TANZANIA itawakilishwa na wachezaji wawili tu katika fainali za Guiness Football Challenge zitakazofanyika Johannesburg, Afrika Kusini.
Nyota watakaopeperusha bendera ya Tanzania ni Daniel Msekwa na mwenzake Mwalimu.
Timu ya pili ya Tanzania ilitolewa wiki iliyopita na timu ya Kenya inayoundwa na Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi.
Timu ya pili ya Tanzania ilitolewa wiki iliyopita na timu ya Kenya inayoundwa na Kenneth Mukuri na Chris Mwamgi.
Kenya sasa itawakilishwa na timu tatu katika fainali za Pan African Challenge. Uganda na Tanzania
zitawakilishwa na timu moja kila moja.
Fainali za mashindano hayo sasa zitawashirkisha Watanzania Msekwa
na Mwalimu, washiriki kutoka Uganda Alex Muyobo na Ibrahim Kawoova pamoja na wenzao kutoka
Kenya, Francis Ngigi na Kepha Kimani, Kenneth Kamau na Wills Ogutuna Ephantus Nyambura na
Samuel Papa.
Hata hivyo, katika mwenendo wa mwanzo wa mashindano hayo, imegundulika kuwa rangi nyekundu
imekuwa na bahati kwa timu ya Kenya.
Timu za Kenya zimekuwa zikitumia rangi nyekundu katika muda wote wa mashindano hayo na zote
Timu za Kenya zimekuwa zikitumia rangi nyekundu katika muda wote wa mashindano hayo na zote
zimeng'ara. Timu hizo zilizofuzu kwa fainali hizo zitavaana na Ghana na Cameroun ili kuwania kitita cha Dola 250,000 (Sh milioni nne).
Washiriki katika mashindano hayo hushirikisha wachezaji wawili, ambao hupata nafasi ya kuonyesha
umahiri wao wa kumiliki mpira, kulenga shabaha kwa mashuti, kupiga penalti, kudaka na kujibu
maswali mbalimbali ya chemsha bongo.
No comments:
Post a Comment