Kenya itakuwa nchi ya 100 ya kigeni kuwa na mchezaji anayekipiga kwenye ligi kuu ya England wakati kiungo wa kimataifa wa nchi hiyo Victor Wanyama atakapocheza mechi yake ya kwanza akiwa na Southampton.
Na yote haya yasingewezekana kama isingekuwa kwa mama wa watoto sita, ambaye ametumia maisha yake yote akifanya kazi ya mkuu wa kitengo cha michezo katika shule moja jijini Nairobi.
Wanyama, 22, alianza kufahamika vizuri kwenye ulimwengu wa kimataifa wa soka mwezi November mwaka jana wakati alipofunga goli katika mechi kati ya klabu yake ya zamani na FC Barcelona na kuisadia klabu hiyo ya Uskochi kushinda 2-1 katika mechi ya makundi ya Champions League.
Kiungo huyo mwenye kimo cha 6ft 2in anayecheza kiungo cha ulinzi alivivutia vilabu vya Manchester United, Arsenal na Everton miongoni mwa vingine vingi lakini hatimaye mwishoni alisaini kuichezea Southampton kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya klabu hiyo £12.5million wakati wa dirisha la usajili hili lilipofunguliwa.
Sehemu wanazotoka wachezaji wanaokipiga kwenye EPL |
Wachezaji kutoka Albania mpaka Zimbabwe na nchi zingine 98, ukiachana na mataifa manne yaliyomo ndani ya ya mipaka ya UK, yameshakuwa na wawakilishi katika misimu 21 tangu ulipoanzishwa rasmi mfumo wa Premier League mnamo 1992 - lakini Wanyama anakuwa mchezaji wa kwanza kuiwakilisha nchi yake ya Kenya.
Akiwa na miaka 22 sasa lakini tayari ameshachezea vilabu vya juu kwa maana ya professional clubs katika nchi tano tofauti, kuanzia AFC Leopards ya nyumbani kwao akiwa na miaka 15, akaenda Helsingborgs huko Sweden akiwa na miaka 16, Beerschot ya Belgium akiwa na miaka 17, Celtic ya Scotland akiwa na miaka 20 na sasa yupo Southampton.
Lakini bila uangalizi na kujitoa kwa mwalimu wa michezo Sophie Makoba, 48, ingekuwa vigumu kwa Wanyama kutambua na kukiendeleza kipaji chake.
Kwa msaada wake, Wanyama aliweza kujiendeleza na kuwa mtu muhimu katika nchi yenye wakazi 44 million kwa kuwa mkenya wa kwanza kucheza kwenye ligi kuu ya England.
'Premier League ni ligi bora na ndio inayofuatiliwa kwa kiasi kikubwa nchini Kenya na najua watapata mashabiki wengi sasa hivi wakiwa wamemsajili Victor,' alisema Makoba katika mahojiano na gazeti la Daily mail.
'Watu wa Kenya wana shauku kubwa ya msimu mpya wa EPL. Watu wengi wanaangalia mechi za EPL japo sio wote wanaoweza kuangalia kwenye TV zao kwa sababu ni gharama kubwa kulipia.'
Akiwa bado mdogo Wanyama alikuwa na bahati nzuri ya kujiunga na shule ya sekondari - Kamukunji High School, ambapo mwalimu amekuwa akifanya kazi. "Hakuwa na akili sana darasani lakini ndio mchezaji mzuri zaidi kiwanjani, aliweza kupata nafasi kwenye timu ya kwanza ya shule akiwa amezidiwa na wenzie umri wa miaka mitatu alipokuwa na miaka 13,' anaelezea mwalimu Makoba.
Makoba alikuwa mwanamichezo wa kweli, aliwahi kucheza michezo ya gymnastic akiwa mdogo na pia akajaribu kucheza netball na riadha kabla ya hajaenda kucheza basketball katika ngazi ya taifa.
Angeweza kuendelea na michezo lakini kwake elimu ilikuwa ni bora zaidi, na hivyo alipopata nafasi ya kusoma chuo akaamua kuachana na micheoz na kujiunga na chuo.
'Wakati nilipomaliza chuo mwaka 1990, nilikuwa nina miaka 25 na nikaamua kufanya kazi katika shule ya Kamukunji kama mkuu wa kitengo cha michezo shuleni. 'Niliona kwamba kuna wanafunzi ambao hawakuwa vizuri kimasomo darasani ambao wangeweza kupata mafanikio kupitia michezo na kuanzia hapo tukaanza kitu ambacho kimekuwa utamaduni wa kuendeleza michezo mashuleni.'
Kamukunji hakukuwa na mazingira mazuri. Ilikuwa ni kama shule nyingine tu za kawaida jijini Nairobi, ambapo wananchi wa maisha ya kawaida ambao wana uwezo wa kupata kiasi kisichozidi £1,000 kwa mwaka na pia vifaa vya ufundishaji shuleni hapo vilikuwa vya kawaida.
Makoba amekuwa mpenzi mkubwa wa soka kwa muda mrefu sana. Anaisapoti klabu ya Manchester United na wachezaji kama George Best, Robin van Persie ndio anawapenda lakini Roy Keane ndio zaidi.
Familia yake yote inapenda soka. Mumewe ni shabiki mkubwa wa Arsenal, watoto wake wawili wa kiume wote wanashabiki a Man united kama mama yao, lakini mtoto mwingine wa kiume yeye ni shabiki wa Chelsea.
Pamoja na kuwa na mapenzi na mchezo lakini Kenya haina vifaa vizuri vya michezo.
'Hatukuwa na uwanja pale Kamukunji hivyo nilikuwa naandaa mpango timu yangu kufanya mazoezi katika uwanja wa kuazima uliopo karibu na shule,' alisema Makoba. 'Uwanja wa kuazima ulikuwa unatumika jioni hivyo ilitubidi kuanza mapema, kabla ya wenye uwanja wenyewe hawajafika. Hivyo tulipendelea kufanya mazoezi asubuhi alfajiri mpaka kulipokucha kwa ajili ya watoto kurudi shule.'
Kujitoa kwa Makoba kulianza kulipa miaka 15 baadae wakati Kamukunji ilipoanza kukuza vipaji vya makinda ambao walienda kupata nafasi kwenye vilabu barani ulaya katika ligi tofauti.
Baadhi ya vipaji vilivyokuzwa katika shule ya Kamukunji chini ya uangalizi wa Makoba, miongoni mwao ni mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Dennis Oliech, 28, anayekipiga Ajaccio inayoshiriki ligi kuu ya Ufaransa, mshambuliaji mwingine Patrick Oboya, 26, ambaye amewahi kuchezea vilabu tofauti nchini Czech Republic na Slovakia, pia wapo wachezaji wanaokipiga kwenye ligi ya nyumbani kama Kevin Ochieng, winga ambaye ameshavichezea vilabu kadhaa vya Kenya.
Bila shaka majina makubwa katika soka la Kenya kwa hivi sasa ni Wanyama na kaka yake McDonald Mariga Wanyama, 26, kiungo wa ulinzi wa Inter Milan ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Parma.
Mariga angeweza kuwa mkenya wa kwanza kucheza katika ligi kuu ya England mnamo mwaka 2010, wakati Roberto Mancini alipojaribu kumnunua kwenda Manchester City, lakini alikosa kibali cha kufanya kazi nchini humo.
Japo suala hilo liliingiliwa kati na waziri mkuu wa Kenya wa wakati huo Raila Odinga, ambaye alitumia masaa kadhaa kuzungumza na waziri mkuu Gordon Brown na maofisa wengine, lakini ilishindikana kumpatia Mariga kibali.
'Siku zote niliamini Victor angeenda mbali,' anasema Makoba. 'Mara zote amekuwa mtaratibu, mpole na mwenye heshima. Mama yake Mildread na baba, Noah, walikuwa wakifanya kazi kwenye shirika la reli la Kenya wakati Victor akiwa mdogo.
Walikuwa maskini, wakiishi na watoto nane katika nyumba ndogo sana. Mildred anaishi kwenye nyumba nzuri sana, kwenye eneo zuri. Wanaendesha magari mazuri kama Hummer na Cadillac. Nina furaha sana na mafanikio ya vijana wangu.'
Makoba alihama kutoka Kamajunji mwaka jana na kuhamia kwenye shule ya wasichana watupu, ambapo jukumu lake ni kuendeleza vipaji vya soka na basketball kwenye shule.
No comments:
Post a Comment