Chama cha soka cha Afrika mashariki na kati (Cecafa)
kimethibitisha kwamba eneo lilogubikwa na vita la Darfur liliopo magharibi mwa Sudan ndio litakuwa mwenyeji wa michuano ya CECAFA Cup maarufu kama Kagame Cup mwezi june mwaka huu.
Chama hicho kimesema kwamba timu ya kimethibitisha kwamba timu kutoka Congo ya St. Eloi Lupopo itashiriki kwenye michuano hiyo.
Katibu mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema mpaka sasa timu kutoka Eritrea haijatoa taarifa kama itashiriki.
Musonye yupo Darfur akikagua miundo mbinu na ameripoti kwamba asilimia 90 ya eneo hilo ipo tayari kwa ajili ya kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa Afrika Mashariki na kati.
"Viwanja viwili vya Al Fashir - Al Nuggaa [chenye uwezo wa kubeba watu 15,000] na Al Fashir [45,000] - vimeonekana kuwa na ubora mzuri huku hotel na usafiri pia ukiwa kwenye hali nzuri," alisema.
Darfur imekuwa na machafuko ya kisiasa tangu mwaka 2003 lakini hivi karibuni kumekuwepo na makubaliano ya amani hivyo vurugu zimepungua.
Michuano hiyo inategemewa kuanza June 15 na itashirikisha washindi wa wa juu wa ligi za mataifa wanachama wa CECAFA.
KLABU ZITAZOSHIRIKI
Young Africans (Tanzania - Mabingwa watetezi), Simba (Tanzania Mainland), Zanzibar representatives, El Merriekh, Al Hilal (Sudan), Tusker (Kenya), Express (Uganda), APR (Rwanda), Vital'O (Burundi), Ports (Djibouti), Elman (Somalia), South Sudan representatives and St George (Ethiopia).
I am surprised and questioning someone's smartness in the mind.....
ReplyDeletesijakusoma hapo mwandishi Simba wanaenda kushiriki kwa kigezo kipi...?
ReplyDeleteAu ya kipindi kile waziri wa michezo akilwa kapuya...?
Sımba anashırıkı kama bıngwa wa bara last season na yanga kama bıngwa mtetezı wa afrıca masharıkı na katı last year.
ReplyDeletehata mimi sijaelewa simba kwa kigezo gani na sijaiona azam hapo
ReplyDeleteVipi mbona Azam hawapo?Au mnachukua msimamo wa ligi ya mwaka juzi?
ReplyDeleteSielewi hao Wachovu Lunyasi wanaenda kwa nafasi gani?????
ReplyDeleteCyril Komba unaonesha kuwa una uelewa mdogo katika masuala ya soka.Simba watakuwa wanaiwakilisha nchi kama bingwa wa Tanganyika na Yanga wanakwenda kama bingwa mtetezi kutetea taji walilolitwaa hapa Dar msimu uliopita.Sometimes kama hujui jambo ni vizuri kuuliza ili upate kueleweshwa na sio kukurupuka tu na kuponda.
ReplyDeleteENDAPO YANGA ITAFANIKIWA KUTWAA KOMBE HILI ITAKUWA IMEFANIKIWA KWA MAMBO YA
ReplyDeleteFUATAYO
1.KUTWAA KOMBE HILO KWA MARA YA TATU MFULULIZO NA KULICHUKUA MOJA KWA MOJA NA KUWEKA HISTORIA YA KUWA TIMU YA KWANZA TANZANIA KUCHUKUA KOMBE HILO MARA TATU MFULULIZO NA MOJA KWA MOJA.
2.KUFIKIA REKODI YA SIMBA YA KUCHUKUA UBINGWA HUO MARA SITA
Ndio effects za copy n paste
ReplyDeletekwa maswali yaliyokuwa yanaulizwa na MASHABIKI WA Yanga kwa nini SIMBA kashiriki inaonyesha nikiasi gani walivyo MASHABIKI yaani hawana records wala siyo WAPENZI wa soccer ila ni MASHABIKI wa team flani flani,kwa nini usiulize Yanga anashiriki kama Mtetezi wa nini???Basi kwa taharifa yenu SIMBA anashiriki kwa sababu msimu uliopita alichukua ndoo na kumpiga Yanga 5-0(Nunge)!mnataka kujifanya mmesahau eeeh!vp nyie vilaza wa soccer mmeisoma???
ReplyDeleteHao wanaohoji uwepo wa Simba huko Kagame, si ndio kizazi cha Facebook, hawajui hata hayo mashindano yanashirikisha washindi wa aina gani??
ReplyDeleteKibaya zaidi hawajui lakini wanajifanya wanajua, mwingine anamuambia Shaffih eti hayo ndio madhara ya kucopy and paste, kumbe hajui yeye ndio kilaza....!
Kwa taarifa yenu mashindano ya Kagame hushirikisha bingwa wa nchi aliyepita na sio current kama sasa, unaweza kuona kama kuna coincedence kwani tayari Yanga ni bingwa, na unaweza kumuona kama bingwa aliyepita, lakini hii imetokana na baada ya kubadilisha calendar kwani zamani ligi ilikuwa ikichezwa mwaka mzima(Jan-Dec), sasa kwa mfumo huo mpaka sasa tungekuwa hatuna bingwa, na bingwa ambaye anapaswa kushiriki Kagame anakuwa wa msimu uliopita, ambaye ni Simba! Yanga mwaka huu anashiriki kama bingwa mtetezi!!
Sasa kwa kuwa ligi siku hizi inachezwa August mpaka May, kwa unajikuta una mabingwa wawili at a time, lakini anayeenda Kagame huwa ni wa msimu uliopita!
Labda Calendar ya Kagame inabidi ibadilishwe ili zisiwe zinapishana na Calendar za ligi husika, challenge waliyonayo ni kwamba wakati wa Kagame nchi nyingine za Afrika Mashariki ligi huwa zinaendelea, wakati ya ligi ya bongo huwa imemalizika!!