TIMU
ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefungwa mabao 4-2 dhidi ya Ivory
Coast na kuzima harakati zake za kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2014
huko Brazil.
Watanzania
wengi na wadau wa michezo walidhani Taifa Stars ingeweza kusonga mbele katika
harakati hizo za kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2014, lakini sasa ukweli
umejidhihirisha.
Sasa
wengi wamekubaliana na uhalisia wa mambo kwamba, inahitaji muda kidogo kuona
Taifa Stars ikisonga mbele katika kuelekea kufuzu Kombe la Dunia na siyo rahisi
kama ilivyodhaniwa hapo kabla.
Ni
mambo mengi yaliyotokea katika mchezo dhidi ya Ivory Coast ambayo yaliigharimu
Taifa Stars licha ya uwanja kujaa idadi kubwa ya mashabiki waliokuwa
wakiishangilia timu yao bila kuchoka.
Jambo
la msingi ni kwamba, Taifa Stars ikiwa katika harakati za kuhakikisha inafuzu
Kombe la Dunia wengi tulisahau kwamba, kwa ‘reality’ ilikuwa ngumu kwa Taifa
Stars kufuzu fainali hizo japokuwa kwa mapenzi tulidhani timu hii ingeweza
kufuzu kwa kuanza na vipigo kwa timu za Morocco na Ivory Coast.
Tukitazama
mchezo kati ya Taifa Stars na Ivory Coast kuna baadhi ya mambo yalionekana
kwamba bado tuna safari ndefu ya kufuzu Kombe la Dunia kama kweli tuna nia ya
kufanya hivyo.
Mambo
mengi mno yalijitokeza katika mchezo kati ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast
na haya ni machache kati ya mengi yake;
TAIFA
STARS ILICHEZA KUFURAHISHA MASHABIKI SIYO KUIFUNGA IVORY COAST
Kiungo
wa Manchester City, Yaya Toure alicheza kama mshambuliaji na alitimiza majukumu
yake kama straika hasa kwa kutokubali kukaa na mpira kwa muda mrefu licha ya
kuwa na uwezo wa kufanya hivyo.
Wakati
Toure mwenye uwezo wa kumiliki mpira atakavyo na kufanya jambo lolote hakutoa
nafasi hiyo zaidi ya kutafuta ushindi kwa timu yake, viungo na wachezaji wengi
wa Taifa Stars walikuwa wakitumia muda mwingi kukaa na mpira bila ya sababu ya
msingi.
Kiungo
Salum Aboubakar ‘Sure Boy’ mara nyingi alikuwa kitumia muda mwingi kukaa na
mpira na kutaka kupambana na wachezaji wa Ivory Coast licha ya kuonekana wazi
kwamba mara zote alizidiwa nguvu.
Tazama
hata Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Frank Domayo walikuwa wakitumia muda
mwingi ‘ku-hold’ mipira huku wakitoa pasi zisizo na macho na kujikuta
wakipoteza mipira mingi kutokana tu na vitendo vyao vya kuchelewesha mipira.
Pamoja
na vitendo hivyo kuwa hatari kwa timu, lakini mashabiki walikuwa
wakiwashangilia kwa nguvu viungo wa Taifa Stars bila ya kujua madhara ya
kufanya hivyo. Hao walijali zaidi kushangiliwa kuliko umuhimu wa mchezo husika.
Taifa
Stars ilihitaji zaidi kucheza kwa kutokubali kukaa na mpira kwa muda mrefu kwa
wachezaji wake ili kuitengeneza nafasi za haraka za kupata bao ili iweze
kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Kuanzia
Sure Boy, Kiemba, Kazimoto na Domayo, wote walionekana kufurahishwa na kelele
za mashabiki waliokuwa wakiwashangilia kutokana na chenga na madoido mengine
waliyokuwa wakiyafanya uwanjani.
SAFU
YA ULINZI ILIPAPARIKA
Ilikuwa
kama kila mchezaji ameahidiwa kiasi kikubwa cha fedha, kwani mara nyingi
wachezaji wa Taifa Stars hawakucheza katika nafasi zao na hilo liligharimu timu
na kujikuta wakilala mabao 4-2.
Erasto
Nyoni ndiye beki anayeweza kuondoka na lawama nyingi lakini halikuwa kosa lake
wakati mwingine kwani alilazimika kwenda katikati kusahihisha makosa ya mabeki
wa kati na kuisahau nafasi yake.
Ilionekana
wazi kwamba yalikuwepo mawasiliano hafifu juu ya kutengeneza mtego wa kuotea
yaani ‘offside trick’ na matokeo yake Ivory Coast walitumia vyema mwanya huo na
kujipatia mabao manne.
Baada
ya kuonekana ‘njia’ tangu dakika za mwanzo, beki Erasto Nyoni inaonekana
hakupata ushauri wa kutosha kuhusu kutulia na kucheza soka kwani hata makelele
ya mashabiki yalimfanya aonekane mtu asiyefaa kikosini. Lakini alikuwepo benchi
anayeweza kumudu nafasi yake moja kwa moja?
NGUVU
HAFIFU
Wachezaji
wengi wa Taifa Stars walionekana kutokuwa na nguvu ya kupambana na wenzao wa
Ivory Coast kutokana na hali halisi ya miili yao.
Sure
Boy mfupi na mwenye mwili mdogo alionekana kama mchezaji wa kawaida mbele ya
Yaya Toure mwenye mwili mkubwa na nguvu, na mara nyingi Toure aliiwahi mipira
ambayo ingeweza kuwahiwa na Sure Boy.
Domayo
naye hakuweza kufua dafu mbele ya Traore Lucina na Jean Jacques ambao wote ni
watu wa miraba minne.
WAO
WALIMKATAA KALOU, SISI TUKAFUATA SAMBUSA
Kabla
hata ya mapumziko, waandishi kadhaa wa Ivory Coast walionekana kutopendezwa na
uchezaji wa Salomon Kalou ambaye muda mwingi kila alipopewa mpira alikuwa
akitaka kukaa nao kwa muda mrefu kama ilivyokuwa kwa kina Sure Boy na wengine
wa Taifa Stars.
Waandishi
hao walionekana wazi kuchukizwa na hali hiyo na mara kwa mara walionyesha wazi
kutoridhika na uchezaji wa Kalou.
Ulipofika
wakati wa mapumziko, waandishi hao walishuka chini katika vyumba vya
kubadilishia na kuzungumza na baadhi ya maafisa wa timu yao ili kutazama
uwezekano wa kumpumzisha Kalou kwa maslahi ya nchi.
Wakati
hayo yakitokea kwa Ivory Coast, waandishi wa Tanzania walikuwa wamekaribishwa
ukumbi wa VIP kupata vitafunwa kama sambusa, mishikaki na vinywaji baridi, hao
hawakuwaza kupeleka mawazo yao kwa benchi la ufundi na hata wangefanya hivyo
wasingesikilizwa kutokana na utaratibu ulivyo.
Mbaya
zaidi siyo waandishi tu, hata viongozi kadhaa wa Kamati ya Ushindi ya Taifa
Stars nao walionekana wakiwa VIP wakijichana kana kwamba Taifa Stars ipo katika
nafai nzuri. Kumbuka hadi muda huo timu ilikuwa ipo nyuma kwa mabao 3-2.
HONGERA
ULIMWENGU
Kama
kuna mchezaji wa Ivory Coast aliyeomba mpira uishe haraka kuliko wengine basi
ni Bamba Souleman ambaye alikuwa akicheza kama beki wa kati anayemkaba
mshambuliaji wa Taifa Stars, Thomas Ulimwengu.
Ulimwengu
alimmudu vizuri Bamba kiasi cha kumkimbiza na kuufanya mpira atakavyo hadi
kufunga bao moja. Mara nyingi Bamba alizidiwa nguvu na kasi na Ulimwengu kiasi
cha kulalamikiwa na wenzake.
Kama
wachezaji wanne tu wa Taifa Stars wangeweza kucheza kama Ulimwengu, ni wazi
timu hiyo ingepata matokeo mazuri na ya kuridhisha.
BY ELIUS KAMBILI
Nimesoma makala yako na nimekubali. Kwa kuongezea tu. Code voire walichofuata ni matokeo ss hatujitambui na hatutajitambua kwa kuwa tunategemea mpira uamuliwe na dua za watanzania na nasaha za viongozi kwa wachezaji. Tizama benchi letu la stars na kila mmoja aulizwe nn kilichomuweka pale ni kichekesho kitupu utakaposikiliza maelezo yake.mwisho hata ukisoma magazeti yetu jinsi yalivyoripoti mechi hiyo hadithi nihiyohiyo ya sambusa bagia na soda za mechi ijayo .niandike vzr ili nisikosane na fulani mwenye dhamana pale au nisimkosoe mchezaji fulani kwa kuwa anatoka timu yangu Mungu akupe nn umepata bao dk 1 . Unataka dua gani? Ya watanzania.
ReplyDeletenakubaliana na wewe,ila tukubali tukatae,Erasto Nyoni ndiye aliyetuchomesha jana,na si jana tu,bali mechi 2 za nyuma nazo alituchomesha pia.Wasaidizi wa Kim hawajui wajibu wao bali kuendelea kubeba wachezaji wanaotuliza washabiki kila siku.
ReplyDeleteNaheshimu sana baadhi ya chambuzi zako mwenye blog ila hapa ngoja nikuweke sawa. Punguza jazba maana umekaa mkao wa lawama zaidi wakati unafaham kwenye soccer pale unapokosea ndipo unaumizwa. Unatumia maneno ya wao taifa stars wakati ni timu yetu wote wadau wa mpira Tanzania.
ReplyDeleteSuala la kukaa na mipra.
Shafi huwez kuwa na pass za haraka kamaunavyodhan pasipo kuwa na uwezo wa mpira wa kasi. Sure boy aliyecheza ndiye yule yule wa azam tatizo tumefungwa. Kiemba alijituma sana na ilimpasa akae na mpira na alimudu kufanya hivyo maana nae si mtu wa kasi. Nadhan ulihitaji wacheze kama kina iniests jambo ambalo hata ww ungepewa timu isingewezekana. Flopy kwenye mido ni domayo sawa maana alionekana kuwa na hofu baada ya kuzidiwa kati.
Kuhusu defence nakubaliana na udhahifu ila sio wa kudhihaki kama unavyosema waliahidiwa pesa. Kumbuka walitumia nguvu zao kulibeba taifa na wewe kama mfau sio unapopata matokeo mabaya unajitoa kifua mbele kukashifu.
WAtanzania wenzangu hafa ninyi wenye access za media nitaendelea kuwanyooshea vidole kwa kuwa mnatoa mchango wa kudhihofisha zaid kuliko kusaidia.
Sasa umekuwa mdaku kuangalia watu wanaenda kula sambusa. Je ni kwel waandishi wote wa ivory walishuka kutoa mapendekezo? Na je ulipoona wanakula sambusa ulichukua hatua gani?
MAJUNGU SI MTAJI ndugu zanguni. Jambo la kitaifa linaanza kuleta kelele. Haya kazi ya sisi mashabiki ni kushangilia mwanzo mpaka mwisho wa game sijui ulitaka tuboo!
Kweli ulimwengu alikuwa shujaa ila je angecheza mwenyewe uwanjani angeweza? Kila mmoja ametoa mchango wake pale.
NI HAYO TU.
Hii ni tathmini ya kukurupuka kama ilivyo kawaida yetu wabongo.Tathmini hii imejikita katika hisia badala ya uhalisia na kwa haraka haraka unaweza kukisia iliandikwa kwa hisia za kabla ya mechi na siyo matukio halisi ya wakati wa mechi.Wachezaji wetu walicheza kwa maelekezo ya kocha na walichokifanya ndiyo uwezo wao ulipoishia.Tulichozidiwa ni mbinu za mchezaji mmoja mmoja ambazo wenzetu wako juu kutokana na uzoefu wao wa mechi za aina hii.Tunapenda kupata tathmini kutoka kwa kwa makocha, wataalamu halisi wa soka na wachambuzi huru badala ya uchambuzi wa hapo juu ambao ni dhahiri umefanywawa na mtu ambaye hata kabla ya mechi tayari alikuwa anaiombea mabaya stars na pia ana maslahi kwenye uchaguzi mkuu wa TFF
ReplyDeleteBado tunaweza cha msingi tusikate tamaa bali tuendelee kujituma zaidi.!
ReplyDeletemimi nimeona mambo kama matatu,kwanza ni kutoelewanba kwa wachezaji kwani hata magoli tuliyofunwa ni marahisi sana,
ReplyDeletepili psychologically wachezaji wa TZ kama dumayo,na nyoni walipaniki,
labda la tau na la kuongezea ni kuwa tukubali tukatae uwezo wetu mdogo,,kama ligi ni mbovu unategemeaje kupata wachezaji wazuri timu ya taifa??
mapendekezo::lets invest in football,,haya mashindano makubwa sio ndo mwisho wake kwani sio mda yatakuja ya chan na baadae mataifa AFRICA,nguvu tulizotumia kutka kwenda brazil ndio tutumie hizo hizo kutengeneza timu bora ya TAIFA ya miaka ijayo,,
ni hayo tu
nakubaliana kabsa na bwana Geogre Paskal
ReplyDeleteshaffih hukutuchambulia mechi ya tanzania 3 morocco 1 kwa nini umechambua kwa haraka sana mechi hii tanzania 2 ivory coast 4
ReplyDelete