SERIKALI imesema tangu Uwanja wa Taifa uanze kutumika Mwezi Agosti 2009 hadi February 2013 imepata makusanyo ya Sh1.533 bilioni.
Jumla hiyo ilitajwa jana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo, Amosi Makalla wakati akijibu kuhusu
kiasi gani cha fedha kilichopatikana katika uwanja huo.
Naibu Waziri alisema kuwa kiasi hicho ni asilimia 15 ya mapato
baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani (VAT), ambayo huingizwa katika mfuko mkuu wa Hazina.
Alikuwa akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu, Philipa Mturano (Chadema), aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu Manispaa ya Temeke kutonufaika na Mapato ya Uwanja wa Taifa, na kiasi cha fedha ambacho na manispaa hiyo imepata kiasi gani.
Makalla alisema Mapato yanayokusanywa kupitia VAT huwasilishwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).
Kuhusu Manispaa ya Temeke kunufaika, alisema halmashauri
hiyo hunufaika kutokana na mapato yatokanayo na matumizi ya uwanja wa Taifa ambayo huingia kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
Kwa mujibu wa Makalla, Mapato hayo ni asilimia 18 ambayo ni VAT inayokatwa kwa kila mchezo unaochezwa na kupelekwa TRA na pia gawio la asilimia 15 ambazo hukatwa kama ada ya matumizi ya uwanja ambapo mapato yote hayo hutumiwa na Serikali katika kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi wakiwemo wa Manispaa ya Temeke.
Mbali na fedha hizo, alikiwa alisema kuwa wananchi wa Temeke
wamekuwa wakinufaika na shughuli mbalimbali zinazofanyika uwanjani hapo ikiwemo wananchi kufanya biashara ndogo ndogo.
HIVI ILE MECHI YA STARS NA UGANDA ILICHEZWA MWEZI GANI MPAKA MAPATO YAANZE KUHESABIWA MWEZI AGOST?
ReplyDeleteuwanja ulianza kutumika 2009 au 2007, mbona kama hapa tunadanganyana!
ReplyDelete