Hatimaye beki wa kimataifa wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Shomary Kapombe amefuzu majaribio aliyokuwa akifanya barani ulaya kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya AS Cannes ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mwandishi wa BBC - Abdul Mohamed ni kwamba Shomary Kapombe amefuzu majaribio hayo na sasa zimebakia taratibu tu za uhamisho ili ajiunge rasmi na timu hiyo ya AS Cannes inayoshiriki kwenye ligi daraja la nne nchini Ufaransa.
Kapombe aliondoka nchini takribani mwezi mmoja uliopita na kwenda barani ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Mtandao huu upo katika kujaribu kufanya mawasiliano na uongozi wa Simba ili kupata taarifa rasmi juu ya usajili huu wa Shomary Kapombe.
hongera sana kaka hata Nonda alipita huko huko uliko pita
ReplyDeleteUnataka kucheza ulaya? Nenda SSC ! Unataka uishie Ashanti ama Lipuli!! Cheza ndala Fc!!! Teh teh teh!!! Kama nawaona walivyofura kwa hasira!!!
ReplyDeletekapombe usiende kula cannes za pombe tu huko sababu we ni kapombe mpenda kakikombe ka pombe
DeleteHongera sana Kapombe, jitihada zako zitakufikisha mbali. Tunakuombea zaidi zaidi na udumishe juhudi na nidhamu..
ReplyDeleteKaza buti komaa, tunakuaminia kwa nidhamu na weledi iko siku tutakuskia umepanda kuchezea Lyon au Monaco. Haruna Mosi alipata bahati kama hii akaichezea, wewe usifanye hivyo.
ReplyDeleteHongera Kapombe pia nawaasa Yanga na vilabu vingine waruhusu wachezaji wao waende nje ilituwe na ma'pro' wa kutosha na kuisaidia timu ya taifa.
ReplyDeletembona watu hawajielewi anatoka premia anaenda kucheza mchangani ligi daraja ya nne huko ndo kupotea au anapenda kukaa na weupe
ReplyDeleteMtu akitaka kuendelea kulipwa 1m awe na akili kama zako hacha simba iboreshe maisha ya wachezaji. Salary zaidi ya $20,000 hata akichezi miaka miwili haoni ndani
Delete