Search This Blog

Monday, April 15, 2013

YANGA YAONDOKA LEO KWENDA TANGA KUWAPIGISHA KWATA MGAMBO JKT

KLABU ya Yanga imeondoka leo Jumatatu kuelekea mjini Tanga kwa ajili ya mchezo wake wa ligi Kuu Bara dhidi ya Mgambo JKT ya Handeni utakaopigwa kesho (Jumatano) Uwanja wa Mkwakwani.
Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Lawrance Mwalusako amethibitisha kwa timu hiyo kuwa imeondoka leo (Jumatatu) mchana na wachezaji wake wote akiwa na walio majeruhi.
Yanga ambayo inaongoza ligi kwa pointi 52 kibindoni huku ikiwa imesaliwa na mechi nne, inahitaji pointi sita tu kufikisha pointi 58 kutawazwa mabingwa wapya wa ligi.
Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye ligi na pointi 47 iwapo itashinda mechi zake tatu zilibaki itagomea kwenye pointi 56.
Kocha wa timu hiyo, Ernest Brandts amesema kikosi chake kwa sasa kinakabiliwa na majeruhi Juma Abdul, Didier Kavumbagu walioumia katika mchezo Oljoro JKT wikiendi iliyopita.
Lakini amevuta pumzi kwa kurejea kundini wachezaji Jerry Tegete, Stephano Mwasika, Omega Seme na Salum Telela ambao walikuwa majeruhi.
"Tunacheza ugenini. Nadhani Mchezo utakuwa mgumu na ushindani mkali. Pia, wachezaji wanatakiwa kufahamu kila mechi kwetu ni kwa sasa ni kama fainali."
Alieleza kuwa hakuna timu ambayo itakubali kufungwa kirahisi kutokana na hali halisi ya mambo ilivyo kwa sasa.
"Kila timu inataka kushinda. Kama si kutwaa ubingwa basi ni kujiweka katika nafasi nzuri kutoshuka daraja." alisema Brandts. 

2 comments:

  1. Acha tukawale mgambo huko kwao. Kila la kheri Yanga.
    Na Uwanja tunataka ujengwe haraka.

    ReplyDelete
  2. Yanga wawe makini na fitna za nje ya uwanja,pia wajiandae kukabiliana na mazingira mabovu ya uwanja hususan pitch na ikibidi waende na viatu vya kukabiliana na hali ya majimaji iwapo mvua itanyesha kwani uwanja ni mbovu.Mbinu ya kufunga mabao ya mapema ili kuwanyongonyeza wapinzani itumike kama ilivyokuwa dhidi ya Oljoro.Aidha katika mzunguko wa kwanza tulipokwenda Tanga kucheza na Coastal Union basi letu lilipigwa mawe njiani na kuvunjwa kioo hivyo tujiandae na hujuma hii

    ReplyDelete