Search This Blog

Monday, April 15, 2013

KUHOFIA UPANGAJI WA MATOKEO LIGI KUU: TOTO YAOMBA MECHI ZAO ZISOGEZWE MBELE

UONGOZI wa Toto African ya Mwanza umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kusogeza michezo yake miwili kwa ajili ya kuhofia upangaji matokeo.
Katibu Mkuu wa timu hiyo, Salum Kaguna amesema jijini Dar es Salaam kuwa wameliandikia barau TFF kutaka mechi hizo zisogezwa.
"Tunafikiri iwapo tutamaliza ligi kabla ya timu nyingine, wanaweza kutumia mwanya huo kupanga matokeo."
"Kwa hiyo, tunaitaka TFF kuhakikisha mechi zetu mbili zinasogezwa mbele ili kuleta usawa wa timu zote kumaliza ligi kwa pamoja." alisema Kaguna.
Alisema iwapo timu hiyo itamaliza mechi zake mapema, timu za African Lyon, Polisi Moro na JKT Ruvu ambazo zipo kwenye hati hati ya kushuka daraja sawa na Toto African zinaweza kutumia nafasi hiyo kupanga matokeo kujinusuru na mkasi huo.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi ya TFF inaonyesha kuwa Toto African itacheza mechi yake kesho dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza na kumalizia na Ruvu Shooting ya Pwani.

1 comment:

  1. Toto wako sahii.Hakuna ligi duniani ambayo katika hatua kama hizi za mwishoni kuna timu zimebakiza mechi mbili huku timu zingine zimebakiza mechi nne hadi tano.Aidha Simba katika wiki tatu wamecheza mechi tatu tu na baada ya mechi na Azam wanapumzika tena kwa wiki nzima ndio wacheze mechi inayofuata,huku Yanga wakilazimika kucheza mechi tatu ndani ya siku nane kwani wakitoka Tanga wanarudi Dar Jumamosi kucheza na JKT Ruvu.Huku ni kuua ushindani katika ligi.

    ReplyDelete