Search This Blog

Monday, August 12, 2013

EXCLUSIVE: BAADA YA YANGA KUENDELEA KUGOMEA MKATABA WA AZAM TV - TENGA AINGILIA KATI - AOMBA MELEZO YA NAMNA AZAM TV WALIVYOPATA DILI LA KUONYESHA LIGI

Sakata la klabu ya Yanga kugomea kukubaliana na mkataba wa kati ya kamati ya Ligi na Azam Media wa kuipa haki za matangazo ya televisheni ya mechi za ligi kuu kituo cha Azam TV limechukua sura mpya baada ya Raisi wa shirikisho la soka la nchini TFF Leogdar Tenga  kuingilia kati.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi mtandao huu ulizozipata ni kwamba Tenga amewaandikia barua Yanga akiwaambia kwamba amepata malalamiko yao dhidi ya mkataba wa urushwaji wa matangazo ya mechi za ligi kupitia Azam TV.

Pia Tenga amewaambia Yanga kwamba ameiomba kamati ya ligi kumpatia maelezo namna mchakato mzima wa ugawaji wa tenda hiyo ulivyofanywa mpaka kufikia maamuzi ya kuingia makubaliano na Azam TV.

Tenga amewaomba Yanga kuwa wavumilivu ili kushughulikia malalamiko yao kuhakikisha muafaka unafikiwa kwa ajili ya manufaa ya soka la Tanzania.

6 comments:

  1. Waungwana humaliza tofauti zao kwa masikilizano. Kuliko kubezana kama watu wako sokoni.yawezekana yanga wakawa hawana hoja ya msingi. Lkn vilevile yawezekana wakawa na hoja ya msingi.tatizo lililopo katika viongozi wa juu wa soka hapa nchini ni ubabe. Wakiamua jambo lao hawataki kabisa masikilizano na upande wowote uliokinyume chao. Ndo maana leo nsmpongeza mh Tenga walau kwa kuwasikiliza yanga.

    ReplyDelete
  2. Tenga huo ndio Uongozi. Safi sana. Tenda haki. Mpaka leo hao Azam Tv hawajawah kurusha kipindi hata kimoja.

    ReplyDelete
  3. viongozi waache ujinga hao ndio washabiki wa yanga ndo maana soka rinaporomoka kila siku tatizo yanga majinga hawataki vilabu vidogo vipate udhamini wanataka wadominate mpoira wa kibongo huku hawana lolote uwanja hawana na uongozi hawana wanabisha hata point za msingi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Viongozi wenu ndio wajinga wanakata mauno huku wamufunga Swaum kisa cheque ya Milioni 100 mamburula nyie Milioni 100 kwa yanga ni pesa ya usajili wa Nyionzima tu Njaa zitawaua

      Delete
    2. kushambulia watu kwa lugha ya kejeli eti kwasababu hawaamini unachokiamini si uungwana..tofauti za mawazo haziondoi utu wa mtu..kusema 'yanga majinga...hawana lolote...na uongozi hawana' si uungwana. unaweza kujenga hoja yako ya msingi ukaeleweka bila kukejeli watu...

      Delete
    3. hivi inaingia akilini kiwa tenga kwa muda wote tangu azam wapewe haki alikiwa hajui mchakato umekwendaje? kama ndo hivyo basi jatuna raisi na soka letu ni halali lidumae. kweli muda wote na mambo yoote hadi kusainishana tenga hajajua azam alishinda vipi au ndo haya ya usimba na uyanga? tusilete siasa za kipuuzi kwenye
      mambo ya maendeleo bwana acha uanga wasuse wenye meno wale YANGA SI TUNA MANJI BWANA ATATOA MIJIHELA NA AKIKWAMA TUTATEMBEZA BAKURI NDO
      MAISHA TULIYOZOEA HAYO

      Delete