Search This Blog

Tuesday, July 9, 2013

LUIS SUAREZ: "HII NDIO SABABU RASMI YA KWANINI NATAKA KUONDOKA LIVERPOOL"


LUIS SUAREZ hatimaye amekiri sababu rasmi ya kwanini anataka kuondoka Liverpool - anataka kucheza kwenye Champions League.

Mshambuliaji huyo huko nyuma alikaririwa kwenye mahojiano huko Uruguay akisema anataka kuondoka kwa sababu anaandikwa vibaya sana na vyombo vya habari vya kiingereza na kuonewa chama cha soka cha nchi hiyo kwa matendo yake ya kumtukana kibaguzi mchezaji wa Manchester United Patrice Evra na kumng'ata mchezaji wa Chelsea Branislav Ivanovic.

Lakini wakala wake ambaye ni kaka wa kocha wa Bayern Munich, Pere Guardiola amekutana na kocha wa Liverpool Brendan Rodgers mkurugenzi mkuu wa Liverpool Ian Ayre katika uwanja mazoezi wa Liverpool Melwood jana na kuthibitisha kwamba kukosekana nafasi ya kucheza michuano ya ulaya ndio chanzo kikuu cha mteja wake kutaka kuondoka.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameonyesha ishara ya kuwa tayari kulipa kiasi cha £30million kupata saini ya Suarez lakini Liverpool walikataa ofa hiyo wakitaka dau la zaidi £40m.

Real Madrid pia wanatajwa kuandaa ofa nzuri kwa ajili ya kumsaini mshambuliaji huyo.

6 comments:

  1. Suarez kuondoka Liverpool yuko sahihi lakini hiyo sidhani kama ndo bei yake halali wanayoitaka Liverpool.

    ReplyDelete
  2. Hakuna mchezaji mkubwa kuliko timu,inatakiwa wamuache aende zake liver bado imara sana wanacheza kwa asilimia 60%bila yeye na akiwepo ni 40%tu wanacheza. Tunakutakia kila la heri suarez

    ReplyDelete
  3. Hata akiondka pengo lake litazbika,mbona aliondka torres ambaye pia alitegemewa sana na timu,lakn mbona liverpool ilijipanga na ikasimama imara??? Wamwache aende bhana liverpool ni timu kubwa haiwezi kuyumbishwa na mtu mmoja....liverpool you will never walk alone.

    ReplyDelete
  4. Yuko sahihi kabisa tokea amejiunga liverpool amekosa champions league na hakuna uhakika kama mwakani liverpool watafuzu. Suarez aliwahi kukaririwa akisema atabaki hata kama hawatafuzu. Hizi taarifa za kuondoka amezianzisha baada ya msimu kuisha. Lakini, je liverpool ndio wanamtuma abague watu au ang'ate watu. Ni kweli kuna wakati vyombo vya habari na fa havimtendei inavyopaswa. Mfano walivyolishughulikia kesi yake na terry kuhusu ubaguzi. Yeye ndio anawapa sababu za kumwandika vibaya kwa sababu ya ujinga wake. Hata kama akienda real madrid kama anavyotaka yeye, bado ataandikwa vibaya tu asipoacha tabia zake. Mfano Holland walimwita carnibal baada ya kumg'ata mwenzie. Sasa sijui ataenda nchi gani ambayo watamuacha ang'ate na kubagua watu halafu wasimwandike vibaya. Liverpool ilikuwepo kabla ya Suarez na itaendelea kuwepo baada yake. Waliondoka wakina Owen, mascherano, torres na bado iliendelea kuwepo. Pengo pekee waliloshindwa kuziba ni la Alonso. Lakini pia inawekana akapata anachokitaka (champs league) lakini asiwe na furaha kama torres. Hata kama akihama cha msingi ni kubadili tabia zake la sivyo yatakua yaleyale.

    ReplyDelete
  5. mi nafikiri kabla ya kufikiria kuhama angefikira kwanza kubadili tabia zake. Huyu sio wa kuwekea bet hata kidogo maana anaweza kufanya vizuri lakini kesho akafanya usichotegemea. Leo kabagua na kung'ata kesho hatujui atafanya nini. Nafikiri hata timu atakayoenda inabidi ijue hilo. Anaweza kufanya kitu kitakachosaidia au kucost timu hata kama ni fainali

    ReplyDelete