Jumapili ya jana matumaini ya watanzania kuishuhudia timu yetu ya taifa ikicheza michuano ya Kombe la dunia yaliisha rasmi baada ya kupoteza mchezo muhimu dhidi ya Ivory Coast kwa kufungwa 4-2 katika uwanja wa Taifa.
Kiuhalisi watu wengi walianza kupoteza matumaini baada ya kufungwa wiki iliyopita jijini Marrakech 2-1 na Morocco, lakini mimi kama Shaffih Dauda nilishauona uhalisia wa nafasi ya Tanzania kwenda Brazil kwamba ni finyu mno. Hili nililiona tangu mwanzo wakati inajiandaa kuanza kuisaka tiketi ya kwenda Brazil.
Ilikuwa tarehe 9 November, 2011 Siku ya jumatano niliandika makala yaliyokuwa na kichwa cha habari "WATANZANIA TUSAHAU WORLD CUP 2014."
Niliyoyandika takribani miaka mwili iliyopita yamejidhihirisha jana. Nguvu iliyotumika katika kuhakikisha Stars inacheza World Cup 2014 ihamie katika kuunda mfumo mzuri wa soka letu ambao ndio mkombozi pekee katika kuifanya Tanzania kung'ara katika soka la kimataifa. Zile kamati za saidie stars ishinde ziundwe sasa au iliyopo iendelee kwa malengo ya kuhakikisha tunajipanga vizuri ili mnamo tutakapoanza safari ya kuitafuta nafasi ya kwenda Russia 2018 tunakuwa tayari kiushindani ili kuweza kupambana na timu yoyote tutakayopangwa na hatimaye tutimize ndoto yetu ya kushiriki michuano mikubwa zaidi kwenye ulimwengu wa soka.
upuuzi mtupu na kukosa uzalendo,huwezi kujisifu kwa ujinga kama huo.Tusipende kutafuta sifa kupitia majanga kama haya ili tuonekane wataalamu au wajuaji wakati ni ubahatishaji na ubabaishaji mtupu. Tunaweza kutekeleza hayo yote uliyoyaandika hapo juu na bado tusifanikiwe kushiriki fainali za kombe la dunia,kwa kuwa hicho sio kigezo pekee cha maendeleo ya soka.Kuna nchi nyingi tu ziko juu zaidi yetu na hazijawahi kushiriki fainali za kombe la dunia.Maendeleo ya soka ni mchakato endelevu,hapa tulipofika sio pabaya ukilinganisha na tulikotoka kwa kuwa ni lazima ku-aim high ili uweke mikakati ya kiwango hicho.kikubwa ni kujenga soka letu kwa kila mmoja kuwajibika kwenye nafasi yake kuanzia katika ngazi ya klabu,wilaya,mkoa na taifa ili wachezaji wetu wapate fursa za kucheza ligi kubwa na za maana ulaya na pia ku
ReplyDeleteKuna watu wameumbwa kazi ya kukatisha tamaa watu wengine. Watu wasipofanikiwa wao ndio wanafurahi, halafu wanakuja na michanganuo yao ya kinafiki.
ReplyDeleteMwamba
Kuna watu wameumbwa kazi ya kukatisha tamaa watu wengine. Watu wasipofanikiwa wao ndio wanafurahi, halafu wanakuja na michanganuo yao ya kinafiki.
ReplyDeleteMwamba
unafiki tu
ReplyDeleteBwana shaffih mafanikio ni pamoja na uzalendo.. hivi kuna inchi iliyo invest kwenye mpira kama south Africa? Nadhani unajua yaliyowakuta. Mafanikio ni pamoja na kukuza timu za wakubwa wakati unakuza vipaji.. pili uwashahuru hao viongozi wa soka wanakumiliki waache wachezaji waende kupata experience nje ya nchi.
ReplyDeleteni mwendawazimu tu anayeweza kufurahia matokeo mabaya ya stars eti utabiri wake umetimia.Hizi ni sifa za kijinga na kuendekeza kasumba ya kusifia timu za ulaya na wachezaji wanaocheza ulaya na kuibeza nchi yake.Kujua soka au kuchambua soka sio kujua habari za timu za ulaya kwa kusoma kwenye mitandao na baadaye kuwadanganya watu kwenye spoti bar
ReplyDeleteMalinzi angekuwa Rais wa TFF na Michael Wambura Makamu wake na Shafii Mkurugenzui wa Ufundi lazima Stars ingeshinda na kwenda Brazil kwa sababu wangetumia fedha za mifukoni mwao kuiwezesha stars kushinda wala tusingekuwa na kamati ya ushindi,na pia program yao ya maandalizi ingetoka Uingereza
ReplyDeleteKusema kile ukionacho kama ni kweli sio kukosa uzalendo. Kesho kutwa ni kina nyie nyie mtakaopiga kelele pale timu ya U17 inaposhindwa kuweka kambi ya muda mkisahau hela yote iliyotumia kujaribu kutupeleka 2014. Msiwe wasahaulifu kiasi hiko.
ReplyDeleteTatizo mnatokwa na povu bure ivi ukimwona gervinho au yaya toure unadhani kaibuka tu misingi ndio inafanya timu iwe na mafanikio wako wapi senegal walipika kizazi kikaisha wamefulia tusikwepe ukweli ,investment kwenye mpira wa vijana ndio tiba ya africon na world cup.
ReplyDeleteShaffih..hata kama hilo lilijulikana we ulitaka tusiipe support?je hao vijana unaotaka wakuzwe si ndio wale wengine wamo kwenye timu ya taifa.So mi nafkiri ile timu inapaswa kupewa support kwani inaundwa na vijana wadogo ambao wanahitaji experience ya mechi kubwa.hatuwezi kukaa na vijana wadogo huku hawapati mechi kama zile za kujipima.
ReplyDeletenchi ya oman ina fedha nyingi na haidaiwi na mtu yeyote imewekeza ktk soka kama unavyosema wewe shaffih sisi tufanye mbona haijafuzu kombe la dunia tena katika zone yao si ngumu kufuzu kama zone ya afrika. hebu angali shaffih tanzania mara zote huwa inapangwa na nani ktk kufuzu. lazima kundi la tanzania kuwe na vigogo viwili imekosewa sana kimoja hebu hiyo russia 2018 watupange TANZANIA,LESOTHO,CHAD,BOTSWANA halafu uje uchambue unafiki wako.
ReplyDelete