Kocha wa Manchester United David Moyes kwa mara nyingine tena amesisitiza kwamba Wayne Rooney hatouzwa msimu huu, pia amekanusha kwamba amegombana na mchezaji huyo.
Chelsea tayari wameshatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa kwa ajili ya Rooney - huku kocha wa timu hiyo Jose Mourinho akiapa kutokata tamaa mpaka siku ya mwisho ya dirisha la usajili litakapofungwa.
Pamoja na yote hayo, Moyes amesisitiza kwamba hakuna kilichobadilika.
"Wayne Rooney hauzwi," Boss huyo wa United aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo wa ngao ya hisani jumapili jana. "Hakuna kiichobadilika kwenye suala hilo hivyo hakuna majibu yoyote ya zaidi kuhusu suala hili."
"Baadhi yenu hamtopenda kusikia kuhusu suala hili kwa sababu mmendika habari zisizokuwa na ukweli. Sijagombana na Wayne. Alifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha ziada kwa sababu aliomba iwe hivyo yeye mwenyewe."
Moyes pia alizungumzia kauli yake kwamba Rooney atakuwa fiti kuichezea England dhidi ya Scotland katikati ya wiki lakini sio kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Swansea City siku ya jumamosi.
"Nataka ajiunge na England. Bado hajapata usawa wa kimwili tayari kucheza mechi ya ushindani. Hajacheza mechi yoyote tangu aumie. Hivyo huwezi kudhani mtu wa namna hiyo kucheza mechi ya ushindani kwa muda mrefu.
"Nimeongea na Roy Hodgson kwa muda wa masaa mawili kwa muda tofauti. Itakuwa jambo zuri kwa Manchester United ikiwa atapata nafasi ya kucheza."
No comments:
Post a Comment