Search This Blog

Tuesday, April 30, 2013

REAL MADRID VS DORTMUND: JE MADRID WATAWEZA KUBADILI MATOKEO KAMA ILIVYOKUWA KWENYE MICHEZO HII

Los Blancos wana deni mikononi mwao usiku wa leo kubadilisha matokeo ya 4-1 dhidi ya  Borussia Dortmund katika usiku wa ligi ya mabingwa wa ulaya. 
Kikosi cha Jose Mourinho kinaweza kikapata nguvu kwa historia nzuri ya klabu hiyo katika kubadilisha matokeo, Madrid wamekuwa na historia nzuri ya kufanya maajabu baada ya kupoteza mechi ya kwanza ya hatua ya mtoano na kuweza kufuzu kuendelea hatua inayofuata.

Tukielekea usiku wa leo tuangalie mechi 5 ambazo Madrid waliushangaza ulimwengu kwa kugeuza matokeo na kuendelea mbele katikaa michuano ya ulaya.

Real Madrid 5-1 Derby County (Agg 6-5, 1975-76 European Cup Raundi ya Pili)




Hat-trick kutoka kwa Charlie George katika mechi ya kwanza katika uwanja wa Derby iliisadia timu hiyo ya England kushinda  4-1 na wakaelekea jijini Madrid wakiwa kifua mbele kwa matokeo mazuri.

Japokuwa, ndani ya dakika 2 za mchezo wa pili ndani ya Santiago Bernabeu, Madrid walikuwa mbele kwa goli la Roberto Martinez, na mhispania huyo alienda na kufunga tena na kufanya ubao kusomeka 2-0 mpaka wakati wa mapumziko.

George akafunga goli kwa upande wa Derby dakika ya 60 baada ya Santillana alipoongeza idadia ya magoli ya Madrid, kabla ya Pirri hajafunga bao la nne dakika 5 kabla ya mchezo kumalizika hivyo kuepelekea ngoma kuendelea kwenye dakika 30 za ziada.

Katika dakika ya 100, Santillana akafunga goli la ushindi na kuufanya uwanja wa Bernabeu kulipuka kwa furaha kwa timu yao kuendelea mbele.

Real Madrid 3-0 Celtic (Agg 3-2, 1979-80 European Cup robo fainali)



Timu tena kutoka Uingereza ilienda tena Bernabeu wakiwa tayari wameshashinda mechi ya kwanza kwa ushindi wa 2-0 waliopata jijini Glasgow, shukrani kwa mabao ya George McCluskey na Johnny Doyle, lakini wiki mbili baadae wakiwa na kiungo ambaye ni sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Spain - Vicente del Bosque wakafanya yasiyotegemewa.

Santillana kwa mara nyingine walikuwa kwenye listi ya wafungaji wa Madrid, akifunga goli la kwanza katika ushindi wa 3-0 ambao uliwapeleka kwenda kucheza nusu fainali ya Komb la ulaya.

Real Madrid 6-1 Anderlecht (Agg 6-4, 1984-85 Uefa Cup Raundi ya 3)



Baada ya kufungwa 3-0 huko Belgium, Madrid walihitaji ushindi wa mabao 4-0 au zaidi kwenye dimba la Bernabeu, na kwa bahati nzuri walikuwa na mtu ambaye alipewa jina la utani la  El Buitre aka Emilio Butragueno.

Mshambuliaji huyo ambaye sasa ni mkurugenzi wa Real Madrid, alifunga hat trick, huku Manuel Sanchis akifunga bao moja na   Jorge Valdano akifunga mawili na kukamilisha ushindi wa 6-1 dhidi ya Anderletch

Real Madrid 3-0 Inter (Agg 3-2, 1984-85 nusu fainali ya Uefa Cup )



Miezi minne baada ya kuwafunga 6-1 Anderlecht, Madrid tena alikuwa kwenye mtihani mgumu wa kuweza kusonga mbele katika michuano ya ulaya, safari hii ilikuwa kwenye nusu fainali ya Uefa Cup.

Inter waliwatungua 2-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa  San Siro lakini kama ilivyokuwa Anderlecht, dakika tisini za mchezo wa pili ndani ya Bernabeu zilikuwa mbaya kwa waitaliano hao - hata mshambuliaji wa wa Madrid Juanito aliwaonya Inter kabla ya mchezo kwamba "Dakika 90 ndani ya Bernabeu zitakuwa kama miaka 9 kwao," na alikuwa sahihi.

Mpaka kufikia mapumziko matokeo yalikuwa sare -  Santillana alifunga mabao mawili na kugeuza matokeo - kabla ya goli la  Michel broke likawapa maumivu makubwa Nerazzurri.

Real Madrid 4-0 Gladbach (Agg 5-5, 1985-86 Uefa Cup raundi ya 3)



December 1985, Madrid waliwakaribisha Borussia Monchengladbach katika mechi ya pili ya raundi ya 3 ya UEFA Cup, wakijua kwamba wanatakiwa kushinda japo kwa mabao manne au zaidi ili kugeuza matokeo.

Ilionekana kama wajerumani wangeweza kufuzu baada ya kushinda 5-1 waliopata North Rhine-Westphalia lakini wakafungasha virago baada ya los Blancos kuwafunga mabao 4-0 na kuendelea mbele kwenye robo fainali.

Wauaji wawili wa Madrid Jorge Valdano na Santillana walikuwa kwenye fomu ya hatari, wote wakifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 4-0.


HII NI HISTORIA LAKINI JE AKINA RONALDO WATAWEZA KUFUATA NYAYO ZA AKINA JORGE VALDANO NA SANTILLANA? TUSUBIRI MAJIBU LEO SAA 3:45

No comments:

Post a Comment