Kozi ya makocha na marefa kwa ajili ya michuano beach soccer imeanza leo jijini Dar es Salaam. |
Kozi hiyo itafanyika kwa wiki nzima kwenye klabu ya Escape iliyoko karibu na Safari Carnival, Mikocheni karibu na makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)- JKT Mlalakuwa. Uzinduzi umefanyika leo saa 3 kamili asubuhi na kuhudhuriwa na Raisi wa Shirikisho la soka nchini Leodgar Tenga, Katibu mkuu Angetile Osiah na mkurugenzi wa ufundi Sunday Kayuni.
Washiriki wa kozi hiyo itakayokuwa chini ya wakufunzi kutoka Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ni 60 ambapo 30 ni makocha wa mpira wa miguu na 30 wengine ni waamuzi wa mpira wa miguu. Miongoni mwao ni wachezaji wa zamani kama Boniface Pawasa, Ally Mkongwe, Juma Mgunda na wengineo wengi.
Wakufunzi hao wa FIFA ni Angelo Schirinzi kutoka Uswisi kwa upande wa makocha wakati George Postmar kutoka Uholanzi ndiye atakayewanoa waamuzi. |
Mtu akiwa hafamiani na Shaffii Dauda hawezi kupata nafasi ya kushiriki mafunzo haya,au Shaffii Dauda akuandike kama mshiriki kwasabababu ya kujuana na kubebana.
ReplyDeleteBeach soccer, karibun sana pande za kigambon, we are da best katka hilo... tumechexa takriban mwaka wa tano au wa 6 tunacheza mpira wa baharin.. tc realy gud we show great skills, karbun sana... mjimwema kigambon... we enjoy much cz kigambon inafukwe nzur sana...
ReplyDelete0659445718, kwa maelezo zaid na uchambuz yakinifu wa soka...
By
Makaveli Jr. Killuminati