Mshambuliaji yosso wa Yanga, George Banda amesema nafasi ambayo amepewa na kocha Ernie Brandts kucheza timu ya wakubwa atahakikisha anaitumia vizuri na kumpoteza, Jerry Tegete na Kavumbagu.
Banda ambaye amepandishwa kwenye kikosi cha timu ya wakubwa na kucheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Tusker ya Kenya na kuonyesha kiwango kizuri alisema;
"Nafikiri ni kama bahati kwangu kupandishwa timu ya wakubwa. Sikutegemea lakini naamini mwalimu amekubali uwezo wangu." alisema yosso huyo.
Banda ambaye amepandishwa toka timu ya vijana sambamba na winga Rehan Kibingu alisema; "Naahidi sintomwangusha mwalimu wangu. Nitafanya kila alichoniagiza ili kulipa fadhila zangu kwake na mashabiki wangu.
"Nafikiri bahati siku zote haiji mara mbili. Nitahakikisha naweka mkazo kwenye mazoezi na kujifunza kila kukicha ili niweze kufikia ndoto zangu nilizojiwekea katika medani ya soka."
Yosso huyo alisema hana cha kupoteza kwa sasa isipokuwa kujituma kwenye mazoezi na kujifunza mambo ambayo anafikiri yatamsaidi kuinua kiwango chake.
Katika hatua nyingine, Yosso huyo amediriki kusema anataka kuja kivingine na kumpoteza kabisa
Tegete. "Kazi yangu ni moja tu. Kucheza kwa kujituma na kufunga kila mechi ambayo nitapewa nafasi. Nafikiri kufanya hivyo nitampoteza Tegete." alisisitiza.
Kocha msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro alisema; "Banda ni mchezaji mzuri. Nafikiri tumeona uwezo wake na kumpandisha timu ya wakubwa pamoja na Kibingu (Rehani)"
Yosso hao walicheza dakika 45 za kwanza kwenye mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Tusker FC ya Kenya iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Januari mwaka huu ambapo Yanga ililala bao 1-0.
Shaffih, our players prolems are similar, I wish FIFA are the only one to solve it, George Banda's profile is incomplete and when you think critically his age and events are irrelevant! Confirm it please coz I've viewed it in his club's website.
ReplyDelete