligi - akishinda kupata ushindi kabisa.

Ikiwa Chelsea itashinda mechi ya leo pale Oild Trafford then watakuwa wameipita United na City pointi 6, Moyes atakuwa akiomba kupata ushindi wa kwanza katika mechi yake ya kwanza ya kimashindano Theatre of Dreams dhidi ya timu ambayo ilimshinda aliyemrithi Sir AleX Ferguson.

No comments:

Post a Comment