Kuelekea
mchezo dhidi ya Simba SC mei 18, Baraza wa wazee wa klabu ya Young
Africans limeomba mwamuzi wa mchezo huo achezeshe kwa kufuata sheria 17
zote za mchezo na kwa kufanya hivyo mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya
Vodacom watoto wa Jangwani lazima wataibuka na ushindi katika mchezo
huo.
Akiongea na wandishi wa habari kwa niaba ya baraza la wazee makao
makuu ya klabu, katibu mkuu wa baraza la wazee Mzee Ibrahim Akilimali
(Ibrahimovich) amesema wanaamini kikosi cha Yanga kitaibuka na ushindi
katika mchezo huo ikiwa mwamuzi atachezesha kwa kufuata sheria zote 17
na kanuni za soka.
Akilimali amesema Yanga ni timu bora kwa sasa
katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kila mmoja anajua hilo, tuna
wachezaji wazuri wenye kiwango cha hali ya juu ambao wamepikwa
wakapikika wakaiva matunda ya mafunzo yao ndio yaliyotupatia ubingwa
kabla ya ligi kumalizika.
Aidha aliongeza kuwa "Tunaahidi kwamba
tutamfunga Simba SC siku ya mei 18 kutokana na umoja wetu, mshikamano na
uongozi bora chini ya mwenyekiti Yusuf Manji na makamu wake Clement
Sanga ambao mpaka sasa wameifnaya timu ya Yanga kuwa ya kuogopewa ukanda
wote huuu".
Naye Mzee Hashim Mwika aliongeza kuwa waanahidi
ushindi katika mchezo huo, idadi ya mabao haijalishi lakini kikubwa
tunasema lazima tumfunge Simba mei 18 kikubwa tunaomba mwamuzi achezeshe
kwa kufuata kanuni 17, na kama wakifanya hivyo basi Simba Sc wajiandae
kupokea mvua ya mawe siku hiyo.
"Mwaka jana walitufunga kwa sababu
hatukuwa pamoja, hatukua na maelewano lakini hivi sasa Yanga ni moja
kuanzia viongozi, wachezaji, makocha na wanachama hivyo tunamini kwa
kuwa pamoja na timu yetu bora lazima simba achezee kichapo "alisema mzee
Mwika
Mbona wanaanza kutoa kumtisha refa mapema, wasubiri tu muda ufike wakutane na Simba mtoto ili wajue mtoto wa Simba hana tofauti na Simba kamili.
ReplyDeletemhhh....!!!! Hawana jipya hao wazee..!! wasianze kujitetea mapema...!!! Msimamo wetu(simba)upo pale pale....!!! Lazima wachezee kichapo cha aibu na manji wao...!!!
ReplyDeleteWazee nyie poleni! Hivi kwanini hampumziki? Mtakufa kwa pressure za soka bure!! Ile ni ndoa ya kanisani, haina talaka labda mmoja wapo awe amekufa.Muwe wamoja au mbalimbali haijarishi, kichapo kipo palepale!! Mnyama nuksi.
ReplyDeleteSOMA alama Mzee umesahau kuvua balakashia mpira uwanjani siyo ofisini leta timu halafu ukishinda uonge. Acheni vitisho kwa lefa.
ReplyDelete