Katika kufuata nyayo za klabu nyingine kubwa duniani klabu ya TP Mazembe imefungua duka kubwa la kuuza bidhaa mbalimbali zenye nembo ya timu hiyo. Duka hilo limefunguliwa siku ya Alhamisi iliyopita na kwa ajili ya wapenzi wa klabu hiyo ambao watapata nafasi ya kununua bidhaa halisi za TP Mazembe.
Uzinduzi huo ambao ulifanyika siku kadhaa kabla ya mechi dhidi ya Mochudi siku ya Jumapili, na walianza kwa kuuza jezi, kofia, na t-shirts zenye nembo ya timu hiyo na washabiki wa timu hiyo walijazana kwenye duka hilo kubwa kuisapoti timu yao kwa namna nyingine.
Hatua hii ya kibiashara ya TP Mazembe ambayo ina wachezaji wawili wa kitanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu inazidi kuifanya klabu hiyo kuviacha mbali vilabu vingine vilivyolala usingizi wa pono katika kusaka maendeleo barani Afrika kama Simba na Yanga ambavyo ni moja ya vilabu maarufu na vikongwe sana ndani ya bara hili la Afrika.
Uzinduzi huo ambao ulifanyika siku kadhaa kabla ya mechi dhidi ya Mochudi siku ya Jumapili, na walianza kwa kuuza jezi, kofia, na t-shirts zenye nembo ya timu hiyo na washabiki wa timu hiyo walijazana kwenye duka hilo kubwa kuisapoti timu yao kwa namna nyingine.
Caps na Tshirts za Mazembe
jamani samahani kama nitakuwa nimekosea tuwaalike kwa kuwaomba wafunguea hayo maduka na huku kwetu ili tuzitamanishe klabu zetu kuwa haya mambo yanawezekana na icwe 2 mradi wa mpira pesa na manji bali uwe mradi wa timu... na ningekuwa na uwezo ningeomba uwakala wa kuuza bidhaa zao ni shindane na zizou fashion na c hiz klab za cmba yanga azam na nyinginezo cuz hawamfikii hata zizou hata kama anauza jez za wa2 cuz wao wameshindwa fanya yaoooo big up mazembe endeleen kuvunja ma rekod afrika
ReplyDeleteAkili yako imechoka kufikiri sasa nakushauri umuombe blogger afute maoni yako hapo juu!! Ishiiii! Lengo la hii habari ni kuzipa changamoto YANGA na SIMBA ni kuzionyesha uchumi wanaukalia wakati wana mashabiki lukuki! Ama sivyo timu zetu kubwa zitaishia kuwasujudia matajiri njaa wachache ambao nao wanazihitaji hizi kupata umaarufu kupitia YANGA na SIMBA.umeelewa baba!!
ReplyDeleteYanga na Simba wanaweza kuingia mikataba na wazalishaji wa vifaa vya michezo vinavyohusiana na timu hizo.Baada ya hapo wanaweza kufungua duka moja moja katika maeneo ya Makao Makuu ya Klabu, Uwanja wa Taifa(mobile kwa siku za mechi tu),Kariakoo,Ubungo,Mwenge na Buguruni kwani maeneo hayo yana watu wengi na mengine ndio njia ya kuelekea uwanjani siku za mechi. kuajiri mtaalamu wa masoko atakayefanya kazi chini ya Katibu Mkuu.Haya mambo yanawezekana kama watu watajicommit na kuachana na uzamani.Kila siku tunashuhudia vifaa hivyo vyenye logo za timu hizo vikiuzwa kwa wingi Uwanja wa Taifa na kuwanufaisha wajanja wachache huku vikiwa na ubora hafifu.
ReplyDeleteklabu inayoweza kufanya kama tp mazembe ni azam peke yake kwa sababu wao nafikiri wanatoa kwa mtengenezaji wao. hizi klabu zingine hazivai jezi original kwa mfano simba na yanga wanavaa jezi za uhlsport lakini ukienda kwenye tovuti ya uhlsport hawajaorodheshwa. unaweza kuuza vifaa kama jezi kama unazovaa ni original. tp mazembe wameingia mkataba na adidas na ndio maana wanaweza kuuza jezi zenye logo ya adidas.
ReplyDeletemwakani mazembe wakicheza na yanga champion leugue wanayanga watanunua jezi za mazembe tena wakati simba inacheza na mazembe wanajangwani walizichangamkia jezi za mazembe kama njugu
ReplyDeleteila mwakahuu hawakuvaa jezi za libolo waliwaachia simba wahangaike nalo
ReplyDelete