Search This Blog

Friday, May 10, 2013

ED WOODWARD MRITHI WA DAVID GILL NDANI YA MAN UNITED - ALIYE NYUMA YA MAFANIKIO YA KIBIASHARA YA MAN UNITED CHINI YA GLAZERS


Ni mtaalam wa zamani wa mambo ya uwekezaji kwenye benki na mtu muhimu nyuma ya uongozi wa familia ya Glazer, ndio yupo nyuma ya mafanikio ya kibiashara ya Manchester United.

Wakati Ed Woodward, 40, anaweza asiwe na jina kubwa, ameweza kujenga sifa wakati wa miaka yake nane ndani ya Old Trafford. 
Na kipindi kijacho cha kiangazi Woodward atachukua nafasi ya ofisa mkuu wa Manchester United David Gill mbaye atastaafu.
Akiwa amehusika kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha familia ya Glazer inainunua klabu hiyo mwaka 2005, Woodward amekuwa mtu muhimu ndani ya klabu hiyo tangu wakati huo.

Akiwa kama msaidizi wa Gill, muingereza huyo amekuwa na jukumu la kuhakikisha mbinu za biashara za United zinakuwa bora, baada ya kuondoka kwa Gill 30 June, ataingia katika majukumu ya kisoka zaidi, yakiwemo masuala ya usajili na uhamisho  pamoja majadiliano ya mishahara ya wachezaji.
Ed Woodward

Woodward anasifika sana kwa kuweza kufanikisha kupatikana kwa dili za mikataba mingi ambayo ilisababisha ongezeko kubwa la faida ndani ya miezi mitatu iliyopita - United wakitangaza faida ya £91 millioni kutoka mwezi January. 
 Kuanzia 2014, dili lingine kama la Chevrolet litaiwezesha United kulipwa na kampuni hiyo ya magari ya Marekani kiasi cha £51m kwa mwaka kutokana na udhamini wa jezi pekee yake.

Jukumu la kuiongoza United linaweza kuonekana kama kitu ambacho hakikutegemewa kwa mhitimu huyo wa fizikia wa Bristol University, japokuwa Woodward alianza kazi hiyo ya masuala ya uongozi huko PricewaterhouseCoopers akiwa kama mhasibu na mshauri wa masuala ya kodi mwaka 1993.
Mwaka 1999 alihamia JP Morgan, ambapo alifanya kazi kama ofisa mkuu wa masuala ya uwezekezaji katika masuala ya biashara za kimataifa.
Na mahala hapo ndipo alipokutana na Malcom Glazer n kumshauri ainunue Manchester United, na mwaka 2005 aliitwa kuajiriwa na United chini ya Glazers.
Mwanzoni alipewa jukumu la upangaji wa masuala ya fedha, kabla hajapewa jukumu la kuendesha biashara na masuala yote ya media ya Manchester United mwaka 2007 na baadae mwaka jana akawa mkurugenzi.

Woodward alikuwa hana uzoefu wowote wa kufanya kazi kwenye taasisi ya kimichezo kabla hajaja United, lakini alianza kuhudhuria vikao vya wana hisa wa premier league kwa pamoja na Gill mwaka 2012 katika jaribio la kumuongezea uelewa kuhusu siasa za soka.

Jukumu lake jipya litamfanya afanye kazi kwa karibu na Sir Alex Ferguson na mrithi wake David Moyes katika kuifanya brand ya Manchester United inafanikiwa kibiashara na kisoka kama ilivyokuwa chini ya David Gill.

No comments:

Post a Comment