KLABU
ya Yanga na Kocha Msaidizi wa timu ya Toto Africans, Athuman Bilali
wamepigwa faini ya sh. 500,000 kila mmoja kutokana na makosa mbalimbali
katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoendelea nchini.
Adhabu
hizo zimetolewa na Kamati ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) iliyokutana Jumapili (Aprili 7 mwaka huu) jijini Dar es
Salaam kupitia ripoti za waamuzi na makamishna kwa michezo namba 108
hadi 171.
Yanga
imepigwa faini hiyo baada ya kupata kadi tano za njano katika mechi
dhidi ya Kagera Sugar iliyochezwa Februari 7 mwaka huu. Vilevile Kagera
Sugar imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao
cha maandalizi ya mechi (pre match meeting) dhidi ya African Lyon
iliyochezwa mjini Bukoba, Februari 23 mwaka huu.
Naye
Kocha Bilali amepigwa faini hiyo na kufungiwa mechi tatu za ligi hiyo
kwa kumshambulia kwa maneno kocha wa timu pinzani, hali iliyosababisha
mwamuzi amtoe kwenye benchi la wachezaji. Alifanya tukio hilo kwenye
mechi kati ya Toto Africans na Tanzania Prisons iliyochezwa Aprili 3
mwaka huu jijini Mwanza.
African
Lyon na Simba zimepigwa faini ya sh. 500,000 kila moja kwa kushindwa
kuchezesha timu zao za U20 kwenye mechi za utangulizi wakati zilipocheza
na Oljoro JKT na Coastal Union, Machi mwaka huu kwenye viwanja vya Azam
Complex na Uwanja wa Taifa.
Suala
la Meneja wa Coastal Union, Akida Manchai kumshambulia kwa maneno
yasiyo ya kiungwana Makamu Mwenyekiti wake Steven Mnguto baada ya kwenye
mechi kati ya African Lyon na Coastal Union iliyochezwa Machi 30 mwaka
huu Uwanja wa Azam Complex limepelekwa Kamati ya Nidhamu kwa ajili ya
hatua za kinidhamu.
Adhabu zote zimetolewa kwa mujibu wa Kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom.
POLISI KUJIULIZA KWA RUVU SHOOTING VPL
Polisi
Morogoro inapambana na Ruvu Shooting katika moja kati ya mechi tatu za
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zitakazochezwa kesho (Aprili 10 mwaka huu).
Matokeo ya mechi hiyo yanatarajia kutoa mwanga kama Polisi inaweza
kubaki kwenye ligi hiyo msimu ujao.
Timu
hiyo itakuwa nyumbani Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro katika mechi
hiyo itakayochezeshwa na Ibrahim Kidiwa kutoka Tanga akisaidiwa na
Godfrey Kihwili na Ephrony Ndissa wa Arusha.
Polisi
Morogoro inayonolewa na Adolf Rishard inakamata nafasi ya mwisho ikiwa
na pointi 18 tu na imebakiza mechi tatu dhidi ya Simba, Kagera Sugar na
Coastal Union.
Mechi
nyingine za kesho ni kati ya Tanzania Prisons iliyo nafasi ya 12 ikiwa
na pointi 20 dhidi ya Mgambo Shooting. Mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es
Salaam ndiye atakayechezesha mechi hiyo kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine jijini Mbeya. Mgambo ina pointi 24 na iko katika nafasi ya tisa.
Mwamuzi
Said Ndege wa Dar es Salaam atachezesha mechi kati ya wenyeji Mtibwa
Sugar na Toto Africans itakayofanyika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani
mkoani Morogoro. Toto Africans ya Kocha John Tegete ina pointi 21 ikiwa
nafasi ya 11 wakati Mtibwa Sugar iko nafasi ya tano na pointi zake 32.
Ligi
hiyo itaendelea keshokutwa (Aprili 11 mwaka huu) kwa mechi moja kati ya
Azam na African Lyon itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex.
KAMATI YAZIPONGEZA ASHANTI, MBEYA CITY, RHINO
Kamati
ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezipongeza
timu za Ashanti United ya Dar es Salaam, Mbeya City ya Mbeya na Rhino
Rangers ya Tabora kwa kupanda Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao
(2013/20114).
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Wallace Karia amezitaka timu hizo kufanya maandalizi ya
kutosha ili ziweze kushindana katika VPL ikiwemo kutimiza masharti ya
kuwa klabu za Ligi Kuu.
Moja
ya masharti ya klabu zenye hadhi ya Ligi Kuu ni kuwa na timu ya pili
(U20) ambayo itakuwa na inacheza mechi za utangulizi kwenye uwanja wa
nyumbani kila timu ya wakubwa inapocheza.
Mbali
ya kuthibitisha timu hizo tatu kupanda daraja, pia Kamati ya Ligi
imethibitisha rasmi timu tatu zilizoshuka daraja kurudi Ligi ya Mkoa
katika mkoa husika. Timu zilizoshuka kutoka Daraja la Kwanza (FDL) ni
Small Kids ya Rukwa kutoka kundi A.
Kundi B timu iliyoshuka ni Moro United ya Dar es Salaam wakati Morani FC ya Manyara yenyewe imeporomoka kutoka kundi C.
kufungwa kubaya sijasikia tena kuhusu man united man city. shafii
ReplyDelete