Search This Blog

Monday, August 26, 2013

MAKALA: KIBADENI, UMRI MKUBWA, NA MZIGO MZITO KICHWANI.


Na Baraka Mbolembole

Kuelekea katika kikomo cha mechi za ligi kuu msimu uliopita, vyombo mbalimbali vya habari nchini vilikuwa vikiripoti habari kuwa klabu ya Simba ilikuwa mbioni kuvunja mahusiano yake ya kikazi na kocha Patrick Liewig. Kocha huyo raia wa Ufaransa alioneshwa mlango wa kutokea mara baada ya Simba kupoteza mchezo wake wa mwisho, Mei 18 dhidi ya mahasimu wao Yanga. Siku 11 baadae, Abdallah ' King' Kibadeni alisaini kandarasi ya miaka miwili kufanya kazi na timu hiyo. Anatazamwa na kuchukuliwa kama ' Mkombozi wa ardhi ya Mtaa wa Msimbazi'. Amepewa kazi hiyo hili kupanga kikosi katika usawa. Kazi ambayo ilimshinda mtangulizi wake ambaye alikaa kwa muda husiozidi miezi mitano klabuni hapo.


 ' Taifa Kubwa', ndivyo jina la utani la Simba linavyotamkwa. Kuwasili kwa Kibadeni, ni wazi kuwa timu ya Simba itabadilisha mfumo wake wa kiuchezaji, lugha na hata kimpira. King, mwenye umri wa miaka kwa sasa, ni ' Mchezaji wa Wachezaji', ni mtu ambaye ana mafanikio makubwa katika uchezaji na ufundishaji hadi kufikia kulinganishwa na mfalme. Ni mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo ambaye ameweka rekodi kubwa kipindi cha uchezaji wake.

Mkataba kati ya Kibadeni na mwajiri wake Simba, ni wa miaka miwili. Wakati, Simba ilipokuwa ikitumia muda mwingi kusaka makocha kutoka barani Ulaya na nchi jirani za Kiafrika kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita, Kibadeni alikuwa ni shujaa ambaye aliweza kuingoza timu ya Moro United kufika fainali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati, 2006 na kufungwa na timu ya Polisi ya Uganda, mbele ya Rais, Jakaya Mrisho Kikwete, baadae akaifundisha timu ya Manyema, na msimu uliopita akashinda tuzo ya kocha bora wa msimu akiwa anaifundisha timu ya Kagera Sugar. Kazi yake nzuri ndiyo iliyompatia tuzo na kuonekana kama mtu sahihi ambaye anaweza kuifanya Simba kuwa timu kali inayotwaa mataji. 


Simba mabingwa hao mara 18 wa ligi kuu, mabingwa mara sita wa michuano ya Kagame Cup.. Hakuna kitu kigeni katika soka, na bila shaka, King anajua na kufahamu mambo mengi kuhusu Simba. Hakuna kijana katika soka, kauli hii inawezekana isiyo na busara kwa mtazamo mwingine, lakini Kibadeni anatakiwa kufanya kazi na kundi kubwa la wachezaji vijana na kuhakikisha anafanya vizuri, vinginevyo mahusiano yake na mwajiri wake yatakwisha haraka. Kibadeni ni mtu anayependa kuweka vitu kama hivi katika hali ya urahisi na mara zote amekuwa rafiki wa wachezaji vijana nchini.

Katika michezo kadhaa ya kujipima nguvu kabla ya kuwakabili, Rhino Rangers wikiendi hii. King, ameonekana kulishughulikia tatizo la safu ya ulinzi ya timu hiyo ambayo imekuwa ikichangia ushindi kwa timu pinzani, ukitazama kuanzia mchezo dhidi ya SC Villa siku ya Tamasha la Simba Day, utakubaliana nami kuwa ubadilikaji wa walinzi wa timu hiyo mchezoni ulikuwa ni mzuri.

Simba ni ile ile, mafanikio ni yale yale, na King ni Yule Yule. King ni mtu anayeijua vizuri kazi yake na bila shaka ni mtu anayeweza kuipaisha Simba zaidi na zaidi kama atapewa muda wa kutosha, lakini timu kubwa kama Simba si rahisi kukuvumilia endapo matokeo yatakuwa ni mabaya uwanjani.

0714 08 43 08

2 comments:

  1. huo umri mbona haujatajwa aliokuwa nao

    ReplyDelete
  2. Hilo ni kweli ila tatizo litakua moja tu,kuvumilia ili apewe muda cdhani kama wanasimba wenzangu watakubali

    ReplyDelete