Search This Blog

Friday, May 10, 2013

BAADA YA MTANDAO HUU KUTOA BARUA HALISI YA FIFA - TFF WATOA SIKU SABA SHAFFIH DAUDA KUTOA MAELEZO ALIPOITOA BARUA HIYO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemtaka Shaffih Dauda ambaye ni mmiliki wa tovuti ya www.shaffihdauda.com kutoa maelezo kuhusiana na barua ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) aliyoiweka kwenye mtandao wake huo.

FIFA ambayo ilisimamisha mchakato wa uchaguzi wa TFF baada ya baadhi ya wagombea kuulalamikia, baadaye ilitoa maelekezo kuhusu mchakato huo kwa barua ambayo iliituma kwa Rais wa TFF, Leodegar Lenga.

Rais wa TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari ambao Dauda alihudhuria alibainisha kuwa barua hiyo ya FIFA hawezi kupewa kila mtu, na kuruhusu waandishi kuisoma kwa Ofisa Habari wa TFF bila kuondoka nayo.

Wakati Rais Tenga anazungumza na waandishi wa habari (Mei 2 mwaka huu), nakala ya barua hiyo ya FIFA ilikuwa kwa viongozi wakuu wa TFF pekee, na viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Hivyo TFF imemtaka Dauda kutoa maelezo ya mahali alipoipata barua hiyo ndani ya siku saba.

26 comments:

  1. Huu ni utovu wa maadili na mhusika anapaswa kuwa mtu wa kwanza kufikishwa kwenye kamati ya maadili mara itakapoundwa.Kama hivi sasa yuko nje ya TFF ananyofoa nyaraka za TFF na kuzisambaza KWA WASIOHUSIKA, je atakapokuwa ndani ya TFF hali itakuwaje?Kwa vyovyote nakala ya barua hii atakuwa ameipata TFF au Wizarani. TFF wanapaswa kuwa makini na wafanyakazi wao wanaovujisha nyaraka.Huko serikalini ni vigumu sana kuvujisha nyaraka isipokuwa kama kuna kigogo anayefacilitate uvujishaji huo kwa maslahi ya kundi analolishabikia kwenye uchaguzi wa TFF zao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wachaa mambo yawe hadharani, tutaficha mpaka lini.. mpiraaa kazima usonge na lazima kuwe na watu kama hawa wanaojiyoa myhanga...wewe utakuwa ni mmoja kati ya wahusikaa…

      Delete
    2. Watanzania ndo mana hawaendelei kabisa. Asa inahusu nini kurusha vitu visivyotuhusu.

      Delete
  2. Jamani kwani kuna jipya lipi ktk hiyo barua..it is a public domain..wkt mwingine najiuliza hivi TFF imekuwa ni mahala pa siri, lkn hata kama pangekuwa mahala pa siri jamani hata hili la mchakato wa uchaguzi ambao ulikuwa public interest na tukafika hapa tulipo...nafikiri hawa jamaa TFF wameshapoteza mwelekeo..thanks God kwamba muda c muda wataondoka..na hata hawa waajiriwa naamini kwa utendaji huu baada ya kuchaguliwa uongozi makini utawapiga chini...

    ReplyDelete
  3. wasikutishe hao

    ReplyDelete
  4. Shafii dauda huna maadili na aliekupa hafai kuwa kiongozi

    ReplyDelete
  5. FIFA wenyewe hawajasema kama hiyo barua ni siri iweje Tenga na Jamaa zake watafute njia za kuficha ukweli wakati wawakilishi wa FIFA kila mtu aliwaona. kaka Shaffih wewe piga mzigo twende, ni imani yangu kuwa wewe umekuwa mkombozi wa soka la Tanzania,kama MANDELA alifungwa jela miaka 27 lakini ukombozi wa S.A ukapatikana basi ndivyo itakavyo kuwa kwako na soka la Tanzania.Tena hakuna sababu ya kujieleza kwani ukweli na uwazi ni 20% ndani ya TFF,KATIKA MANENO YA TENGA KWA WATANZANIA KUNA MAMBO HATUKUYASIKIA,MFANO;"MISUSES OF FUNDS" NA KWA-NINI AONGELEE MAMBO YA KATIBA TU WAKATI KUNA MENGI YAMESEMWA NA FIFA."LET US MAKE THIS AS A STARTING POINT". MAY OUR ALMIGHTY GOD GUIDE YOU AS YOU PREPARE/MAKE DECISION TO RESPOND UP ON SUCH HUMILATION ORDER..!!!!!

    ReplyDelete
  6. Sasa unafanyaje kaka Shaffih?.Wambie uliikota mitaa ya karume.Tenga anatapatapa na aibu aliyoipata.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yes. pale mlangoni kwa ofisi ya yenga. uliikuta ikazagaa zagaa ukaiokota. wenyewe ndio wazembe. wajieleze wao kwanza, dauda amepataje?

      Delete
  7. Kuna mambo mengi sana ya msingi ya kujadili juu ya mustakabali wa maendeleo ya mpira ndani ya nchi yetu,kuliko kutaka kuanza kufatilia na kujadili juu ya wapi barua ilipopatikana..Inawezekana nikawa mpofu juu ya hili,ila km waandishi walipewa ruhusa ya kuisoma na nakala kusambazwa kwa wahusika,tafsiri yake nchi imeshafahamu kinachoendelea,kwa kuruhusu watu waone kilichopo ndani,tafsiri yake ni kuwa hiyo sio barua ya siri tena,.Kama si siri tena,kuna ubaya gani kwa sisi wadau tusiokuwa na uwezo wa kuisoma hapo tukaiona hata kupitia kwenye vyombo vya habari.?Maana hata yaliyoelezwa ni yaleyale ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na wadau,na kila mmoja alitegemea matokeo ya namna hiyo..Mi nadhani tatizo labda lipo kwa mheshimiwa rais,ambapo aliitolea ufafanuzi ambapo nahisi kabisa kuna baadhi ya maneno hakuyaweka clear,alilieleza kiujumla zaidi kwa kuonesha kuwa wao hawakukosea sehemu yeyote tangu mchakato wa marekebisho ya katiba hadi mchakato wa uchaguzi.Lkn kumbe mambo yakaelezwa tofauti na jinsi tulivyomsikia..Mi nadhani km kuna pahala ambapo mmiliki wa blog hii alivunja sheria au aidha katiba ya TFF au katika ya nchi,hapo ndio anaweza kupewa amri yeyote aitekeleze.lkn km ni kinyume chake,basi tuache kuteka tention za watu kana kwamba kuna jambo zito sana linalohitaji mjadala mkubwa kiasi cha kupoteza muda,nguvu na mali ktk kulisolve..Tuache siasa za chuki hasa kwa wale wanaokosoa,kuyasema au kufichua maovu..SHALL WE MAKE IT..!!!???

    ReplyDelete
  8. Just foolish leodgership.Jukumu la kutunza siri ni la mwenye siri mwenyewe si mpata siri by the way hakuna cha siri kwenye hiyo barua zaidi ya kuanikwa kwa utumbo uliofanywa na TFF hapo awali. Ina maana hilo ndilo la siri?!!!

    ReplyDelete
  9. Kuna nini ambacho hutaki Watanzania wakijue kwenye hiyo barua kwani hiyo barua ni yako binafsi acheni ukilitimba wenu bwana kama FIFA waliuona uozo mahali wacha na sisi tujue maana mmezoea kuficha madhambi yenu sasa yakianikwa hadharani mnaona aibu.Tunayo haki kikatiba kupata habari zote zilizozungumzwa na FIFA na matokeo yote bora SHAFFIH umeitoa hadharani wangebadilisha maelekezo hao lakini mpaka hapo wameumbuka. swala kusema umeipata wapi si hapo TFF si waliwaita muisome palepale sasa anauliza nini wasikutishe bwana.

    ReplyDelete
  10. Du! Hii ndo Tanzania.Ina maana "ukweli na uwazi" uliishia mara tu mkapa alipotoka ikulu? Baba sneijder, aluta continua

    ReplyDelete
  11. Demokrasia hiyo ndio misukosuko yake kama ingekua siri isinge kua na haja ya maelezo ya waandish wa habari na hilo shirikisho sio la mtu binafsi, aibu imewakuta na unafki wao piga mzigo upo kwa ajili yetu sio wao.

    ReplyDelete
  12. hakuna jipya hapa

    ReplyDelete
  13. shaffi hufai kuwa kiongozi hata tone!sidhan kama proffesional code of conduct unaijua si kila kitu lazima public wajue kwasababu ni kwa matumiz ya ofisi ndio maana kuna stamp za SIRI,UNATAFUTA SIFA AU UNAKUWA KWENYE HEAD LINE NDIO TABIA YAKO?UBK UNAKUSUMBUA,

    ReplyDelete
  14. TFF wako sahihi kama barua toka FIFA is not for public consumption. Hapa inabidi tujulishwe sisi tusiojua je Dauda aliipata barua hiyo through proper channels? Na kama aliipata kihalali, alitoa taarifa au kuomba ruhusa ya kuipublish kwenye website yake? Je kwa kuiweka kwenye website, TFF inapata hasara gani kwa wadau wengi kuisoma?

    ReplyDelete
  15. Kaka shaffih kwanza nikupongeze kwa kutupatia taarifa muhimu na kwa muda muafaka sisi tuliopo kampla na nairobi khs michezo huko kwetu TZ. Namfahamu makamu wa kwanza wa TFF ni muajiliwa wa serikali aliisha ona wapi barua ya wazi ikafichwa kama ya siri? Hiyo barua ni ya wazi na wanatakiwa pia kuweka covering letter na kuambatanisha hiyo barua kwenda kwa serikali kama hawakupata nakala ili kutoa taarifa lakni cha ajabu barua sio ya siri unauliza imepata wapi? Na wasi wasi kama hao wanaoajiliwa TFF kama wanaelewa administration.Kila la kheri.

    ReplyDelete
  16. Alichofanya Shaffih ni jambo la kawaida kwa watoa habari walio na weledi. Kutoa nakala ya barua kwenye 'public domain' kuhusu swala ambalo limechukua hisia za watanzania wengi huku upotoshaji wa wahusika wa TFF ukiwa umezidi kipimo. TFF walijifanya kutisha sijui tutafungiwa kimichezo serikali ikitoa muongozo lakini wapi, majibu na muongozo wa serikali ndio huo huo FIFA imepiga nyundo na pia kutoa mwanga mwingine wa matumizi "mabaya ya fedha". TFF ipo chini ya serikali kuu lakini viongozi wake walikuwa wanawahadaa Watanzania kama vile wao ndio wao na hakuna wa kuwaambia kitu. Kwa mtu makini ukifuatilia taarifa za mapato ya mechi za TFF wanazotoa kwenye vyombo vya habari na huku kwenye blogs kweli utasikitika jinsi matumizi yanavyopikwa ili malengo yao ya kuonesha kilichopatikana ni kidogo yatimie. Tatizo ambalo baadhi ya wachangiaji humu ndani hawajaligundua ni kwamba hiki ni kizazi kingine ambacho kinathubutu, kinaweza kufanya mabadiliko ya uozo wa uko walikotoka hao viongozi wa TFF wasiopenda ukweli na mabadiliko. Nchi hii bila vugu vugu la mabadiliko ya kifikra, kinadharia, kiitikadi haitaenda uko tunakotaka.
    FM

    ReplyDelete
  17. Big up shaffih kwa kuweka mambo hadharani!

    ReplyDelete
  18. ni ujinga kujadili ujinga lakini ni ujinga zaidi kujadili.ujinga kwa ujinga,Tenga badala ya kutumia muda uliobaki kuisaidia stars ifuzu word cup unatumia muda mwingi kujadili barua,unataka watanzania wakukumbuke kwa barua hiyo au mafanikio ya soka?

    ReplyDelete
  19. ingekua ni barua ya posa ya mwanao ndo ingekua siri na ungemtaka ndugu yetu atoe maelezo....bwana raisi aibu imekujaa....na kwa taarifa yako hata mtoto mdogo alikua anajua kitakachotokea hata kabla huo ujumbe wa FIFA kuja hapa nchini.....acha ujanja ujanja!....zinapatikana barua za ndani kabisa itakua hiyo ambayo ni ya kwetu kabisa..embu maliza mda wako uondoke zako bwana....

    ReplyDelete
  20. Hapa TFF wanataka kuwapumbaza wananchi juu ya swala la msingi lililopo hivi sasas na kuanzisha malumbano na waandishi wahabari kisa barua . Na Angetile osia kumbuka TFF sio mali yako na familia yako hiki ni chombo cha watanzania tuna kila sababu yakujua kila kinachoendelea hapo so acha vitisho vya kitoto we ni mtu mdogo sana huwezi kuzuia sisi kupata habari zinazoeandelea hapo TFF. Na hiyo mnafanya hivyo kutokana na mdudu mnayoyafanya hapo kwanza watanzania walipoteza nafasi ya msingi sana kukuchagua umekuwa kiongozi wakwanza kuongoza kitu usichokijua kucheza kwako mabonanza ndio uje uongoze chombo kikubwa kama hilki umetuharibia sana mpira wa tanzania...

    ReplyDelete
  21. Hivi kumbe kuna watanzania akili zao bado zinawaza upuuzi,ingekua ya siri ingekua na muhuri wa confidential,na ikumbukwe kua hata kama document ni confidential lakini ina masuala ambayo maamuzi yake yanabeba interest za public na muandishi akaona kwamba kuna haja ya jamii kuyajua anatakiwa kufanya hivyo kwakua ni jukumu lake,ile barua ina maelekezo ya wazi tu ya FIFA kwa TFF ikieleza namna wanavyotaka zoezi liendeshwe,hivi hilo ni jambo la siri?ku spot mapungufu na kutoa mwongozo hapo kuna kitu cha kuficha?Tenga aache ubabaishaji na nyie watu mnaokurupuka kumshambulia shafih eti code of conducts mnazijua hizo code of ethics nyie,acheni umburula,javan chela

    ReplyDelete
  22. TFF ya sasa siyo taasisi ya kihuni kama Shafii na wenzake wanavyotaka ionekane,au kama ilivyokuwa Enzi za Wambura na Ndolanga,tulishatoka huko M MUDA MREFU.Huu ni ujasiri wa kijinga ambao ni wajinga tu wanaoweza kukusifia kwa kuiba nyaraka zisizokuhusu na kuzisambaza kwa wasiohusika.Ukizisoma comments nyingi za hapo juu utabaini kwamba wachangiaji wengi wanaokusifia ni wale wenye upeo finyu wa ku-analyse issues. TFF hawajasema barua hiyo ni ya siri, kwani waandishi waliruhusiwa kuiona na kuisoma.Issue ni yeye Shafii kaipata wapi barua ya TFF ambayo ameandikiwa Tenga kwa jina na yeye hajapewa nakala.Umefika wakati sasa Tanzania itunge sharia ya kulinda taarifa za watu na taasisi ili kuwadhibiti makanjanja, kumiliki blog bado hakumfanyi mtu kuwa mwandishi wa habari na kujificha kwenye uhuru wa vyombo vya habari


    ReplyDelete