DAVID MOYES ameanza kazi rasmi leo ya kufiundisha klabu ya Manchester United.
Kocha huyo wa zamani wa Everton leo asubuhi ndio ameanza rasmi kazi ya kuwa boss wa benchi la ufundi la Manchester United akirithi mikoba ya msoctland mwenzie Alex Ferguson.Moyes aliwasili katika kituo cha mazoezi cha Carrington mnamo saa mbili asubuhi akiendesha gari la alilopewa na wadhamini wa klabu hiyo Chevrolet.
Aliwapungia mkono waandishi wa habari huku akitabasamu nje ya uwanja wa Carrington kabla ya kuingia ndani na kuanza rasmi kazi yake ya kupeleka mbele gurudumu la United.
Wakati huo huo Manchester United leo imethibitisha uteuzi wa makocha Steve Round atakayekuwa msaidizi wa Moyes, Chris Woods kocha wa makipa na Jimmy Lumsden kama kocha wa kikosi cha kwanza.
Makocha hawa watatu wanakuja kurithi nafasi zilizoachwa wazi na Mike Phelan, Rene Meulensteen na Eric Steele, ambao wote waliondoka baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson mwezi May mwaka huu.
Makocha hawa watatu wote wamefanya kazi na Moyes wakiwa Everton - na baada ya kuthibitishwa kwao Moyes alisema: "Nimefanya kazi na Steve, Chris na Jimmy kwa miaka mingi na nina furaha kwamba wameamua kuungana nami kwenye klabu hii kubwa.
No comments:
Post a Comment