Wakati habari za kwamba Anzhi Makhachkala, klabu inayomilikiwa na billionea wa kirusi, ilikuwa inapunguza matumizi yake na pia imewaweka sokoni baadhi ya wachezaji, waandishi wa habari wengi - nikiwemo tulidhani ni habari za kizushi tu.
Bajeti ya klabu, ambayo ilikuwa ikifikia kiasi cha £116m kwa msimu (ya pili kwa ukubwa baada ya Zenit St Petersburg ya Russia), ilikuwa inapunguzwa kutoka £32m mwisho £45m.
Rene Meulensteen, msaidizi wa zamani wa Sir Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United ambaye alimrithi kazi Guus Hiddink, alifukuzwa kazi baada ya siku 16 tu. Na pia wachezaji wa kigeni na wakirusi pia, walionunuliwa kwa fedha nyingi katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, walikuwa wamewekwa sokoni.
Baadhi ya waandishi wa habari wamekuwa wakijaribu kuangalia sababu za kisoka kuhusu uamuzi wa Kerimov na zipo kadhaa.
Baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu msimu uliopita, matarajio yalikuwa makubwa - kuchukua ubingwa, lakini Anzhi tayari wameshaanza vibaya msimu mpya, wakifungwa mechi mbili na kutoa suluhu moja katika michezo yao minne ya kwanza.
Taarifa rasmi ya klabu ilisema vizuri zaidi kwamba "kwa kuzingatia matokeo ya klabu ya hivi karibuni, uamuzi umefikiwa kwamba inabidi kuundwa mpango wa muda mrefu kwa ajili ya maendeleo ya klabu".
Tetesi zinasema kwamba kulikuwepo na hali ya kutokuelewana miongoni mwa wachezaji ikiwa ni wiki mbili tu tangu Meulensteen alipopewa ukocha mkuu, kulikuwepo na ugomvi baina ya nahodha wa Urusi aliyesajiliwa hivi karibuni Igor Denisov na mshambuliaji mcameroon Samuel Eto'o, huku Meulensteen akiwa hajui amtetee nani kati ya hao jambo lilopelekea kuonekana hana mamlaka.
Pia kuna taarifa kwamba Eto'o hataki kufanya kazi na kocha wa zamani wa timu hiyo Gadzhi
Gadzhiev - na hili linaweza kutoa ishara kwamba mwisho wa Eto'o unakaribia kwa sababu Gadzhiev anatajwa kuwa ndio atakemrithi Meulensteen.
Lakini matukio ya kiufundi ni baadhi ya vitu ambavyo vinavyopelekea hatua hii mpya ya kuivuruga timu. Habari ambazo hazijathibitishwa ni kwamba masuala ya kibiashara ya tajiri Kerimov pia yanahusika.
Ingawa taarifa kwamba tajiri huyo mwenye miaka 47 ni mgonjwa sana zimekanushwa, jambo ambalo halina ubishi ni kwamba biashara zake haziendi vizuri kwasa. Wiki iliyopita ilitangazwa kwamba kampuni yake ya nishati ilivunja mkataba na kampuni nyingine ya Belarus wa dili ambalo ambalo linasemekana lingeweza kumuingizia Kerimov na wafanyabiashara wenzie kiasi cha paundi billioni 4 kupitia kampuni ya Uralkali.
Masaa kadhaa baada ya kutangazwa kwa kuvunjika kwa mkataba huo, kiasi cha paundi billioni 5.5 zilizondolewa kwenye akaunti ya kampuni ya Uralkali ya Kerimov na wenzie - huku mfanyabiashara huyo akipoteza kiasi kisichopungua £325m katika utajiri wake wote. Lakini baadae hali ya hisa za kampuni ikarudi sawa.
Wawakilishi wa Kerimov wanajaribu kwa kila hali kutohusisha mambo ya Anzhi na kwenda vibaya kwa mambo ya kampuni ya Uralkali - lakini mfuatano wa matukio haya uneeleza vinginevyo.
Raisi wa klabu hiyo Konstantin Remchukov amekaririwa akisisitiza kwamba Kerimov bado anaimiliki timu hiyo na ataendelea kuisadia kifedha. Na pia uamuzi wake wa kupunguza matumizi ya klabu hiyo umepokelewa vizuri na mashabiki wa timu hiyo.
"Akiwa tayari kashatumia kiasi cha £290m, hakuna cha zaidi Kerimov alichokifanya zaidi ya kuwatajirisha baadhi ya wachezaji wapenda fedha," Alisher Aminov, mmoja wa mjumbe wa bodi ya umoja wa vyama vya soka Urusi alisema.
Mashabiki pia nao walitoa maoni yao - huku mengi yakiunga mkono uamuzi wa tajiri huyo. "Wengi tulisubiri kwa jambo hili kufanyika kwamuda mrefu, haijalishi ni mchezaji gani yupo kwenye timu yetu kinacholeta maana ni ile tu kwamba amevaa jezi yetu na anaiwakilisha Anzhi' alisema Gubden ambaye ni shabiki wa timu hiyo..
Baada ya mabadiliko haya sasa inaaminika mpango wa Anzhi ni kugeukia vipaji vya nyumbani zaidi.
Na hatimaye wanaweza kurudi kwenye eneo lao la Dagestan; wachezaji sasa wanaishi na kufanya mazoezi jijini Moscow, halafu husafiri kwa maili 800 kwenye uwanja wa nyumbani wa Makhachkala kwa ajili ya michezo ya nyumbani.
`Na hata kwa bajeti ya kuanzia £32 mpaka £45m, wanaweza kuendelea kushindana kwenye ligi ya Urusi kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza kwenye UCL.
lakini matumizi ya kuweza kumridhisha Etoo kama mkataba wake unavyotaka hayatakuwepo tena. Hivyo siku za nahodha huyo wa Cameroon ndani ya uzi wa njano zinahesabika.
MANUNUZI YA BEI MBAYA YA ANZHI - UTAWALA LA KERIMOV
- £30m Willian from Shakhtar Donetsk
- £23.7m Samuel Eto'o from Inter
- £15.8m Lacina Traore from Kuban Krasnodar
- £13.2m Yuri Zhirkov from Chelsea
- £12.3m Christopher Samba from Blackburn
- £12.3m Balazs Dzsudzsak from PSV
- £8.8m Jucilei from Corinthians
- £7m Mbark Boussoufa from Anderlecht
MATUMIZI YA FEDHA YA VILABU VYA RUSSIA MSIMU ULIOPITA.
- Zenit St Petersburg (£184m)
- Anzhi (£116m)
- Rubin Kazan (£93.45m)
- Dinamo Moscow (£80.5m)
- Lokomotiv Moscow (£75m)
- Spartak Moscow (£67m)
- CSKA Moscow (£58m)
No comments:
Post a Comment